Katibu Mkuu, Ofisi ya Waziri Mkuu
Kazi, Vijana, Ajira na Wenye Ulemavu Bw. Andrew Massawe akihutubia
wakati wa ufunguzi wa mkutano wa SADC wa wataalamu wa utatu sekta ya
kazi na ajira uliofanyika katika Kituo cha Kimataifa cha Mikutano cha
Julius Nyerere (JNICC), Jijini Dar es Salaam.
Sehemu ya wataalamu waliohudhuria
mkutano wa SADC wa utatu sekta ya kazi na ajira uliofanyika katika Kituo
cha Kimataifa cha Mikutano cha Julius Nyerere (JNICC), Jijini Dar es
Salaam.
Baadhi ya wajumbe wakisikiliza
hotuba ya Katibu Mkuu, Ofisi ya Waziri Mkuu Kazi, Vijana, Ajira na Wenye
Ulemavu Bw. Andrew Massawe (hayupo pichani) wakati wa ufunguzi wa
mkutano wa SADC wa wataalamu wa utatu sekta ya kazi na ajira.
Mkurugenzi wa Huduma za Kijamii na Rasilimali Watu Bi. Duduzile Simelane akieleza jambo wakati wa Mkutano huo.
Mkurugenzi wa Shirika la Kazi
Duniani (ILO) Kanda ya Afrika Mashariki, Bw. Willington Chibebe
akizungumza wakati wa mkutano huo uliowakutanisha wataalamu wa utatu
sekta ya kazi na ajira.
Baadhi ya wajumbe wakifuatilia
mada zilizokuwa zikiwasilishwa katika mkutano wa SADC wa wataalamu wa
utatu sekta ya kazi na ajira.
Watumishi Ofisi ya Waziri Mkuu
wakifuatilia mada zilizokuwa zikiwasilishwa katika mkutano wa SADC wa
wataalamu wa utatu sekta ya kazi na ajira uliofanyika katika Kituo cha
Kimataifa cha Mikutano cha Julius Nyerere (JNICC), Jijini Dar es Salaam.
Katibu Mkuu, Ofisi ya Waziri Mkuu
Kazi, Vijana, Ajira na Wenye Ulemavu Bw. Andrew Massawe (kushoto) kwenye
meza kuu akisikiliza taarifa ya Mkurugenzi wa Huduma za Kijamii na
Rasilimali Watu Bi. Duduzile Simelane (hayupo pichani). Kulia ni
Mkurugenzi wa Shirika la Kazi Duniani (ILO) Kanda ya Afrika Mashariki,
Bw. Willington Chibebe, Mwakilishi wa Vyama vya Kibiashara vya Nchi za
Kusini mwa Afrika (SADC) Bw. Michael Akuupa na Mwenyekiti wa Shirikisho
la Waajiri wa Nchi Wanachama wa Jumuiya ya Maendeleo ya Nchi za Kusini
mwa Afrika (SADC) Dkt, Aggrey Mlimuka
Katibu Mkuu, Ofisi ya Waziri Mkuu
Kazi, Vijana, Ajira na Wenye Ulemavu Bw. Andrew Massawe (wa tatu kutoka
kushoto) akiwa kwenye picha ya pamoja na wataalamu wa nchi wanachama wa
Jumuiya ya Maendeleo ya Nchi za Kusini mwa Afrika (SADC) waliohudhuria
mkutano wa utatu sekta ya kazi na ajira uliofanyika katika Kituo cha
Kimataifa cha Mikutano cha Julius Nyerere (JNICC), Jijini Dar es Salaam.
PICHA ZOTE NA OFISI YA WAZIRI MKUU
(KAZI, VIJANA, AJIRA NA WENYE ULEMAVU)
……………….
Na; Mwandishi Wetu
Wataalamu wa Sekta ya Kazi na
Ajira kutoka nchi wanachama wa Jumuiya ya Maendeleo ya Nchi za Kusini
mwa Afrika wamedhamiria kuboresha na kuendeleza sekta ya kazi na ajira
kwa kutatua changamoto zilizopo katika sekta hiyo.
