Katibu Tawala wa Mkoa wa Simiyu, Bw. Jumanne Sagini (kushoto) akimkabidhi kofia Afisa Tarafa wa Dutwa, wilayani Bariadi Bi. Isabela Nyaulingo ikiwa ni ishara ya kumkabidhi pikipiki katika tukio la makabidhiano ya pikipiki zilizotolewa na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. John Pombe Magufuli kwa Maafisa Tarafa ambazo zimekabidhiwa Mei 08, 2020 Mjini Bariadi.
Katibu Tawala wa Mkoa wa Simiyu, Bw. Jumanne Sagini (kushoto) akimkabidhi ufunguo Afisa Tarafa wa Tarafa ya Busega, Bw. David Pallangyo wilayani Busega ikiwa ni ishara ya kumkabidhi pikipiki katika tukio la makabidhiano ya pikipiki zilizotolewa na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. John Pombe Magufuli kwa Maafisa Tarafa ambazo zimekabidhiwa Mei 08, 2020 Mjini Bariadi.
Katibu Tawala wa Mkoa wa Simiyu, Bw. Jumanne Sagini amewakabidhi pikipiki Maafisa Tarafa 15 wa Mkoa huo ambazo ni utekelezaji wa ahadi ya Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. John Pombe Magufuli aliyoitoa mwezi Mei 2019 wakati alipokutana na Maafisa tarafa wote nchini katika kikao kazi jijini Dar es Salaam.
Akiwakabidhi pikipiki hizo Mei 08, 2020 Mjini Bariadi Sagini amemshukuru Mhe. Rais kwa kutoa pikipiki hizo zitakazorahisisha utekelezaji wa majukumu ya Maafisa tarafa huku akiwaagiza kuzitunza na kuzitumia kwa malengo yaliyokusudiwa; ikiwa ni pamoja na kufuatilia mkakati wa elimu wa Mkoa wa kuwawezesha wanafunzi kusoma wakiwa katika likizo ya dharura ya tahadhari ya maambukizi ya Virusi vya Corona.
Tumeandaa mkakati wa mkoa wa kuwawezesha wanafunzi kusoma kipindi ambacho wako likizo ikiwa ni tahadhari ya maambukizi ya Virusi vya Corona; moja ya majukumu yenu katika kipindi hiki ni kuhakikisha mkakati unatekelezwa kwenye maeneo yenu ya utawala; walimu, maafisa elimu watatimiza wajibu wao nanyi pia mna sehemu yenu,”alisema Sagini.
Aidha, Sagini amewataka maafisa tarafa hao kuzitumia pikipiki hizi kwa kuwafikia wananchi wote wakiwemo wakulima hasa kipindi hiki cha mavuno na lengo kuu likiwa ni kuwaasa kutunza chakula.
Awali akisoma taarifa katibu tawala msaidizi utawalana rasilimaliwatu katika Ofisi ya mkuu wa Mkoa wa Simiyu, Bw. Ekwabi Mujungu amewataka maafisa tarafa hao kuzitumia pikipiki hizo kwa madhumuni yaliyokusudiwa ikiwa ni pamoja na kusukuma shughuli za maendeleo ya jamii ikiwemo kusimamia miradi ya elimu ,afya kilimo na hifadhi ya mazingira.
Wakati huo huo Mujungu ametoa maelekezo kwa makatibu tawala wa wilaya mkoani Simiyu kutenga fedha kwa ajili ya mafuta na matengenezo ya pikipiki hizo kwa kila tarafa ili pikipiki hizo ziweze kudumu kwa muda mrefu.
Akiongea kwa niaba ya maafisa tarafa mara baada ya kukabidhiwa pikipiki hizo afisa tarafa ya Dutwa , Isabela Nyaulingo amemshukuru Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. John Pombe Magufuli kwa kuwawezesha kupata usafiri huo ambao utarahisisha utendaji kazi wao huku akiahidi kuwa watazitunza na kufuata maelekezo yote waliyopewa na viongozi.
Jumla ya pikipiki 15 zimekabidhiwa kwa maafisa tarafa mkoani hapa zikiwa na thamani ya shilingi milioni 33,285,000/=, ambapo pikipiki moja inagharimu kiasi cha shilingi milioni 2,219,000.
Tarafa zilizonufaika mkoani Simiyu ni Dutwa, Nkololo na Muhango(BARIADI), Kivukoni na Busega(BUSEGA), Itilima, Kanadi, Bumela na Kinang'weli (ITILIMA) Mwagala,Sengerema,na Nung'hu( MASWA), Kisesa Nyalanja na Kimali (MEATU).
0 comments:
Post a Comment