Naibu Waziri wa Ardhi Nyumba na
Maendeleo ya Makazi Dkt Angeline Mabula akiangalia wamiliki wa viwanja
walioingizwa katika Mfumo wa ukusanyaji kodi ya ardhi kwa njia ya
Kieletroniki katika ofisi za Ardhi za Halmashauri ya Wilaya ya Gairo
mkoani Morogoro jana wakati wa ziara yake ya kukagua utendaji wa sekta
ya ardhi katika wilaya hiyo jana. Wa tatu kulia ni Mkuu wa wilaya ya
Gairo Sirieli Mchembe na aliyekaa ni Afisa Ardhi Msaidizi wa
Halamashauri ya Wilaya ya Gairo Salivius Sarapion.
Naibu Waziri wa Ardhi Nyumba na
Maendeleo ya Makazi Dkt Angeline Mabula akipata maelezo kutoka kwa
Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya wilaya ya Gairo Agnes Mkandya
kuhusiana na makusanyo ya kodi ya ardhi wakati wa ziara yake ya kukagua
utendaji wa sekta ya ardhi katika wilaya ya Gairo mkoani Morogoro jana.
Katikati ni Mkuu wa wilaya ya Gairo Sirieli Mchembe.
Naibu Waziri wa Ardhi Nyumba na
Maendeleo ya Makazi Dkt Angeline Mabula akiwa na Mkuu wa Wilaya ya Gairo
Sirieli Mchembe akiangalia sehemu ya Mizinga ya Nyuki katika eneo la
Msingisi Gairo wakati wa ziara yake katika wilaya ya Gairo jana.
Naibu Waziri wa Ardhi Nyumba na
Maendeleo ya Makazi Dkt Angeline Mabula akielekea katika Shamba la Miti
la Ukaguru kukagua maendeleo ya ujenzi wa ofisi na nyumba za Wakala wa
Huduma za Misitu Tanzania (TFS) jana. Katikati ni Mkuu wa wilaya ya
Gairo Sirieli Mchembe na Kulia ni Meneja wa Shamba la Miti la Ukaguru
Mohamed Msalu.
Naibu Waziri wa Ardhi Nyumba na
Maendeleo ya Makazi Dkt Angeline Mabula akitoka kukagua ujenzi wa ofisi
na nyumba za Wakala wa Huduma za Misitu Tanzania (TFS) jana katika
hifadhi ya Msitu wa Ukaguru. Anayemfuatia ni Mkuu wa wilaya ya Gairo
Sirieli Mchembe.
Naibu Waziri wa Ardhi Nyumba na
Maendeleo ya Makazi Dkt Angeline Mabula akiwa na Mkuu wa Wilaya ya Gairo
wakitembea katika hifadhi ya Msitu wa Ukaguru wilaya ya Gairo jana
alipokwenda kukagua maendeleo ya ujenzi wa ofisi na nyumba za Wakala wa
Huduma za Misitu Tanzania (TFS) jana.
Naibu Waziri wa Ardhi Nyumba na
Maendeleo ya Makazi Dkt Angeline Mabula akiwa na Viongozi pamoja na
watendaji wa sekta ya ardhi katika wilaya ya Gairo kwenye Maporomoko ya
hifadhi ya Msitu wa Ukaguru wilayani Gairo jana. Kulia kwa Naibu Waziri
ni Mkuu wa Wilaya ya Gairi Sirieli Mchembe.
……………………
Na Munir Shemweta, WANMM GAIRO
Kasi ndogo ya ukusanyaji mapato ya
Kodi ya pango la ardhi katika halmashauri ya wilaya ya Gairo mkoa wa
Morogoro imemsononesha Naibu Waziri wa Ardhi Nyumba na Maendeleo ta
Makazi Dkt Angeline Mabula na kuagiza halmashauri hiyo kuongeza kasi ili
kufikia lengo la mapato ya kodi ya ardhi.
Akiwa katika ziara yake ya
siku moja katika wilaya hiyo jana tarehe 19 Novemba 2019 Dkt Mabula
alielezwa na Afisa Ardhi katika halmashauri ya Gairo Nicolaus Matsuva
kuwa halmashauri hiyo katika kipindi cha mwaka 2018/2019 imekusanya
shilingi milioni 12.3 na mwaka huu kufikia Novemba imekusanya milioni
10 ya kiwango ilichopangiwa cha milioni 55.
Naibu Waziri wa Ardhi Nyumba
na Maendeleo ya Makazi alisema, kiwango hicho cha makusanyo katika
halmashauri ya Gairo ni kidogo na hakijafikia hata nusu ya makadirio ya
shilingi milioni 55 iliyowekewa halmashauri hiyo kukusanya kwa mwaka na
makadirio hayo hayalingani na uhalisia wa makusanyo ya halmashauri.
Aliitaka halmashauri ya Gairo
kupitia idara yake ya ardhi kuongeza kasi ya makusanyo ya maduhuli ya
kodi ya pango la ardhi kwa kuwa kodi hiyo ndiyo inayoisaidia serikali
kutekeleza miradi mikubwa aliyoieleza kuwa mingi inataegemea kodi ya
ndani.
‘’Msipokusanya kodi ya ardhi
mjue mnamkwamisha Mhe Rais kutekeza miradi mikubwa kama vile mradi wa
kufufua umeme wa Mwl. Nyerere maarufu kama stiglers hivyo ni lazima
tuongeze kasi ya makusanyao’’ alisema Dkt Mabula.
