METDO Tanzania

METDO Tanzania

Wednesday, July 24, 2019

MHE HASUNGA ATETA NA MADEREVA WA MALORI MKOANI SONGWE

Mbunge wa Jimbo la Vwawa mkoani Songwe ambaye ni Waziri wa Kilimo Mhe Japhet Hasunga akisisitiza jambo mbele ya wanachama wa chama cha Madereva wa Malori mkoani Songwe tarehe 24 Julai 2019 wakati alipokutana nao kwa ajili ya mazungumzo. (Picha Zote Na Mathias Canal, Wizara ya Kilimo)
Mbunge wa Jimbo la Vwawa mkoani Songwe ambaye ni Waziri wa Kilimo Mhe Japhet Hasunga akikabidhi mchango wake kwa Mwenyekiti wa  Chama cha Madereva wa Malori mkoani Songwe Ndg Deogratius Agripa tarehe 24 Julai 2019.
 Mbunge wa Jimbo la Vwawa mkoani Songwe ambaye ni Waziri wa Kilimo Mhe Japhet Hasunga akiwa katika picha ya pamoja na wanachama wa chama cha Madereva wa Malori mkoani Songwe tarehe 24 Julai 2019 wakati alipokutana nao kwa ajili ya mazungumzo.
Mbunge wa Jimbo la Vwawa mkoani Songwe ambaye ni Waziri wa Kilimo Mhe Japhet Hasunga akisisitiza jambo mbele ya wanachama wa chama cha Madereva wa Malori mkoani Songwe tarehe 24 Julai 2019 wakati alipokutana nao kwa ajili ya mazungumzo.

Na Mathias Canal, Wizara ya Kilimo-Songwe

Mbunge wa Jimbo la Vwawa mkoani Songwe ambaye ni Waziri wa Kilimo Mhe Japhet Hasunga leo tarehe 24 Julai 2019 amekutana na kufanya mazungumzo na madereva wa Malori mkoani Songwe ili kubaini changamoto zinazowakabili.

Katika mkutano huo uliofanyika katika ukumbi wa mikutano wa Chama Cha Mapinduzi katika eneo la Vwawa mkoani Songwe Mhe Hasunga amewahakikishia madereva hao kuwa serikali ya awamu ya tano inayoongozwa na Mhe Rais Dkt John Pombe Magufuli imejipanga vyema katika ujenzi wa miundombinu ili kuimarisha usafirishaji.

Alisema kuwa serikali inaendelea na mpango wake wa uboreshaji wa miundombinu zikiwemo barabara kubwa na ndogo ili kuongeza ufanisi wa magari yanayotumia barabara hizo kumaliza safari zao katika hali ya usalama.
Kadhalika madereva hao wamempongeza Mbunge huyo wa Jimbo la Vwawa kwa kuteuliwa na Mhe Rais Dkt John Pombe Magufuli kuwa waziri katika sekta muhimu ya kilimo hapa nchini kwani jambo hilo limeongeza heshima.

Walisema kuwa imani iliyoonyeshwa na Rais Magufuli kwa wananchi wa Vwawa na Mkoa wa Songwe kwa ujumla ni matokeo ya imani ya wananchi hao waliyoionyesha kwa mbunge huyo baada ya kumchagua kwa kishindo katika uchaguzi mkuu uliofanyika Octoba 2015.

Mhe Hasunga ameahidi kushirikiana na chama hicho cha madereva ili kutatua changamoto zinazowakabili.

MWISHO
Share:

0 comments:

Post a Comment

Copyright © WAZO HURU | Powered by Blogger Design by ronangelo | Blogger Theme by NewBloggerThemes.com