WAZIRI MKUU, Kassim Majaliwa
*Ni
baada ya wanafunzi 72 wa kike kupewa ujauzito wilayani Nyang’hwale
WAZIRI
MKUU, Kassim Majaliwa amechukizwa na vitendo vya watoto wa kike kukatisha
masomo yao kwa kupata ujauzito wilayani Nyang’hwale ambapo jumla ya wanafunzi
72 wamepata ujauzo katika kipindi cha miaka mitatu cha kuanzia mwaka 2016 hadi
2018.
Kutokana
na wilaya hiyo kuwa na idadi kubwa ya watoto wa kike wanaokatisha masomo
kutokana na ujauzito, Waziri Mkuu amemuagiza Mkuu wa wilaya ya Nyang’hwale
Hamim Gwiyama kufanya operesheni katika kila kijiji na kubaini waliowapa
wanafunzi ujauzito na kuwafikisha kwenye vyombo vya sheria.
Waziri
Mkuu aliyasema hayo jana jioni (Jumatano, Novemba 28, 2018) alipozungumza na
wananchi katika mkutano wa hadhara uliofanyika kwenye uwanja wa
Sabasaba, ,kijiji cha Kalumwawilaya ya Nyang’hwale, akiwa katika ziara
yake mkoani Geita.
“Jambo
lingine litakalowawezesha kukabiliana na tatizo la ujauzito kwa wanafunzi wa
kike ni kuanzisha miradi ya ujenzi wa mabweni ili watoto wa kike waweze kusoma
bila ya kupata vishawishi vinavyosababisha wao kupata ujauzito.”
Waziri
Mkuu alisema Serikali haiwezi kuacha jambo hilo likiendelea, hivyo aliwataka
wananchi washirikiane katika kuwalinda watoto wa kike na Serikali
itawachukulia hatua watendaji wote ambao katika maeneo yao watoto wa kike
watabainika kuwa na ujauzito.
“Watoto
wa kike lazima waheshimiwe waachwe wasome bila ya usumbufu na atakayekatisha
masomo adhabu yake ni kali. Tukikukuta umesimama na binti katika kona
isiyoeleweka tutakukamata. Ole wenumtakaobainika kuwapa ujauzito wanafunzi,
adhabu yake ni miaka 30 jela.”
Waziri
Mkuu pia, alitoa onyo kwa wazazi au walezi watakaowaozesha watoto kike ambao
bado ni wanafunzi na kwa upande wa wazazi watakaomsindikiza mtoto wao wa kiume
kwenda kuoa mwanafunzi wote watachukuliwa hatua za kisheria.
Katika
kuoneshwa kuchukizwa na jambo hilo, Naibu Waziri Ofisi ya Rais-TAMISEMI, Mwita
Waitara ambaye anashughulikia elimu, amemueleza Waziri Mkuu kwamba Novemba 30,
2018 yeye arudi wilayani hapo kwa ajili ya kuwashughulia wote
wanaokatisha masomo wanafunzi kike. Ametoa namba ya simu ili wananchi waanze
kumpa taarifa za wahusika.
Katika
hatua nyingine,Waziri Mkuu alisemaSerikali imedhamiria kusambaza
umeme katika vijiji vyote ambavyo bado havijaunganishiwa nishati hiyo nchini
vitaunganishiwa katika awamu ya tatu ya Mradi wa Nishati Vijijini (REA).
“Rais
wetu Dkt. John Magufuli anataka kuona nyumba ya kila Mtanzania inapata umeme
tena kwa gharama nafuu na ametenga fedha nyingi zitakazotosheleza kusambaza
umeme katika vijiji vyote nchini. Gharama za kuunganishiwa umeme huo ni sh.
27,000 tu.”
Kuhusu
suala la gharama za kulipia nguzo, Waziri Mkuu alisema wananchi hawatowajibika
tena katika kulipia gharama za nguzo pamoja na zile za fomu za maombi ya
kuunganishiwa umeme kwa sababu tayari gharama hizo zimeshabebwa na Serikali.
Awali,
Waziri Mkuu alitembelea kiwanda cha kuchenjua dhahabu cha Nyamigogo ambapo
alikagua miundombinu ya kiwanda hicho na kisha aliweka jiwe la msingi la ujenzi
wa kiwanda hicho, ambacho muwekezaji wake ni mzawa.
0 comments:
Post a Comment