Naibu Waziri wa Kilimo, Mhe. Omary Mgumba
(kulia) akikagua moja ya kitalu nyumba wakati wa ziara ya kukagua
maandalizi ya Maonesho ya Nanenane Kitaifa mwaka 2019 yatakayofanyika
kuanzia Julai 28, 2019 Viwanja vya Nyakabindi Bariadi.
Mtaalam kutoka JKT (kulia) akitoa maelezo
kwa Naibu Waziri wa Kilimo, Mhe. Omary Mgumba (katikati) wakati
akikagua moja ya tanki la ufugaji wa samaki wakati wa ziara ya kukagua
maandalizi ya Maonesho ya Nanenane Kitaifa mwaka 2019 yatakayofanyika
kuanzia Julai 28, 2019 Viwanja vya Nyakabindi Bariadi.
Naibu Waziri wa Kilimo, Mhe. Omary Mgumba
(kulia) akikagua baadhi ya vipando wakati wa ziara ya kukagua
maandalizi ya Maonesho ya Nanenane Kitaifa mwaka 2019 yatakayofanyika
kuanzia Julai 28, 2019 Viwanja vya Nyakabindi Bariadi.
Naibu Waziri wa Kilimo, Mhe. Omary Mgumba
(kulia) akipokea maelezo kutoka kwa Afisa wa JKT akikagua baadhi ya
vipando wakati wa ziara ya kukagua maandalizi ya Maonesho ya Nanenane
Kitaifa mwaka 2019 yatakayofanyika kuanzia Julai 28, 2019 Viwanja vya
Nyakabindi Bariadi.
Baadhi ya vipando vilivyo katika Viwanja
vya Maonesho ya Nanenane Kanda ya Ziwa Mashariki vilivyopandwa kwa
ajili ya maandalizi ya Maonesho ya Nanenane Kitaifa mwaka 2019 .
Mtaalam kutoka JKT (kulia) akitoa maelezo
kwa Naibu Waziri wa Kilimo, Mhe. Omary Mgumba (katikati) wakati
akikagua moja ya Bwawa la ufugaji wa samaki wakati wa ziara ya kukagua
maandalizi ya Maonesho ya Nanenane Kitaifa mwaka 2019 yatakayofanyika
kuanzia Julai 28, 2019 Viwanja vya Nyakabindi Bariadi.
Mtaalam kutoka JKT (kulia) akitoa maelezo
kwa Naibu Waziri wa Kilimo, Mhe. Omary Mgumba wakati akikagua moja ya
tanki la ufugaji wa samaki wakati wa ziara ya kukagua maandalizi ya
Maonesho ya Nanenane Kitaifa mwaka 2019 yatakayofanyika kuanzia Julai
28, 2019 Viwanja vya Nyakabindi Bariadi.
Mkuu wa Mkoa wa Mara, Mhe. Adam Kighoma
Malima(kulia) akizungumza katika kikao cha Kamati ya maandalizi ya
Maonesho ya Nanenane Kitaifa 2019 Kanda ya Ziwa Mashariki,
kilichofanyika katika Viwanja vya Nyakabindi Bariadi, (kushoto) ni Mkuu
wa Mkoa wa Simiyu, Mhe. Anthony Mtaka.
……………………….
Na Stella Kalinga, Simiyu
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa
Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan anatarajia kuwa mgeni rasmi katika
ufunguzi wa Maonesho ya Nanenane Kitaifa mwaka 2019, yatakayofanyika
Kanda ya Ziwa Mashariki katika Viwanja vya Nyakabindi Mjini Bariadi
kuanzia tarehe 29/07/2019 hadi 08/08/2019.
Hayo yamesemwa na Mkuu wa Mkoa wa Simiyu,
Mhe. Anthony Mtaka wakati akizungumza na waandishi wa habari katika
mkutano maalum wa kutoa taarifa kwa Umma uliofanyika Mjini Bariadi,
Julai 24, 2019.
Mtaka amesema Mhe Makamu wa Rais
atafungua rasmi maonesho hayo Agosti Mosi, 2019 na waoneshaji mbalimbali
zikiwemo Taasisi, Mashirika mbalimbali na wajasiriamali wataanza
kuonesha teknolojia, huduma na bidhaa zao Julai 29, 2019 ikiwa ni
maandalizi ya ufunguzi rasmi utakaofanywa na Mhe. Makamu wa Rais.
“Shughuli ya ufunguzi itafanywa tarehe
01/08/2019 na Mhe. Makamu wa Rai, haya ni maonesho ambayo yatakaribisha
viongozi wa Kitaifa, Agosti 03, 2019 tutakuwa na Mhe. Waziri Mkuu,
Agosti 06, 2019 tutakuwa na Waziri Mkuu Mstaafu, Mizengo Pinda na Kilele
tunatarajia kuwa na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt.
John Pombe Magufuli” alisema.
Naibu Waziri wa Kilimo, Mhe. Omary Mgumba
amesema ameridhishwa na maandalizi ya Maonesho ya nanenane
yanayoendelea mkoani Simiyu na kutoa wito kwa wakulima na wananchi wote
kwa ujumla kujitokeza kwa wingi kushiriki katika maonesho haya ili kuja
kujionea teknolojia mbalimbali zitakazojibu changamoto za wakulima,
wafugaji na wavuvi.
Aidha, Mhe. Mgumba ametoa wito kwa
waoneshaji kuwa wabunifu katika teknolojia, huduma na bidhaa
watakazoonesha ili maonesho haya yawe chachu ya kuwasaidia wakulima,
wavuvi na wafugaji kuongeza tija katika uzalishaji
Naye Mkuu wa Mkoa wa Mara, Mhe. Adam
Malima amesema matarajio ya mikoa ya Simiyu, Mara na Shinyanga inayounda
Kanda ya Ziwa Mashariki ni kuwa na maonesho ya tofauti na mwaka jana,
lengo likiwa ni kuifanya kanda hiyo kuwa ni mahali pa kudumu pa
wakulima, wafugaji na wavuvi kuwa na maonesho ya kilimo biashara.
Maonesho ya Nanenane Kitaifa yanafanyika
kwa mara ya pili sasa mkoani Simiyu tangu Kanda ya Ziwa ilipogawanywa
katika kanda mbili yaani, Kanda ya Ziwa Mashariki(Simiyu, Mara na
Shinyanga) na Kanda ya Ziwa Magharibi(Mwanza, Geita na Kagera) ambapo
mwaka huu yanaadhimishwa chini ya kauli Mbiu:-“KILIMO, MIFUGO NA UVUVI KATIKA UKUAJI WA UCHUMI WA NCHI”
0 comments:
Post a Comment