Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu (Uwekezaji), Angellah Kairuki akimkabidhi Kitabu chenye Fursa na Miradi yenye Uhitaji Mitaji ya Uwekezaji nchini , Mwekezaji toka nchini Uturuki ambaye pia ni Mwenyekiti wa Bodi ya Kampuni ya MNG Group of Companies mara baada ya kufanya kikao juu ya fursa na miradi ya uwekezaji nchini leo, tarehe 5 Januari, 2019, jijini Dodoma.
Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu (Uwekezaji), Angellah Kairuki akiwasikiliza wataalamu wa masuala ya uwekezaji wa Ofisi ya waziri Mkuu wakati wa kikao na wawekezaji toka nchini Uturuki katika Kampuni ya MNG Group of Companies (hawapo pichani), wakati walipofanya kikao ofisini kwake juu ya fursa na miradi ya uwekezaji nchini leo, tarehe 5 Januari, 2019, jijini Dodoma.
Na. OWM, DODOMA
Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu
(Uwekezaji), Angellah Kairuki amekutana na Wawekezaji kutoka nchini
Uturuki katika Kampuni ya MNG Group of Companies na kufanya nao
mazungumzo nao juu ya miradi waliyoonesha nia ya kuwekeza hapa nchini.
Kikao hicho ambacho kimehudhuriwa na Waziri wa
Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano, Mhandisi, Isack Kamwelwe, Wataalamu wa masuala
ya Uwekezaji na maendeleo ya Sekta Binafsi pamoja na wataalam wa
Kituo cha Uwekezaji nchini, leo mjini Dodoma, tarehe 5 Januari 2019, Waziri Kairuki
amebainisha wazi kuwa nia ya serikali ya awam ya tano ni kuhakikisha uwekezaji
wenye tija nchini, na kwa kuzingatia mfumo wa sera ya Ushirikiano baina
ya sekta Binafsi na Umma inahakikisha inavutia wawekezaji zaidi.
“Tunazo fursa na miradi inayohitaji mitaji ya
uwekezaji hapa nchini, jukumu letu ni kuhakikisha wawekezaji mnapata
mazingira wezeshi katika fursa na miradi mnayotaka kuwezesha ili nchi iweze
kupata tija kutokana uwekezaji huo” Amesisitiza Kairuki.
Akiongea katika kikao hicho mwenyekiti wa Bodi ya
MNG Group of Companies, Mehmet Gunal, amefafanua kuwa , Kampuni hiyo iko tayari
kuwekeza nchini katika Sekta ya Uchukuzi, Utalii, Nishati, Usafiri wa Anga na
Ujenzi hapa nchini.
“Tumevutiwa na mazingira ya uwekezaji hapa nchini,
Tanzania ndio maana nimeamua kampuni yetu iweze kujua fursa na miradi yenye
kuhitaji uwekezaji nchini ili tuweze kukamilisha taratibu za uwekezaji na
tuweze kuwekeza na tuko tayari kuwekeza hata kwa mfumo wa sera ya ushirikiano
baina ya Sekta ya Binafsi na Umma au kuwekeza sisi wenyewe ” Masema Gunal
Kampuni ya MNG Group of Companies inao uzoefu
katika masuala ya uwekezaji kwa miaka 42 katika mabara matatu Duniani, ikiwa
imejikita katika uwekezaji kwenye sekta sita na tayari hadi hivi
sasa imetekeleza miradi zaidi ya mia mbili katika mabara hayo.
Baadhi ya Miradi ambayo imetekelezwa na Kampuni
hiyo ni pamoja na , Bwawa la kufua Umeme la Chief Dam la nchini Algeria,
Ujenzi wa uwanja wa Ndege wa Kimataifa KOTOKA (terminal III),
wa nchini Ghana, Ujenzi wa makao makuu ya Benki ya Halk
nchini Uturuki, Uwanja wa mpira wa TIZI Ouzu pamoja na
MWISHO
0 comments:
Post a Comment