Hayo yamebainishwa na Katibu Mkuu,
Ofisi ya Waziri Mkuu Kazi, Vijana, Ajira na Wenye Ulemavu Bw. Andrew
Massawe alipomwakilisha Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu
anayeshughulikia Sera, Bunge, Kazi, Vijana, Ajira na Wenye Ulemavu Mhe.
Jenista Mhagama katika ufunguzi wa mkutano SADC wa wataalamu wa utatu
sekta ya kazi na ajira na kueleza kuwa mkutano huo umewakutanisha kwa
wataalamu wa nchi wanachama wa SADC kwa ajili ya kuangalia namna ya
kuboresha sekta ya kazi na ajira ikiwemo sera ambazo zitachangia kwa
kiasi kikubwa kutatua changamoto ya ukosefu wa ajira.
“Mustakabali wa sekta ya kazi na
ajira unategemea jinsi ambavyo tunashughulikia fursa na changamoto
zitokanazo katika mazingira ya sekta hiyo, hivyo mada zitakazo jadiwa
katika mkutano huu zitatoa mwelekeo kwa wajumbe kuona namna ya kuwa na
sera rafiki za kazi na ajira,” alieleza Massawe
Alifafanua kuwa kulingana na
taarifa ya mwenendo wa ajira ulimwenguni ya mwaka 2019 iliyotolewa na
Shirika la Kazi Duniani (ILO) imeelezea hali ya ajira inayoonesha zaidi
ya watu milioni 170 hawana kazi ikiwa ni sawa na asailimia 5.1, na
wafanyakazi bilioni 2 wapo katika ajira isiyo rasmi ikiwa ni sawa na
asilimia 61.2.
“Ni matumaini yangu ajenda
zitakazo jadiliwa zitatoa mwelekeo wa namna bora ya kutatua changamoto
zilizopo sasa na mapendekezo yatakayotolewa na wataalamu kutoka nchi
wanachana yatakuwa yanazingatia vipaumbele na malengo endelevu katika
sekta ya kazi na ajira,” alisema Massawe
Sambamba na hayo alieleza kuwa
Serikali imeendelea kushirikiana na Shirika la Kazi Duniani (ILO) kwa
kutoa elimu ya sheria za kazi ili kuongeza uelewa kwa wananchi kufanya
kazi zenye staha na kuboresha mazingira ya kazi.
Akitolea mfano Ofisi ya Waziri
Mkuu inavyotekeleza Programu ya Taifa ya Kukuza Ujuzi ambayo imekuwa na
mchango mkubwa katika kuwezesha vijana ambao ndio nguvukazi ya taifa
wanavyoshiriki katika kufanya kazi za staha kupitia mafunzo wanayopatiwa
chini ya programu hiyo.
Kwa upande wake Mkurugenzi wa
Huduma za Kijamii na Rasilimali Watu Bi. Duduzile Simelane alieleza kuwa
ukuaji wa sayansi na teknolojia umechangia kwa kiasi kikubwa nchi
wanachama za SADC kukuwa kiuchumi hivyo kumekuwa na hitaji la kuwa na
miongozo sahihi, sera na sheria zitakazo wawezesha kushirikiana kwa
pamoja katika kukuza sekta ya kazi na ajira.
Naye, Mwenyekiti wa Shirikisho la
Waajiri wa Nchi Wanachama wa Jumuiya ya Maendeleo ya Nchi za Kusini mwa
Afrika (SADC) Dkt, Aggrey Mlimuka alisema kuwa ajenda zitakazojadiliwa
zitatoa fursa kwa nchi wanachama kuzingatia sheria, kanuni, taratibu na
miongozo kwa wafanyakazi ambao ni chachu ya ukuaji uchumi.
Mkutano huo unafanyika kwa siku
tano kuanzia tarehe 18 hadi 22 Novemba, 2019 na umeshirikisha wajumbe
kutoka nchi ya Angola, Botswana, Eswatini, Malawi, Msumbiji, Lesotho,
Afrika Kusini, Namibia na Zimbabwe. Wajumbe wengine kutoka Shirika la
Kazi Dunianai (ILO), SATUCC, SPSF, Chama cha Waajiri Tanzania (ATE),
Shirikisho la Vyama vya Wafanyakazi Tanzania (TUCTA), ZANEMA na ZATUC.
0 comments:
Post a Comment