METDO Tanzania

METDO Tanzania

Wednesday, October 16, 2019

KATIBU MKUU ALAT AWATAKA VIJANA KUSOMEA KILIMO KUJIKWAMUA

Afisa Kilimo wa wilaya ya Mpwapwa, Edson Kileo,akizungumza wakati Katibu Mkuu wa Jumuiya ya Tawala za Mitaa  chini(ALAT),  Elirehema Kaaya alipofanya ziara ya kukagua maendeleo ya mradi unaoendelea wa uboreshaji kituo cha Kilimo,Mawasiliano na Taaluma cha mafunzo ya kilimo Kibakwe wilayani humo.
Mkuu wa kituo hicho Samson German akisoma taarifa kwa upande wa kulia ni Katibu Mkuu wa Jumuiya ya Tawala za Mitaa  chini(ALAT),  Elirehema Kaaya akimsikiliza wakati alipofanya ziara ya kukagua maendeleo ya mradi unaoendelea wa uboreshaji kituo cha Kilimo,Mawasiliano na Taaluma cha mafunzo ya kilimo Kibakwe wilayani humo.
Katibu Mkuu wa Jumuiya ya Tawala za Mitaa  chini (ALAT),  Elirehema Kaaya ,akikagua miradi huku Mkuu wa kituo hicho Samson German akimuonyesha jinsi gani mbogamboga zinazolimwa  wakati alipofanya ziara ya kukagua maendeleo ya mradi unaoendelea wa uboreshaji kituo cha Kilimo,Mawasiliano na Taaluma cha mafunzo ya kilimo Kibakwe wilayani humo.
Katibu Mkuu wa Jumuiya ya Tawala za Mitaa  chini(ALAT),  Elirehema Kaaya ,akiendelea na ukaguzi wa  maendeleo ya mradi unaoendelea wa uboreshaji kituo cha Kilimo,Mawasiliano na Taaluma cha mafunzo ya kilimo Kibakwe wilayani humo.
Katibu Mkuu wa Jumuiya ya Tawala za Mitaa  chini (ALAT),  Elirehema Kaaya, akitoa maelezo kwa  Mkuu wa kituo hicho Samson German  wakati alipofanya ziara ya kukagua maendeleo ya mradi unaoendelea wa uboreshaji kituo cha Kilimo,Mawasiliano na Taaluma cha mafunzo ya kilimo Kibakwe wilayani humo.
…………………….
Na.Alex Sonna,Mpwapwa
Katibu Mkuu wa Jumuiya ya Tawala za Mitaa nchini (ALAT),  Elirehema Kaaya,amewataka vijana kukitumia kituo cha kilimo,Mawasiliano na Taaluma kilichopo Mpwapwa mkoani Dodoma kupata ujuzi wa kilimo cha mbogamboga na maua ili waweze kuondokana na tatizo la ajira.
Hayo ameyasema jana wakati alipofanya ziara ya kukagua maendeleo ya mradi unaoendelea wa uboreshaji kituo hicho cha mafunzo ya kilimo Kibakwe wilayani humo.
Bw.Kaaya alisema kuwa  mradi huo umetumia  zaidi ya Sh.Milioni 240 huku Halmashuari ya Mpwapwa ikitoa zaidi ya Sh.Milioni 90 na kwamba ni miongoni mwa miradi wa kuboresha mazingira ya biashara na uwekezaji(LIC) unaotekelezwa kwenye mikoa ya Dodoma na Kigoma kwa ushirikiano kati ya Ofisi ya TAMISEMI na ubalozi wa Denmark.
Aidha amewashauri vijana wanaomaliza kidato cha nne kujifunze kwenye kituo hicho ili kuondokana na malalamiko ya kukosa ajira.
Bw.Kaaya alisema kuwa hakuna ajira,lakini wajue hakuna ajira inayozidi kilimo cha aina hii, hii elimu wanayopata hapa wakaifanye wakati wanasubiri matokeo ya kuendelea na elimu ya juu.
 Alisema kuwa  kumekuwa na mwamko mdogo wa vijana kuchangamkia mafunzo yanayotolewa na kituo hicho na wengine kuona kama kilimo ni utumwa wakati kinaweza kuwakwamua kiuchumi.
Hata hivyo Kaaya ,aliagiza kujengwa kwa mfumo wa kuvuna maji ya mvua kwenye majengo ya kituo hicho ili kukabiliana na upungufu wa maji kwenye eneo hilo.
Alisema kuwa changamoto iliyopo katika kituo hiki ni kutokuwa na maji ya kutosha,uzio na kutokuwa na nguvu kazi wakihitajika vibarua hawapatikani,”alisema.
Awali, Mkuu wa kituo hicho Samson German akitoa taarifa alisema kituo hicho kinatoa huduma za kilimo na mifugo kwa wakulima katika eneo husika.
Alisema changamoto iliyopo ni vijana wanaozunguka eneo la kituo hicho kutotaka kujishughulisha kufanya kazi hasa shughuli za kilimo.
“Mpaka sasa kituo kimetoa elimu kwa vitendo kwa wanafunzi 30 wa mafunzo ya ujuzi waliotoka chuo cha kilimo na mifugo Visele Mpwapwa, pia wakulima 60 kutoka vijiji vya Kibakwe, Iyenge na Chamtumile juu ya kanuni za kilimo bora cha mbogamboga ili kuboresha lishe na kuongeza kipato,”alisema German
Naye, Afisa Kilimo wa wilaya ya Mpwapwa, Edson Kileo alisema kuna mwitikio mdogo kwa wakulima kujifunza.
Share:

0 comments:

Post a Comment

Copyright © WAZO HURU | Powered by Blogger Design by ronangelo | Blogger Theme by NewBloggerThemes.com