KAMPUNI ya Puma Energy Tanzania imesema
itaendelea kutoa elimu ya mafunzo ya usalama barabarani kwa shule za
msingi mbalimbali nchini ikiwa ni mkakati wake wa kupunguza ajali
nchini.
Pamoja na ahadi hiyo kampuni hiyo imetoa
mafunzo ya usalama barabarani kwa wanafunzi zaidi ya 4500 katika shule
tano za msingi katika Jiji la Dodoma kwa mwaka huu wa 2019 huku ikiahidi
kuendelea kutoa elimu hiyo na kufanya kazi kwa karibu na Serikali ili
kuhakikisha elimu hiyo inawafikia wanafunzi wengi zaidi ambao watakuwa
mabalozi kwa wengine.
Akizungumza leo Julai 25 jijini Dodoma
mgeni rasmi Naibu Waziri Ofisi ya Waziri Mkuu, Sera, Bunge, Ajira na
Vijana Athony Mavunde, Mkurugenzi Mtendaji wa Puma Energy Tanzania
Dominic Dhanah amesema programu hiyo ya mwezi mmoja kwa Dodoma
ilihusisha mafunzo ya usalama barabarani kwa walimu 15 na wanafunzi
4500, katika shule tano.
Amefafanua kulikuwa na shindano la
uchoraji wa michoro inayo hamsisha usalama barabarani ikiwa ni sehemu ya
mwendelezo wa kampeni iliyozinduliwa rasmi mwaka 2013 ambapo zaidi ya
shule 80 zimefikiwa huku wanafunzi 100,000 wakiwa wamepatiwa mafunzo
katika mikoa ya Dar-es-salaam, Geita, Ruvuma na Dodoma.
“Puma Energy Tanzania imeamua kuja jijini
Dodoma kwa sababu ya ukuaji wa haraka wa jiji hili ambapo shughuli za
kijamii na ongezeko la watu na magari ambayo yanahatarisha usalama wa
watoto wanapokwenda shuleni na kurudi nyumbani,”,amesema Dhanah na
kuongeza “Hadi sasa tumeweza kufundisha wanafunzi zaidi ya 4500 wa shule
tano za msingi zilizopo jiji la Dodoma”.
Dhahana amesema mafunzo hayo ya usalama
barabarani na uchoraji alama za barabarani ni kipaumbele kwa lengo la
kuwapa uelewa watoto hususani wa shule za msingi juu ya namna bora ya
matumizi ya barabara.
Alibainisha lengo ni kuwafanya watoto
kuwa na uelewa wa matumizi ya barabara ili kuongeza uelewa kuhusu dhima
nzima ya usalama barabarani kwa Watanzania.
“Lengo letu kama kampuni ni kuongeza wigo
ili kufikia shule nyingi zaidi nchi nzima. Puma Energy Tanzania
itaendelea kuwekeza katika kampeni ya usalama barabarani ikishirikiana
na serikali kupitia jeshi la Polisi ili kuokoa maisha ya watanzania,”
amebainisha.
Akieleza zaidi amesema unzo hayo
yametolewa na Kampuni ya Mafuta ya Puma Tanzania kupitia Shirika lisilo
la kiserikali la Amend ambapo elimu hiyo pia imetolewa kwa walimu 15 wa
shule hizo.
Awa upande wake Naibu Waziri, Ofisi ya
Waziri Mkuu Sera,Bunge,Kazi ,Ajira na Vijana Anthony Mavunde amesema
Puma Energy Tanzania ni kampuni iliyoamua kutoa elimu ya usalama
barabara nchini huku akitoa ombi kwa kampuni hiyo kufundisha walimu hizo
ili wakifundisha masomo ya kawaida wawe pia wanataka na elimu ya
usalama.
Amesema kwa kufanya hivyo inasaidia
kupunguza ama kumaliza kabisa ajali za barabarani huku akifafanua
Serikali itaendelea kuweka alama za usalama barabarani ili kuondoa
changamoto za ajali.
Amesema kuwa kutokea kwa elimu hiyo kwa
Jiji la Dodoma kunakwenda kutengeneza jamii yenye mabalozi wazuri katika
kutoa elimu ya usalama barabarani huku akieleza Dodoma ni ya pili kwa
mtandao wa barabara za lamo,hivyo ni muhimu elimu hiyo kuendelea
kutolewa.
“Nimesikia ombi la walimu na wanafunzi la
kuhitaji alama za barabarani, hivyo Serikali itaendelea kuweka alama
hizo.Pia nimezungumza na wenzetu wa Puma wamekubali kupaka rangi za
usalama barabarani na wataanza na shule tano ambazo zimepatiwa elimu hii
ya usalama barabarani,”amesema Mavunde
Wakati huo huo walimu wakuu katika shule
za msingi katika Jiji la Dodoma wametoa ombi la kuweka alama za
barabarani na hasa alama za pundamilia au matuta ili kuhakikisha
wanafunzi wanapovuka wanakuwa salama kwani barabara nyingi hazina alama
hizo.
Mwalimu Mkuu wa Shule ya Msingi General
Musuguri Beatrice Chidumizi amesema changamoto iliyopo kwenye eneo la
shule yao ni kukosekana kwa matuta au alama za barabarani, hivyo
wanalazimika kumuweka mtu wa kuvusha wanafunzi ambaye analipwa fedha.
“Changamoto kubwa iliyopo katika shule
yetu ni barabara yetu kutokuwa na matuta na alama za pundamilia,hivyo
tunaomba tuwekewe alama za barabarani kwa ajili ya usalama wa wanafunzi
wetu.Tunaishukuru Puma kwani imetusaidia sana kuwajengea uelewa
wanafunzi wetu na sasa wanafahamu cha kufanya wanaoutaka kuvuka
barabara.
“Tunaamini kupitia mafunzo haya
tutapunguza ajali kwa watoto wetu na watumiaji wengine wa barabara
zetu,”alisema Mwalimu Chidumizi na kuongeza kuwa umefika wakati kwa
elimu hiyo kuendelea kutokea kwa Jiji la Dodoma hasa kwa kuzingatia
Dodoma inakuwa kwa kasi kutokana na Serikali kuhamia Dodoma.
0 comments:
Post a Comment