Katibu
Mkuu Ofisi ya Waziri Mkuu (Sera, Uratibu na Uwekezaji) Bi. Dorothy
Mwaluko pamoja na Mkurugenzi wa Mfuko wa Kimataifa wa Maendeleo ya
Kilimo, IFAD kwa nchi za Tanzania na Rwanda Bw. Francesco Rispoli
wakiweka saini ya mkataba wa Makubaliano ya Awali ya Programu ya
Kuendeleza Sekta ya Uvuvi na Uzalishaji wa Mbegu Bora za Mazao ya
Kilimo.Mikataba hiyo imesainiwa Oktoba 11, 2019 katika Ukumbi wa
Mikutano wa Ofisi ya Waziri Mkuu Dodoma.Katibu
Mkuu Ofisi ya Waziri Mkuu (Sera, Uratibu na Uwekezaji) Bi. Dorothy
Mwaluko akimkabidhi Mkurugenzi wa Mfuko wa Kimataifa wa Maendeleo ya
Kilimo, IFAD kwa nchi za Tanzania na Rwanda Bw. Francesco Rispoli nakala
ya mkataba wa Makubaliano ya Awali ya Programu ya Kuendeleza Sekta ya
Uvuvi na Uzalishaji wa Mbegu Bora za Mazao ya Kilimo mara baada ya zoezi
la uwekaji saini mkataba huo, Mikataba hiyo imesainiwa Oktoba 11, 2019
katika Ofisi ya Waziri Mkuu Dodoma.Katibu
Mkuu Ofisi ya Waziri Mkuu (Sera, Uratibu na Uwekezaji) Bi. Dorothy
Mwaluko akizungumza wakati wa kikao cha uwekaji saini wa Makubaliano ya
Awali ya Programu ya Kuendeleza Sekta ya Uvuvi na Uzalishaji wa Mbegu
Bora za Mazao ya Kilimo.Mikataba hiyo imesainiwa Oktoba 11, 2019 katika
Ukumbi wa Mikutano wa Ofisi ya Waziri Mkuu Dodoma.Katibu
Mkuu Ofisi ya Waziri Mkuu (Sera, Uratibu na Uwekezaji) Bi. Dorothy
Mwaluko pamoja na Katibu Mkuu Uvuvi Dkt. Rashid Tamatama wakipitia
Mkataba wa Makubaliano ya Awali ya Programu ya Kuendeleza Sekta ya Uvuvi
na Uzalishaji wa Mbegu Bora za Mazao ya Kilimo kabla ya zoezi la utiaji
saini wa mkataba huo kati ya Serikali na Mfuko wa Kimataifa wa
Maendeleo ya Kilimo Oktoba 11, 2019.Katibu
Mkuu Ofisi ya Waziri Mkuu (Sera, Uratibu na Uwekezaji) Bi. Dorothy
Mwaluko akimkabidhi nakala ya Mkataba wa Makubaliano ya Awali ya
Programu ya Kuendeleza Sekta ya Uvuvi na Uzalishaji wa Mbegu Bora za
Mazao ya Kilimo Mkurugenzi Idara ya Uratibu wa Sera na Shughuli za
Serikali wa Ofisi hiyo Bw. Paul Sangawe mara baada ya zoezi la utiaji
saini mikataba hiyo.Naibu
Katibu Mkuu Kilimo Profesa Siza Tumbo akimsikiliza Mkurugenzi Idara ya
Uratibu wa Sera na Shughuli za Serikali Ofisi ya Waziri Mkuu Bw. Paul
Sangawe (mwenye suti ya kaki) wakati wa zoezi la Uwekaji saini Mkataba
wa Makubaliano ya Awali ya Programu ya Kuendeleza Sekta ya Uvuvi na
Uzalishaji wa Mbegu Bora za Mazao ya Kilimo.Baadhi
ya washiriki wa kikao cha zoezi la uwekaji wa saini kati ya Serikali na
IFAD kuhusu Mkataba wa Makubaliano ya Awali ya Programu ya Kuendeleza
Sekta ya Uvuvi na Uzalishaji wa Mbegu Bora za Mazao ya Kilimo
wakifuatilia maelekezo ya Katibu Mkuu Ofisi ya Waziri Mkuu (Sera,
Uratibu na Uwekezaji) Bi Dorothy Mwaluko (hayupo pichani) wakati wa
