
Waziri wa Nishati, Dkt Medard
Kalemani (wa tatu kulia), Mkurugenzi wa Utawala na Rasilimali Watu,
Wizara ya Nishati, Raphael Nombo (wa pili kushoto) na watendaji
mbalimbali kutoka TANESCO wakiimba wimbo wa ‘solidarity’ kabla ya kikao
cha wafanyakazi wa TANESCO, Kanda ya Kaskazini.

Baadhi ya wafanyakazi wa TANESCO,
Kanda ya Kaskazini wakimsikiliza Waziri wa Nishati, Dkt Medard Kalemani
(hayupo pichani) wakati wa kikao chake na wafanyakazi hao.

Waziri wa Nishati, Dkt Medard
Kalemani akiwa na Mkuu wa Mkoa wa Tanga, Martin Shigella katika Ofisi ya
Mkuu wa Mkoa wa Tanga kabla ya kikao chake na wafanyakazi wa TANESCO wa
Kanda ya kaskazini.

Baadhi ya wafanyakazi wa TANESCO,
Kanda ya Kaskazini wakimsikiliza Waziri wa Nishati, Dkt Medard Kalemani
(hayupo pichani) wakati wa kikao chake na wafanyakazi hao.

Waziri wa Nishati, Dkt Medard
Kalemani akizungumza na wafanyakazi wa TANESCO, Kanda ya Kaskazini.
Kikao hicho kilifanyika jijini Tanga.
…………………
Shirika la Umeme Tanzania
(TANESCO) kwa sasa linakusanya shilingi bilioni 46 kwa wiki hali
inayofanya Shirika hilo kuendelea kujitegemea baada ya kuacha kupokea
ruzuku kutoka serikalini ili kujiendesha.
Hayo yalielezwa na Waziri wa
Nishati, Dkt Medard Kalemani tarehe 18 Oktoba, 2019 wakati wa kikao
chake na wafanyakazi wa TANESCO wa Kanda ya kaskazini kilichofanyika
jijini Tanga na kuhudhuriwa na Mkurugenzi wa Utawala na Rasilimali Watu
wa Wizara ya Nishati, Raphael Nombo na viongozi kutoka TANESCO Makao
Makuu.
” Niwapongeze TANESCO kwa
kuendelea kujiendesha kwani hampokei tena ruzuku kutoka Serikalini na
sasa mnakusanya shilingi Bilioni 46 kwa wiki tofauti na miaka miaka
miwili iliyopita mlipokuwa mkikusanya bilioni Sita hadi Tisa kwa wiki,
mnao uwezo, endeleeni.”alisema Dkt Kalemani
Kuhusu mkakati wa kuongeza mapato
ya Shirika alisema kuwa, kunzia mwaka huu wa fedha, Kila Ofisi ya Mkoa
ya TANESCO itapewa malengo ya makusanyo na atakayefikia malengo hayo
atapewa motisha, ila atakayeshindwa atachukuliwa hatua.
Kuhusu ongezeko la wateja
waliounganishwa na umeme, Dkt Kalemani ameliagiza Shirika hilo kufanya
kazi kama makampuni ya simu kwa kufuata wateja kule waliko ili idadi ya
wateja hao iongezeke na hivyo mapato ya Shirika kuongezeka.
Katika hatua nyingine, Dkt
Kalemani alisema kuwa, kuanzia sasa miradi yote ya TANESCO
inayotekelezwa kwa fedha za ndani itasimamiwa na wataalam wa ndani ya
nchi ukiwemo mradi mkubwa wa kuzalisha umeme wa Julius Nyerere (MW
2115).
” Niwapongeze TANESCO kwa
kusimamia mradi huu mkubwa wa Julius Nyerere, zamani tulikuwa
tukisimamiwa lakini sasa tunawasimamia wakandarasi na hii inaokoa fedha
za Serikali ambazo zingetumika kutafuta wasimamizi wa miradi kutoka nje
ya nchi kuja kusimamia miradi yetu.” alisema Waziri wa Nishati
Kuhusu suala la umeme vijijini,
Dkt. Kalemani alisema kuwa bei ya umeme vijijini ni shilingi 27,000 bila
kujali umbali aliopo mteja hivyo kila mtumishi ahakikishe hilo
linatekelezeka.
Aidha, aliagiza wataalam wa
TANESCO kuacha mara moja lugha lugha ya “hakuna vifaa” ambayo mara
kadhaa imekuwa ikitumika wakati wateja wanapotaka kuunganishiwa umeme na
kueleza kuwa vifaa vya umeme kama vile nguzo, mita, transfoma na nyaya
vinazalishwa ndani ya nchi na kupatikana kwa urahisi hivyo lugha za
visingizio zisiwepo.]
Kwa upande wake, Mkurugenzi wa
Utawala na Rasilimali Watu, Raphael Nombo alizungumza na wafanyakazi hao
kuhusu masuala ya muundo wa TANESCO, mikataba ya wafanyakazi na suala
la mishahara.
TANESCO, Kanda ya Kaskazini inajumuisha mikoa minne ambayo ni Kilimanjaro, Arusha, Tanga na Manyara.
0 comments:
Post a Comment