Wakazi wa Kijiji cha Hanseketwa kilichopo kata ya Ihanda wakimlaki Mbunge wa Jimbo la Vwawa mkoani Songwe ambaye ni Waziri wa Kilimo Mhe Japhet Hasunga mara baada ya kuwasili katika kijiji hicho akiwa katika ziara ya ukaguzi wa miradi ya maendeleo jimboni humo. (Picha Zote Na Mathias Canal, Wizara ya Kilimo)
Sehemu ya wakazi wa kijiji cha Shilanga kilichopo kata ya Ihanda wakifatilia mkutano wa Mbunge wa Jimbo la Vwawa mkoani Songwe ambaye ni Waziri wa Kilimo Mhe Japhet Hasunga wakati akiwa katika ziara ya ukaguzi wa miradi ya maendeleo jimboni humo.
Mbunge wa Jimbo la Vwawa mkoani Songwe ambaye ni Waziri wa Kilimo Mhe Japhet Hasunga akisisitiza jambo wakati akizungumza na Katibu Tawala wa Mkoa wa Songwe Ndg David Kafulila mara baada ya kuwasili mkoani humo kw aajili ya ziara ya ukaguzi wa miradi ya maendeleo jimboni humo.
Sehemu ya wakazi wa kijiji cha Hanseketwa kilichopo kata ya Ihanda wakimsikiliza kwa makini Mbunge wa Jimbo la Vwawa mkoani Songwe ambaye ni Waziri wa Kilimo Mhe Japhet Hasunga wakati akiwa katika ziara ya ukaguzi wa miradi ya maendeleo jimboni humo.
Sehemu ya wakazi wa kijiji cha Shilanga kilichopo kata ya Ihanda wakimsikiliza kwa makini Mbunge wa Jimbo la Vwawa mkoani Songwe ambaye ni Waziri wa Kilimo Mhe Japhet Hasunga wakati akiwa katika ziara ya ukaguzi wa miradi ya maendeleo jimboni humo.
Na Mathias Canal, Wizara ya
Kilimo-Songwe
Mbunge wa Jimbo la Vwawa
mkoani Songwe ambaye ni Waziri wa Kilimo Mhe Japhet Hasunga amewahimiza
wananchi kujiandikisha kwenye daftari la mkaazi ili kupata fursa ya kuchagua
viongozi bora katika uchaguzi wa serikali za mitaa.
Mhe Hasunga ametoa wito huo
leo tarehe 24 Julai 2019 kwa wananchi wakati wa mikutano ya hadhara aliyoifanya
katika kijiji cha Ipapa, Ipanzya na Mpela katika kata ya Ipunga sambamba na
vijiji vya Maronji, Shilanga na Hanseketwa vilivyopo katika kata ya Ihanda.
Alisema kuwa uchaguzi wa serikali
za mitaa kwa ajili ya kuchagua wajumbe na wenyeviti wa Vitongoji, Vijiji na
Mitaa ni muhimu kwani ndio sehemu ya maandalizi ya uchaguzi mkuu
utakaowahusisha Madiwani, Wabunge pamoja na Rais.
Hivyo umuhimu wa wananchi
kujiandikisha ni sehemu ya kufanya maamuzi ya viongozi watakaowawakilisha
katika kipindi cha miaka mitano kwa ajili ya kuchochea shughuli za maendeleo.
Akizungumzia changamoto
zinazowakabili wananchi katika jimbo hilo ambazo kwa sehemu kubwa zimetajwa
kuwa ni pamoja na uboreshaji wa barabara, Zahanati na upatikanaji wa maji, Mhe
Hasunga alisema kuwa serikali ya awamu ya tano inayoongozwa na Mhe Rais Dkt
John Pombe Magufuli imejikita katika dhamira ya utatuzi wa changamoto hizo kwa
kipindi cha muda mfupi na malengo ya muda mrefu.
Alisema kuwa Uongozi wa Taasisi
itakayoshindwa kufikisha pembejeo kwa wakati na kukwamisha juhudi za serikali
katika kuongeza tija na uzalishaji wa mazao ya wakulima utachukuliwa hatua za
haraka ikiwemo kusimamishwa kazi.
Kadhalika Mhe Hasunga amepiga
marufuku kuzuia kwa kufunga mipaka ya biashara ya Mazao badala yake wananchi wametakiwa
kuuza popote watakapo.
MWISHO
0 comments:
Post a Comment