Dar es Salaam. Baada ya kukosa soko la uhakika
kwa miezi mitatu huku wakulima vijijini wakilazimika kuuza mbaazi zao
kati ya Sh150 na 200 kwa kilo, hatimaye masoko matatu yamepatikana nje
ya nchi.
Masoko hayo yametajwa kuwa katika nchi za
Dubai, Afrika Kusini na Uingereza. Katika baadhi ya maeneo ya vijijini
ikiwamo mkoani Lindi, wakulima wa mbaazi wanauza hadi Sh150 kwa kilo.
Kudorora kwa soko la mbaazi nchini kulitokana na baadhi ya nchi ikiwamo India kuzuia uingizwaji wa zao hilo kutoka Tanzania.
Mkurugenzi
wa Kampuni ya Quality Pulse Exporters, George Fererra alisema jana
kuwa, kuanzia sasa wameanza kufungasha mbaazi baada ya kupata masoko
hayo.
Kampuni hiyo ambayo ipo katika Mamlaka ya Ukanda
Maalumu wa Uwekezaji (EPZA), ililazimika kusitisha ununuzi na
ufungashaji wa zao hilo, huku mzigo wenye thamani ya Dola 500,000 za
Marekani (sawa na zaidi ya Sh1 bilioni) ukikosa soko.
Ferrera
alisema uamuzi wa India kusitisha ununuzi wa mbaazi kutoka Tanzania
umewaathiri wakulima na wafanyabiashara kutokana na kuporomoka bei kwa
kuwa zilikuwa zikiuzwa kwa wingi nchini humo.
“Kampuni
nyingi za Tanzania zilitegemea soko la India pekee na hatukuangalia
sehemu nyingine. Hili ndilo kosa kubwa tulilolifanya,” alisema.
Mkurugenzi
wa Mipango na Maendeleo wa EPZA, Lamau Mpolo alisema ili kukabiliana na
ushindani wa soko ni muhimu kwa viwanda kuongeza tija kwenye
uzalishaji.
0 comments:
Post a Comment