kikao hicho.Baadhi
ya washiriki wa kikao cha zoezi la uwekaji wa saini Mkataba wa
Makubaliano ya Awali ya Programu ya Kuendeleza Sekta ya Uvuvi na
Uzalishaji wa Mbegu Bora za Mazao ya Kilimo wakifuatilia maelekezo ya
Katibu Mkuu Ofisi ya Waziri Mkuu (Sera, Uratibu na Uwekezaji) Bi Dorothy
Mwaluko (hayupo pichani) wakati wa kikao hicho.Baadhi
ya washiriki wa kikao cha zoezi la uwekaji wa saini Mkataba wa
Makubaliano ya Awali ya Programu ya Kuendeleza Sekta ya Uvuvi na
Uzalishaji wa Mbegu Bora za Mazao ya Kilimo wakifuatilia maelekezo ya
Katibu Mkuu Ofisi ya Waziri Mkuu (Sera, Uratibu na Uwekezaji) Bi Dorothy
Mwaluko (hayupo pichani) wakati wa kikao hicho. (PICHA ZOTE NA OFISI YA WAZIRI MKUU)
……………………
MWANDISHI WETU
Serikali kupitia Ofisi ya Waziri
Mkuu, Sera, Uratibu na Uwekezaji imeingia Mkataba na Mfuko wa Kimataifa
wa Maendeleo ya Kilimo (IFAD) kwa kusaini Makubaliano ya Awali ya
Programu ya Kuendeleza Sekta ya Uvuvi na Uzalishaji wa Mbegu Bora za
Mazao ya Kilimo nchini.
Mkataba huo ulisainiwa na Katibu
Mkuu wa Ofisi hiyo anayeshughulikia masuala ya sera, uratibu na
uwekezaji,Dorothy Mwaluko na Mkurugenzi wa IFAD kwa Nchi za Tanzania na
Rwanda Bw. Francesco Rispoli hii leo Oktoba 11, 2019 katika Ofisi Waziri
Mkuu Jijini Dodoma.
Mkataba huo wa awali umelenga
kuhakikisha kunakuwa na ongezeko la uzalishaji wa mbegu bora za mazao na
samaki na kuendelea kuwa na tija katika sekta ya kilimo na uvuvi.
Akizungumza kabla ya utiaji
saini wa mkataba huo, Katibu Mkuu wa ofisi hiyo amesema kuwa hatua hiyo
ni mwendelezo wa maboresho mbalimbali yanayoendelea kufanyika ili
kuwafikia wananchi katika kujiletea maendeleo kwa kuzingatia mchango wa
sekta ya Kilimo na Uvuvi nchini.
“Leo tumetia saini mkataba wa
makubaliano ya awali na Mfuko wa Kimataifa wa maendeleo ya Kilimo,
tunamatarajio makubwa katika hatua hii na huu ni mwanzo mzuri utakao
leta tija kwa maendeleo yetu,”allisema Mwaluko
Aidha, Mkurugenzi wa Mfuko huo
IFAD, Francesco Rispoli ameutaka Mfuko huo kutekeleza makubaliano hayo
ya awali kwa ufanisi, ikiwa ni pamoja kuzingatia maeneo yote kama
yalivyoainishwa katika mkataba huo.
Kwa upande wake Kaimu Mkurugenzi
wa Maendeleleo ya Biashara kutoka Wakala wa Mbegu za Kilimo (ASA) Bi.
Jackline Shayo alieeleza kuwa uwepo wa makubaliano hayo utaleta chachu
katika kuendeleza sekta ya kilimo na uvuvi kwa kuzingatia malengo ya
mkataba huo.
“Kipekee niipongeze Serikali kwa
hatua hii ya awali, matarajio ni makubwa hususan endapo Mfuko huu
utatekeleza malengo kama ilivyokusudiwa na itasaidia kuleta maendeleo
katika sekta ya kilimo kupitia uboreshwaji wa miundombinu ya uzalishaji
wa mbegu bora,”alisema Shayo.
0 comments:
Post a Comment