
Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri
Mkuu, Sera, Bunge, Kazi, Ajira, Vijana na wenye ulemavu, Mhe. Jenista
Mhagama ( wa pili kulia) akimkabidhi Bi. Efrancia Kabuga kutoka Wilaya
ya Kishapu mfano wa Hundi ya shilingi 50,000,000/=mkopo kutoka benki ya
CRDB , ambao amefadhiliwa na Taasisi ya PASS, katika kilele cha
Maonesho ya tatu ya Mifuko/ Programu za Uwezeshaji na Vikundi vya
Kifedha vya Kijamii, Oktoba 20, 2019 Mjini Baradi Mkoani Simiyu.

Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri
Mkuu, Sera, Bunge, Kazi, Ajira, Vijana na wenye ulemavu, Mhe. Jenista
Mhagama ( katikati) akikata utepe kama ishara ya kuzindua Mpango mkakati
wa Baraza la Taifa la uwezeshaji wananchi Kiuchumi(NEEC) kwa kipindi
cha 2018/2019 mpaka 2022/2023, katika kilele cha Maonesho ya tatu ya
Mifuko/ Programu za Uwezeshaji na Vikundi vya Kifedha vya Kijamii,
Oktoba 20, 2019 Mjini Baradi Mkoani Simiyu(kushoto) Mkuu wa Wilaya ya
Bariadi, Mhe. Festo Kiswaga na kulia ni Mwenyekiti wa NEEC, Dkt. Festus
Limbu

Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri
Mkuu, Sera, Bunge, Kazi, Ajira, Vijana na wenye ulemavu, Mhe. Jenista
Mhagama akiwasikiliza baadhi ya wajasiriamali waliowezeshwa na Shirika
la Maendeleo ya Viwanda Vidogo(SIDO), wakati alipotembelea mabanda ya
maonesho, katika kilele cha Maonesho ya tatu ya Mifuko/ Programu za
Uwezeshaji na Vikundi vya Kifedha vya Kijamii, Oktoba 20, 2019 Mjini
Baradi Mkoani Simiyu.

Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri
Mkuu, Sera, Bunge, Kazi, Ajira, Vijana na wenye ulemavu, Mhe. Jenista
Mhagama akiwasikiliza baadhi ya wajasiriamali waliowezeshwa na Shirika
la Maendeleo ya Viwanda Vidogo(SIDO), wakati alipotembelea mabanda ya
maonesho, katika kilele cha Maonesho ya tatu ya Mifuko/ Programu za
Uwezeshaji na Vikundi vya Kifedha vya Kijamii, Oktoba 20, 2019 Mjini
Baradi Mkoani Simiyu.

Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri
Mkuu, Sera, Bunge, Kazi, Ajira, Vijana na wenye ulemavu, Mhe. Jenista
Mhagama akimsikiliza mwakilishi wa Kiwanda cha Waziri Mkuu, Mizengo
Pinda akitoa maelezo kuhusu asali inayotengeenzwa na kiwanda hicho,
wakati alipotembelea mabanda ya maonesho, katika kilele cha Maonesho ya
tatu ya Mifuko/ Programu za Uwezeshaji na Vikundi vya Kifedha vya
Kijamii, Oktoba 20, 2019 Mjini Baradi Mkoani Simiyu.
…………………….
Na Stella Kalinga, Simiyu RS
Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri
Mkuu , Sera, Bunge, Kazi, Vijana, Ajira na wenye ulemavu
Jenista Mhagama , ameziagiza halmashauri zote nchini kufanya uhikiki
wa kina wa taasisi ndogo za kifedha zinazotoa mikopo kwa wananchi na
vikundi, ili kuzibaini taasisi zinazowaibia Watanzania badala ya
kuwanufaisha kiuchumi..
Waziri Mhagama ametoa agizo
hilo, katika kilele cha Maonesho ya tatu ya Mifuko/ Programu za
Uwezeshaji na Vikundi vya Kifedha vya Kijamii, yaliyofanyika Kitaifa
katika Uwanja wa Halmashauri ya Mji wa Bariadi Oktoba 20, 2019.
“Ninajua baadhi ya taasisi
ndogo za fedha badala ya kuwasaidia wanachama zimekuwa ziifanya kazi ya
kuiba fedha za wanachama na kuwafanya wanachama warudi nyuma badala
kusonga mbele, agizo hili Baraza la Taifa la Uwezesheshaji wananchi
Kiuchumi mlifuatilie kwa kushirikiana na Ofisi ya Rais TAMISEMI,”
alisema Mhagama.
Katika hatua nyingine ameitaka
mifuko/programu za uwezeshaji wanachi kiuchumi kutoa mikopo kwa riba
nafuu tofauti na taasisi nyingine za kifedha, ambapo amebainisha kuwa
takribani wajasiriamali 1,237,984 wamenufaika na mikopo ya mifuko hiyo
na hadi kufikia Juni 2019 jumla shilingi bilioni 388.4 zimetolewa.
Mwakilishi wa Mkuu wa Mkoa wa
Simiyu, Mkuu wa Wilaya ya Bariadi, Mhe.Festo Kiswaga ametoa wito kwa
Taasisi za kifedha kuhakikisha zinajibu changamoto za wananchi huku
akiwataka wananchi (wajasiriamali) walioshiriki maonesho haya kutumia
vema fursa walizoziona katika mifuko ya uwezeshaji wananchi kiuchumi ili
wakuze uchumi wao
Baadhi ya wanufaika wa mikopo
wilaya ya Bariadi na Busega mkoani Simiyu na Chato Mkoani Geita
wamezishukuru Taasisi za kifedha zilizowakopesha mitaji jambo ambalo
limewasaidia kuimarsisha shughui zao za kiuchumi wanazofanya ikiwa ni
pamoja na kilimo na ufugaji.
“Naishukuru Benki ya AZANIA na
wadhamini wangu Taasisi ya PASS kwa kuniwezesha kupata mkopo wa shilingi
milioni 20, kuanzia sasa nitalima kisasa na nitaenda kuongeza
miundombinu ya maji kwenye shamba langu maana nilikuwa nalima ekari 10
kwa kumwagilia badala ya ekari 30 nilizo nazo,” alisema Elisha Malugu
kutoka wilayani Busega.
Mwenyekiti wa Baraza la Taifa
la Uwezeshaji wananchi kiuchumi(NEEC) Dkt. Festus Limbu amesema NEEC
inaendelea kufuatilia agizo la Waziri Mkuu, Mhe. Kassim Majaliwa
alilolitoa Juni 2019 la kila mkoa kuwa na kituo cha uwezeshaji wananchi
kiuchumi, lengo likiwa kuvifanya vituo hivyo kuwa kitovu cha uwezeshaji
wananchi kiuchumi.
Katibu Mtendaji wa NEEC, Bi. Beng’
Issa amesema Maonesho haya yameshirikisha Taasisi 45, wajasiriamali
zaidi ya 200 kutoka mikoa ya Simiyu, Mbeya, Pwani, Mwanza, Tabora,
Kagera , Mara, Singida na Dar es Salaam na kutoka nchi jirani za Burundi
na Kenya.
Maonesho ya tatu ya Mifuko/ Programu za Uwezeshaji na Vikundi vya Kifedha vya Kijamii chini ya Kauli Mbiu, “Mitaji ni Chachu ya Kujenga Uchumi wa Viwanda” yametanguliwa na maonesho ya kwanza yaliyofanyika Mbeya mwaka 2017, ambapo ya pili yalifanyika mwaka 2018 jijini Dodoma.
0 comments:
Post a Comment