Mkuu wa Mkoa wa Geita Mhandisi Robert Grbriel Akiwasilisha Mada katika kakao cha Bodi ya Barabara Mkoani Geita.
Baadhi ya wajumbe walioshiriki kikao cha Bodi ya Barabara Mkoani Geita
Waziri wa Madini Doto Biteko akiandika faarifa katika kikako cha Bodi ya. Barabara kilichofanyika Mkoani Geita.
…………………..
Na Tito Mselem Geita,
Waziri wa Madini Doto Biteko
ameshiriki katika Kikao cha Bodi ya Barabara kilichofanyika Oktoba
15,2019 katika Ukumbi wa Mikutano wa Mkuu wa Mkoa wa Geita ili kujadili
changamoto za barabara mkoani hamo.
Kikao hicho kiliudhuliwa na
viongozi mbalimbali wa Serikali na Chama cha Mapindizi wakiwemo Wabunge
wa Majimbo ya Mkoa wa Geita akiwemo Mbunge wa Bukombe ambaye pia ni
Waziri wa Madini Doto Biteko, Mbunge wa Chato ambaye pia ni Waziri wa
Nishati Dkt. Medard Kalemani, Mbunge wa Geita Mjini ambaye pia Naibu
Waziri wa Maliasili na Utalii Costantine Kanyasu, Mbunge wa Geita
Vijijini Joseph Msukuma, Mbunge wa Mbogwe Augustino Masele, Mbunge wa
Busanda Lolesia Bukwimba, Mbunge wa Viti Maalumu wa Chadema Pendo
Peneza.
Vingozi wengine walioshiriki
ni pamoja na Mkuu wa Mkoa wa Geita Mhandisi Robert Gabriel, Mkuu wa
Wilaya ya Geita Mjini Josephat Maganga, Mkuu wa Wilaya ya Bukombe Said
Mkumba, Mkuu wa Wilaya ya Mbogwe. Martha Mkupasi, Mkuu wa Wilaya ya
Nyang’hwale Hamim Gwiyama, Mwenyekiti wa Chama cha Mapinduzi (CCM) Mkoa
Geita Alhaji Said Kalidushi pamoja na Wakuu wa Idara mbalimbali.
Aidha Waziri Biteko
amewapongeza viongozi wa TANROADS na TARURA kwa kazi nzuri wayoifanya
katika Mkoa wa Geita kwa kuhakikisha kuwa barabara zinatengenezwa kwa
kiwango kizuri na kumalizika kwa wakati.
Hata hivyo, Waziri Biteko
amempongeza Mkuu wa Mkoa wa Geita Mhandisi Robert Gabriel kwa usimamizi
na ufuatiliaji mzuri katika kuhakisha barabara za Mkoa wa Geita
zinakamilika kwa muda uliopangwa na zinakuwa kwenye viwango
vinavyotakiwa.
Imeelezwa kuwa Mji wa Geita ni
kati ya miji inayokua kwa kasi sana sambamba na ongezeko la watu na
shughuli za kiuchumi, hivyo kuwepo na msongamano mkubwa wa vyombo vya
usafiri na watembea kwa miguu barabarani.
Kwa upande wake Mkuu wa Mkoa wa
Geita Mhandisi Robert Gabriel amesema katika awamu hii ya tano Rais Dkt.
John Pombe Magufuli alitupa ahadi ya ujenza wa barabara na ametekeleza
ujenzi wa barabara ya Ushirombo mpaka Lusahunga kilometa 110 kwa gharama
ya shilingi bilioni 114.557, Uwanja wa Ndege wa Chato kilometa 3.5 kwa
gharama ya Shilingi Billioni 39.15.
Aidha, Mhandisi Gabriel
amesema kwamba, kazi ambazo zimekamilika ni pamoja na ujenzi wa barabara
ya Runzewe mpaka Bwanga kilometa 45 kwa gharama ya shilingi bilioni
43.357 na barabara ya Bwanga mpaka Biharamuro kilometa 65.0 miradi yote
hii inatekelezwa kwa fedha za serikali.
Katika hatua nyingine Mhandisi
Gabriel ameeleza kwamba katika Mkoa wa Geita TANROADS inasimamia miradi
ya usanifu wa kina katika barabara za Geita mpaka Kahama yenye kilometa
139.557 kwa gharama ya shilingi bilioni 440 inatelekezwa na mkandarasi
ENV Engeneering, kazi imekamilika.
“TANROADS inasimamia pia
usanifu katika barabara ya Nyamirembe mpaka Katoke yenye urefu wa
kilometa 50 kwa gharama ya shilingi bilioni 861.046 na Mhandisi Consult
ambapo kazi hiyo imekamilika,” Gabriel amesema Mhandisi Gabriel.
Katika hatua nyingine Mhandisi
Gabriel ametoa rai kwa wananchi kutunza miundombinu ya barabara kwa
kutopitisha mifugo na kunyofoa alama za barabarani pamoja na kutovamia
hifadhi za barabara.
Katika bajaeti ya mwaka
2018/2019 TARURA Mkoa wa Geita unatarajiwa kutumia kiasi cha shilingi
6,844,393,140.37 kutoka mfuko wa barabara (Road fund) kwa ajili ya
matengenezo ya barabara na shilingi 1,612,500,000.00 kwa ajili ya kazi
za maendeleo, fedha hizo ni kutoka OR-TAMISEMI.
Hadi kufikia Tarehe 03/01/2019
jumla ya shilingi 2,249,253, 616.84 sawa na asilimia 32.86 zimepokelewa
kwa ajili matengenezo ya barabara na jumla ya shilingi 612,654,524.43
sawa na asilimia 37.99 zimepokelewa kwa ajili ya miradi maendeleo ya
barabara za mkoani Geita.
0 comments:
Post a Comment