Sambamba na hilo Dkt Mabula
aliitaka halmashauri ya wilaya ya Gairo kuhakikisha kufikia Desemba 2019
inarejesha fedha shilingi milioni 31 ilizopatiwa mwezi Juni 2019 kama
mkopo kwa ajili ya upimaji viwanja katika halmashauri hiyo.
Hatua hiyo inafuatiwa Naibu
Waziri Mabula kuhoji kuhusiana na marejesho ya fedha za mkopo huo na
kuelezwa na Afisa Ardhi kuwa, halmashauri hiyo hajarejesha kiasi
chochote cha fedha za mkopo iliopatiwa kwa ajili ya upimaji viwanja na
kuomba kuongezewa muda wa kurejesha hadi mwezi Machi 2019.
‘’ Toka mwezi Juni hadi leo
Desemba hamjarejesha wakati ulitakiwa kurejeshwa ndani ya miezi mitatu,
Mkopo huu unazunguka kwa nini hamjarejesha hadi leo? Kazi mliyopewa
hamjamaliza naagiza hadi kufikia Desemba fedha hiyo iwe imerejeshwa’’
alisema Mabula.
Aidha, Naibu Waziri wa Ardhi
Nyumba na Maendeleo ya Makazi ameshangazwa na idara ya ardhi katika
halmashauri ya Gairo kuingiza viwanja 155 kati ya 1,198 kwenye mfumo wa
makusanyo ya kodi ya ardhi kwa njia ya kielektroniki jambo alilolieleza
linaikosesha serikali mapato yataokanayo na kodi ya pango la ardhi
sambamba na kushindwa kutoa ilani kwa wadaiwa sugu wa kodi ya ardhi
ingawa ilani hizo zilizndaliwa tangu mwezi Machi 2019.
Dkt Mabula alielezwa na Afisa
Ardhi wa Halmashauri ya wilaya ya Gairo Nicolaus Matsuva kuwa, baadhi ya
wadaiwa sugu wa kodi ya ardhi walishindwa kupatiwa ilani hizo kutokana
na maeneo wanayomiliki kukutwa wakiishi watu wengine tofauti na wamiliki
waliopo kwenye kumbukumbu zao jambo lilimfanya Naibu Waziri kumuagiza
Kaimu Kamishna wa Ardhi Msaidizi Kanda Maalum ya Morogoro Erick Makundi
kufuatilia suala hilo kwa kwenda uwandani na kupatiwa taarifa kufikia
Desemba mwaka huu.
Kwa upande wake Mkuu wa
Wilaya ya Gairo Sirieli Mchembe alisema, wilaya yake ina changamoto
kubwa ya ujenzi holela na kubainisha kuwa hata zoezi la urasimishaji
katika wilaya hiyo linakabiliwa na changamoto mbalimbali ikiwemo sebule
za baadhi ya nyumba kuelekezwa kwenye vyoo vya nyumba nyingine.
Hata hivyo, alimuahidi Naibu
Waziri wa Ardhi Nyumba na Maendeleo ya Makazi kuwa ofisi yake
itayafanyia kazi maagizo yote aliyoyatoa ikiwemo uandaaji wa Mpango
Kabambe katika wilaya hiyo iweze kupangika kimji sambamba na kuwa na Mji
wa Serikali utakaojumuisha taasisi zote za serikali zilizopo katika
wilaya hiyo.
Ktika hatua nyingine Naibu
Waziri wa Ardhi nyumba na Maendeleo ya Makazi Dkt Angeline Mabula
alitembelea hifadhi ya Msitu wa Ukaguru uliopo Tarafa ya Nongwe kata ya
Mandege wilaya ya Gairo mkoa wa Morogoro na kukagua maendeleo ya ujenzi
wa nyumba na ofisi za Wakala wa Huduma za Misitu Tanzania (TFS)
unaofanywa na Shirika la nyumba la Taifa (NHC).
Akiwa kwenye ukaguzi wa ujezi
huo, Dkt Mabula alipata malalamiko ya baadhi ya vibarua wanaojenga ofisi
hiyo kutopatiwa malipo kwa wakati jambo walilolieleza kuwa
linawakatisha tamaa kuendelea na kazi hiyo. Hata hivyo, Naibu Waziri
Mabula aliwataka vibarua hao kuendelea kufanya kazi kwa bidii na kuahidi
kulifuatialia suala hilo haraka ili vibarua hao walipwe fedha kwa
wakati.
Aidha, Dkt Mabula alipata
fursa ya kutembelea Maporomoko katika hifadhi ya shamba la Miti la
Ukaguru ambapo alijionea namna eneo hilo linavyoweza kuwa moja ya
vyanzo vya umeme sambamba na kuwa kivutio kikubwa cha utalii kinachoweza
kuingizia serikali mapato yatokanayo na sekta hiyo.
Mkuu wa Wilaya ya Gairo
Sirieli Mchembe alielezea ziara ya Naibu Waziri Mabula kwenye Maromoko
hayo kuwa ni ya kwanza kufanywa na Waziri na kubainisha kuwa ziara hiyo
inaweza kuwa chachu ya hifadhi ya Msitu huo kutumika kwa shughuli
mbalimbali kama vile za kitalii.
0 comments:
Post a Comment