Baadhi ya Wananchi katika Kijiji cha Mwamanenge
wakimsikiliza Naibu Waziri wa Nishati, Subira Mgalu wakati alipofika Kijijini
hapo kuwasha umeme.
Naibu Waziri wa Nishati, Subira Mgalu akiwasha umeme
katika Kijiji cha Mwamanenge wilayani Maswa mkoa wa Simiyu
Mwananchi katika Kijiji cha Mwamanenge, Rahel Daniel
ambaye nyumba yake iliwashiwa umeme na Naibu Waziri wa Nishati, Subira
Mgalu (kulia) akishukuru juhudi za Serikali kupeleka umeme Kijijini hapo.
Naibu Waziri wa Nishati, Subira Mgalu, akifurahi mara
baada ya kuweka jiwe la Msingi katika Shule ya Sekondari Simiyu iliyopo
wilayani Bariadi, baadhi ya vyumba vya madarasa kwenye shule vimejengwa na
Shirika la Umeme Tanzania (TANESCO).
....................
Imeelezwa kuwa, zaidi ya shilingi bilioni 179
zilizotolewa na Wadau wa Maendeleo kama vile nchi za Norway, Sweden, Jumuiya ya
Umoja wa Ulaya (EU) na Shirika la
Maendeleo la Ufaransa (AFD) zinatarajia kutumika katika mradi wa usambazaji
umeme wa ujazilizi ambapo vitongoji zaidi ya 1103 vinatarajia kufaidika
katika mikoaTisa nchini.
Hayo yalielezwa na Naibu Waziri wa Nishati, Subira
Mgalu, Septemba 18, mwaka huu wakati
alipokuwa akizungumza na wananchi wa kijiji cha Mwamanenge, Wilaya ya Maswa,
Mkoa wa Simiyu kabda hajawasha umeme.
Mikoa itakayofaidika na mradi huo ni Kilimanjaro,
Mbeya, Dodoma, Tanga, Pwani, Shinyanga, Mwanza, Singida na Tabora.
Alisema, Serikali imeleta umeme wa bei nafuu nchini
ili kuleta usawa katika utoaji huduma kwa wananchi wenye vipato tofauti na
kwamba wananchi wote waliopitiwa na miondombinu ya umeme watapatiwa nishati
hiyo.
“Kwa upande wa Wilaya ya Maswa, matarajio yetu ni
kuwa, mapema mwaka 2021 vijiji vyote vya Maswa takriban 125 vitakuwa
vimeshaunganishiwa umeme, tumesema hatuchangui nyumba, nyumba zote zitawekewa
umeme.” Alisemaa Mgalu
Naye mwananchi wa Kijiji cha Mwamanenge, Rahel Daniel
ambaye nyumba yake iliwashiwa umeme, aliishukuru Serikali kwa kuwajali
wananchi wa kipato cha chini kwa kuwawekea bei ya umeme ya shilingi 27,000
ambayo hata wao wameweza kuimudu na alimhakikishia Naibu Waziri kuwa, ataitumia
huduma hiyo ya umeme kujiendeleza kiuchumi.
Naibu Waziri pia
aliweka jiwe la msingi katika shule ya sekondari Simiyu iliyopo wilayani
Bariadi ambayo Shirika la Umeme Tanzania (TANESCO) limejenga baadhi ya
vyumba vya madarasa na aliwaasa wanafunzi hao kusoma kwa bidii na
watumie fursa ya umeme kujisomea haswa katika nyakati za usiku.
0 comments:
Post a Comment