Katibu Mkuu Wizara ya Afya,
Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Dkt. Zainab Chaula
akifungua Mkutano wa Makatibu Wakuu wa Wizara ya Afya kwa Nchi Wanachama
wa Jumuiya ya Maendeleo ya Kusini Mwa Afrika (SADC), ambao ni moja ya
vikao vya Mkutano wa Mawaziri wa Wizara hiyo kwa nchi za SADC, Mkutano
huo unaendelea katika Ukumbi wa Mikutano Benki Kuu ya Tanzania Jijini
Dar es Salaam.
Katibu Mkuu Wizara ya Afya,
Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Dkt. Zainab Chaula, akiwa
katika picha ya pamoja na Makatibu Wakuu na Wakuu wa Sekta ya Afya
Kutoka Nchi 16 za Jumuiy ya Maendeleo Kusini mwa Afrika (SADC) mara
baada yakufungua Mkutano wa Afya na UKIMWI unaoendelea katika Ukumbi wa
Mikutano Benki Kuu ya Tanzania Jijini Dar es Salaam.
Katibu Mkuu Wizara ya Afya,
Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Dkt. Zainab Chaula, akiwa
katika picha ya pamoja na Kamti ya Maandalizi ya Mkutano wa Mawaziri wa
Afya na UKIMWI kwa nchi Wanachama wa SADC mara baada yakufungua Mkutano
huo unaoendelea katika Ukumbi wa Mikutano Benki Kuu ya Tanzania Jijini
Dar es Salaam.
Makatibu Wakuu na Wajumbe wa
Sekta ya Afya kutoka nchi Wanachama SADC wakifuatilia ufunguzi wa
Mkutano wa Afya na UKIMWI wa Mawaziri Wizara ya Afya unaoendelea katika
Ukumbi wa Mikutano Benki Kuu ya Tanzania.
(Picha na Idara ya Habari-MAELEZO)
…………………..
Na. Paschal Dotto-MAELEZO.
Mkutano wa Mawaziri wa Nchi za
Jumuiya ya Maendeleo ya nchi za Kusini mwa Afrika SADC, Sekta ya Afya
umeanza rasmi Jijini Dar es Salaam kwa Kutanguliwa na Kikao cha Makatabu
Wakuu wa Wizara ya Afya kutoka nchi wanachama, huku ajenda 13 zikitajwa
kujadiliwa katika Mkutano huo uonafanyika katika Ukumbi wa Benki Kuu ya
Tanzania (BOT).
Akizungumza katika Ufunguzi
Katibu Mkuu Wizara ya Afya Maendeleo ya Jamii Jinsia Wazee na Watoto,
Dkt.Zainab Chaula amesema kuwa katika kati ya ajenda hizo 13, Kifua
Kikuu itakuwa ni ajenda ambayo italengwa zaidi kwani malengo ya nchi za
SADC ni kupunguza ugonjwa huo kwa kiasi kikubwa au kuufuta kabisa
ifikapo 2030.
“Ajenda kubwa kati ya zile 13
katika Mkutano huu ni ile ya kupunguza ugonjwa wa kifua kikuu au
kukomesha kabisa kwa nchi wanachama wa SADC, kwani malengo ya nchi hizi
16 ni kukomesha TB ifikapo mwaka 2030”, Alisema Dkt.Chaula.
Dkt.Chaula alisema kuwa ajenda
nyingine ni pamoja na kupambana na maambukizi ya virusi vya ukimwi,
masuala ya malaria, Afya ya mama na mtoto, chanjo ya mtoto, masuala ya
lishe bora, utapiamlo na viribatumbo, uimarishwaji wa mfumo wa Afya
hususani upatikanaji wa dawa na upatikanaji wa takwimu za Afya,
rasilimali watu, rasilimali fedha na masuala ya ununuzi wa dawa ambapo
Bohari Kuu ya Dawa kutoka Tanzania(MSD) inafanya kazi ya ununuzi na
kusambaza dawa kwenye nchi za kusini mwa Afrika.
Ili kutekeleza azma hiyo,
Mawaziri wa Sekta ya Afya kwa Nchi za SADC makatibu wakuu na wajumbe
mbalimbali tayari wameanza kuandaa ajenda hizo, na mwitikio wa
mahudhurio kwa wajumbe umekuwa mkubwa ambapo mpaka sasa ni asilimia 95.
Aidha Dkt. Chaula alisema
kuwa, Tanzania imepewa heshima ya kuwa wanunuzi na wasambazaji wa dawa
kwa nchi za SADC kwa hiyo Mawaziri watapata nafasi ya kutembelea Bohari
Kuu ya dawa pamoja na kiwanda Kikubwa cha viua dudu cha kibaha.
“Mawaziri kutoka Nchi
Wanachama wa SADC watapata fursa ya kutembelea kiwanda cha viua dudu
Kibaha, kwa kuwa uwezo wake sasa umekuwa ni mkubwa na mnajua sasa hivi
ajenda kama nchi ni kuhakikisha Tanzania inakuwa na uchumi wa kati wenye
viwanda, kwa hiyo kiwanda hiki pia kinatuwakilisha kwenye nchi hizi za
SADC”, alisema Dkt. Chaula.
Kwa upande wake Mkurugenzi
Mtendaji Tume ya Kudhibiti UKIMWI Tanzania (TACAIDS), Dkt. Leonard
Maboko amesema kuwa Tanzania imepiga hatua kubwa katika kukabiliana na
maambukizi ya Virusi vya UKIMWI baada ya kufanikisha kwa kiasi kikubwa
tohara kwa wanaume.
“Tunaingia na ajenda
tulizowekeana katika kipindi kilichopita, sisi Tanzania kuna eneo ambalo
tumefanya vizuri kuliko nchi zote za ukanda huu katika kupambana na
maambukizi mapya ya virusi vya UKIMWI eneo hilo ni tohara kwa wanaume,
kwa hiyo katika mkutano huu tutabadilishana uzoefu katika eneo la
mafanikio kwa kila nchi kwa nchi 16 za SADC”, Alisema Dkt. Maboko.
0 comments:
Post a Comment