METDO Tanzania

METDO Tanzania

Monday, November 4, 2019

MHE MGUMBA ABAINISHA MKAKATI WA KUDHIBITI MARADHI YANAYOIKUMBA MIMEA YA MIPAPAI NCHINI

Naibu Waziri wa Kilimo Mhe Omary Mgumba (Mb) akijibu swali bungeni Jijini Dodoma leo tarehe 5 Novemba 2019 wakati wa mkutano wa kumi na saba.
Naibu Waziri wa Kilimo Mhe Omary Mgumba (Mb) akijibu swali bungeni Jijini Dodoma leo tarehe 5 Novemba 2019 wakati wa mkutano wa kumi na saba.

Na Mathias Canal, Wizara ya Kilimo-Dodoma

Serikali kupitia Wizara ya Kilimo imefanya utafiti na kugundua kuwa ugonjwa wa Ubwili unga ndio unaoathiri mipapai kwa kiwango kikubwa.

Baada ya kugundulika ugonjwa huo, Wizara ya kilimo imechukua hatua za kuudhibiti kwa kutumia viuatilifu vyenye viambata vya croripynfos (udhibiti wa kwenye udongo), Profenophos na Dichlorovosch (udhibiti kwenye majani). 

Aidha, njia nyingine ya uthibiti ni kwa kutumia mbinu bora za kilimo (Cultural Control) kwa kupanda miche wakati wa kiangazi ili mimea isishambuliwe ikiwa michanga, kupalilia shamba kwa wakati na kug’olea miche iliyoathirika na utumiaji wa wadudu marafiki (Biological Control).

Naibu Waziri wa Kilimo Mhe Omary Mgumba ameyasema hay oleo tarehe 5 Novemba 2019  bungeni Jijini Dodoma Wakati akijibu swali la Mheshimiwa Mbunge wa Viti Maalum Zainabu Mussa Bakari aliyetaka kufahamu serikali imechukua hatua gani kudhibiti maradhi katika mimea ya mipapai nchini ambayo yanahatarisha kupotea kwa mimea hiyo.

Amesema kuwa Serikali inaendelea kutoa elimu kwa wakulima kuhusu kufuata kanuni bora za kilimo ili kuepuka magonjwa mbalimbali yanayoweza kuathiri mimea ukiwemo mpapai.

Serikali kupitia Kituo cha Utafiti cha TARI-Horti TENGERU imeendelea kufanya utafiti magonjwa na wadudu wanaoathiri mazao ya bustani ikiwemo mipapai. Utafiti huo umegundua kuwa ugonjwa wa Ubwili unga unaoathiri mipapai unaosababishwa na vimelea vya kuvu (fungus) vijulikanavyo kitaalam kama Oidium caricae papaya.

Ameongeza kuwa Mipapai haiwezi kupotea nchini kwa kuwa tayari njia za kudhibiti      magonjwa na wadudu wanaoshambulia mimea hiyo zipo.

kadhalika, Wizara itaendelea kuwaelimisha wakulima na wadau mbalimbali juu ya udhibiti wa ugonjwa na wadudu wanashambulia mimea na mazao ikiwemo mipapai ili kuongeza uzaliahaji na tija.

   MWISHO
Share:

0 comments:

Post a Comment

Copyright © WAZO HURU | Powered by Blogger Design by ronangelo | Blogger Theme by NewBloggerThemes.com