NAIBU Waziri wa Mifugo na Uvuvi,
Abdallah Ulega,akizungumza na wafugaji kabla ya kuzindua kampeni ya
uhimilishaji ng’ombe (Kupandikiza ng’ombe mimba kwa njia ya chupa)
katika kambi ya Ranchi ya Kongwa jijini Dodoma.
Mkuu wa Wilaya ya Kongwa Mhe.Deogratius Ndejembi,akizungumza na wafugaji katika kambi ya Ranchi ya Kongwa jijini Dodoma.
Meneja wa Ranchi ya Kongwa Raymond
Lutege akitoa taarifa kwa Naibu Waziri wa Mifugo na Uvuvi, Abdallah
Ulega,ambaye amezindua kampeni ya uhimilishaji ng’ombe (Kupandikiza
ng’ombe mimba kwa njia ya chupa) katika kambi ya Ranchi ya Kongwa jijini
Dodoma.
Mwenyekiti wa wafugaji Kongwa
Bw.Mshando Palutu,akitoa mapendekezo kwa Naibu Waziri wa Mifugo na
Uvuvi, Abdallah Ulega,ambaye leo amezindua kampeni ya uhimilishaji
ng’ombe (Kupandikiza ng’ombe mimba kwa njia ya chupa) katika kambi ya
Ranchi ya Kongwa jijini Dodoma.
Sehemu ya wafugaji wakimsikiliza
Naibu waziri wa Mifugo na Uvuvi Mhe.Abdallah Ulega wakati akizungumza
kabla ya kwenda kuzindua kampeni ya uhimilishaji ng’ombe (Kupandikiza
ng’ombe mimba kwa njia ya chupa) katika kambi ya Ranchi ya Kongwa jijini
Dodoma
NAIBU Waziri wa Mifugo na Uvuvi,
Abdallah Ulega,akikagua malisho ya ng’ombe katika kambi ya Ranchi ya
Kongwa kabla ya kuzindua kampeni ya uhimilishaji ng’ombe (Kupandikiza
ng’ombe mimba kwa njia ya chupa).
NAIBU Waziri wa Mifugo na Uvuvi,
Abdallah Ulega,akiangalia ng’ombe wakati wa kuzindua kampeni ya
uhimilishaji ng’ombe (Kupandikiza ng’ombe mimba kwa njia ya chupa)
katika kambi ya Ranchi ya Kongwa jijini Dodoma.
NAIBU Waziri wa Mifugo na Uvuvi,
Abdallah Ulega,akipata maelezo kutoka kwa Mtaalam Mwandamizi Mkuu wa
Mifugo toka NAIC USA River,Philbert Balongo wakati wa kuzindua kampeni
ya uhimilishaji ng’ombe (Kupandikiza ng’ombe mimba kwa njia ya chupa)
katika kambi ya Ranchi ya Kongwa jijini Dodoma.
Mtaalam Mwandamizi Mkuu wa Mifugo
toka NAIC USA River,Philbert Balongo akichoma Sindano ng’ombe kwa njia
ya kupandikiza mimba kwa njia ya chupa katika kambi ya Ranchi ya Kongwa
jijini Dodoma.
NAIBU Waziri wa Mifugo na Uvuvi,
Abdallah Ulega,akizindua kampeni ya uhimilishaji ng’ombe (Kupandikiza
ng’ombe mimba kwa njia ya chupa) katika kambi ya Ranchi ya Kongwa jijini
Dodoma.
……………………….
Na Alex Sonna, Kongwa
NAIBU Waziri wa Mifugo na Uvuvi,
Abdallah Ulega amewahimiza wafugaji kuunga mkono zoezi la uhimilishaji
ng’ombe (Kupandikiza ng’ombe mimba kwa njia ya chupa) ili kuwa na tija
na kukidhi mahitaji ya viwanda nchini.
Ulega ametoa wito huo leo
alipokuwa akizindua kampeni uhimilishaji wa ng’ombe uliofanyika kambi la
Ranchi ya Kongwa, mkoani Dodoma.
Amesema lengo la kufanya
uhimilishaji huo ni kupata ng’ombe milioni moja kwa mwaka ili kuboresha
koosafu kutoka katika ng’ombe za asili na kuboresha zaidi.
“Lengo ni kuunga mkono jitihada za
rais za Tanzania ya viwanda, tunataka tupate ng’ombe wa kutosha wenye
tija wa kuingiza kwenye viwanda tunavyojenga, hivi sasa tunajenga
viwanda vingi sana vya uchinjaji na uchakataji wa mazao ya mifugo, sasa
hivi viwanda vyote vinahitaji malighafi na tunataka mifugo yetu iwe na
tija zaidi,”amesema.
Ameeleza kuwa pia wamedhamiria kupata ng’ombe ambao wana uwezo wa kuhimili magonjwa wanakuwa na kilo za kutosha na tija zaidi.
“Leo tumefanya uzinduzi katika
kambi hili la wilaya ya kongwa ambapo tulishafanya uzinduzi kambi la
mkoa wa Simiyu tumepata ng’ombe takribani laki saba, tutakwenda Rukwa,
Katavi.
“Hii sayansi yake ni kwamba
tunaowapandisha si wote watakaopata ndama, tuna makisio kati ya asilimia
60-70 ya kuhakikisha tunapata ndama, kwa hiyo tukipata katika ng’ombe
tunaowapandisha wa wafugaji wetu, hapa ranchi ya kongwa tumepata ng’ombe
67,000 walioonekana wana uwezo wa kufanyiwa zoezi hili,”amesema.
Naibu Waziri huyo amesema asilimia
60-70 ya ng’ombe hao wanatarajiwa kupata mimba,huku akiwataka wafugaji
wote nchini kuunga mkono serikali katika zoezi hilo la uboreshaji
koosafu.
“Tuna njia ya upandishaji kwa
kutumia mirija kwa maana ya chupa, vilevile tunayo njia nyingine ya
kutumia viini tete itakapokuwa tayari tutaisambaza, lakini kwasasa
tunayo njia ya kutumia mirija, tumetoa mbegu hizi bure katika makambi
haya yote tunayofanyia upandishaji, mfugaji atachangia Sh.5,000 kwa
ajili ya ng’ombe kuchomwa homoni,”amesema.
Naye, Mfugaji Anuari Bahanusi
ameshukuru serikali kwa zoezi hilo na kwamba wamelipokea wakiamini kuwa
ng’ombe zao zitakuwa na thamani.
Ametoa rai kwa wafugaji wote kuunga mkono zoezi hilo ili mifugo yao iwe na tija.
0 comments:
Post a Comment