Na Faustine Ruta, Bukoba.
Mchungaji
King James wa Kanisa la Pentekoste Assemblies of God (P.A.G) kutoka
Maeneo ya Kahororo Kyamaizi Bukoba, King James ambaye pia ni mmoja wa
wadau wa maendeleo Manispaa ya Bukoba jana jumatano septemba 14, 2016
jioni amewatembelea Waathiriwa wa Tetemeko na kuwafariji Wananchi. Ni
baada ya maafa kutokea katika janga la tetemeko la ardhi, lililotokea
jummosi iliyopita mkoani hapa Kagera, ambapo imeripotiwa idadi ya vifo
kuongezeka na kufikia watu 17, huku wengine 253 wakijeruhiwa na
kusababisha simanzi na masikitiko kwa familia nyingi. Katika tukio hilo,
pia nyumba 840 za makazi zimeanguka, nyumba 1,264 zimepata nyufa kubwa
na majengo 44 ya taasisi mbalimbali zikiwemo shule kuanguka.
King
James ametembele sehemu tofauti tofauti kama Kata ya Hamugembe, Kashai,
Rwamishenye na kutoa Misaada ya dharura kama Mahema, mchele, Sukari na
Pesa taslimu na kuwaombea pia. Mchungaji James pia kesho ataendelea
kutoa Misaada kwa Wahanga wa Tetemeko la Ardhi la nguvu ya 5.7 katika
vipimo vya Richter lilitokea eneo la Bukoba, kaskazini magharibi mwa
Tanzania ambalo limeathiri sehemu kubwa ya Wanakagera kuanzia kwenye
Makazi yao na wengine kukosa makazi na mpaka sasa kulala nje kutokana na
nyumba zao kubomolewa.
Takribani
shilingi bilioni 1.4 zimepatikana mpaka sasa katika harambee
iliyoongozwa na serikali ili kusaidia athari za tetemeko la ardhi hapa
mkoani Kagera.
Hamugembe
Omukishenye ni sehemu kubwa iliyoathiriwa na tetemeko la Ardhi na
Nyumba Nyingi kuanguka na nyingi kubomoka huku ikiwa imepoteza zaidi ya
Wakazi 6.
Wengi mpaka sasa wanapikia nje baada ya nyumba zao kubomolewa.
Moja ya Nyumba iliyobomolewa na Tetemeko ndani ya Mtaa wa Hamugembe Omukishenye.
King
James wa Kanisa la Pentekoste Assemblies of God (P.A.G) Bukoba akiteta
na Watoto Yatima katika Kituo hicho chenye makazi yake Hamugembe.
Bi. Saada
akishukuru kwa Msaada aliopokea kutoka kwa King James ambao ni wa
dharura kutokana na Tetemeko la Ardhi lililotokea hivi karibuni.
King
James wa Kanisa la Pentekoste Assemblies of God (P.A.G) akitoa Misaada
ya Mchele katika kituo hicho cha Yatima ambacho ni kikongwe katika Mji
huu wa Bukoba ambacho mpaka sasa kinalea watoto zaidi ya 36.
Mtoto
mdogo zaidi anayelelewa katika kituo hicho cha yatima kilichopo
Hamugembe ambaye ameokotwa hivi karibuni mwezi uliopita ambaye King
James ameguswa nae.
King
James wa Kanisa la Pentekoste Assemblies of God (P.A.G) akiwa amebeba
Mtoto Mchanga aliyeokotwa hivi karibuni na wapita njia na kumpeleka
katika kituo hicho. Mchungaji James amehaidi kukisaidia kituo hicho kwa
kukijengea Vyumba Viwili vya kulala.
Furaha
kwa Mama Saada mama Mlezi wa Watoto Yatima baada ya kutembelewa na
kupokea Misaada, Na hapa akiwashukuru wageni hao waliompatia msaada huo
wa Dharura katika kipindi hiki kigumu kinachowalaza nje baada ya Nyumba
yao kuangushwa na Tetemeko la Ardhi lililotokea Jumamosi septemba 10,
2016.
0 comments:
Post a Comment