Thursday, October 10, 2019

NAIBU WAZIRI ULEGA AWATAKA WAFUGAJI KUUNGA MKONO ZOEZI LA UHIMILISHAJI NG’OMBE (KUPANDIKIZA NG'OMBE MIMBA KWA NJIA YA CHUPA)


NAIBU Waziri wa Mifugo na Uvuvi, Abdallah Ulega,akizungumza na wafugaji kabla ya kuzindua kampeni ya uhimilishaji ng’ombe (Kupandikiza ng’ombe mimba kwa njia ya chupa) katika kambi ya Ranchi ya Kongwa jijini Dodoma.
Mkuu wa Wilaya ya Kongwa Mhe.Deogratius Ndejembi,akizungumza na wafugaji  katika kambi ya Ranchi ya Kongwa jijini Dodoma.
Meneja wa Ranchi ya Kongwa Raymond Lutege akitoa taarifa kwa Naibu Waziri wa Mifugo na Uvuvi, Abdallah Ulega,ambaye amezindua kampeni ya uhimilishaji ng’ombe (Kupandikiza ng’ombe mimba kwa njia ya chupa) katika kambi ya Ranchi ya Kongwa jijini Dodoma.
Mwenyekiti wa wafugaji Kongwa Bw.Mshando Palutu,akitoa mapendekezo kwa Naibu Waziri wa Mifugo na Uvuvi, Abdallah Ulega,ambaye leo amezindua kampeni ya uhimilishaji ng’ombe (Kupandikiza ng’ombe mimba kwa njia ya chupa) katika kambi ya Ranchi ya Kongwa jijini Dodoma.
Sehemu ya wafugaji wakimsikiliza Naibu waziri wa Mifugo na Uvuvi Mhe.Abdallah Ulega wakati akizungumza kabla ya kwenda kuzindua kampeni ya uhimilishaji ng’ombe (Kupandikiza ng’ombe mimba kwa njia ya chupa) katika kambi ya Ranchi ya Kongwa jijini Dodoma

NAIBU Waziri wa Mifugo na Uvuvi, Abdallah Ulega,akikagua malisho ya ng’ombe katika kambi ya Ranchi ya Kongwa kabla ya kuzindua kampeni ya uhimilishaji ng’ombe (Kupandikiza ng’ombe mimba kwa njia ya chupa).
NAIBU Waziri wa Mifugo na Uvuvi, Abdallah Ulega,akiangalia ng’ombe  wakati wa kuzindua kampeni ya uhimilishaji ng’ombe (Kupandikiza ng’ombe mimba kwa njia ya chupa) katika kambi ya Ranchi ya Kongwa jijini Dodoma.
NAIBU Waziri wa Mifugo na Uvuvi, Abdallah Ulega,akipata maelezo kutoka kwa Mtaalam Mwandamizi Mkuu wa Mifugo toka NAIC USA River,Philbert Balongo wakati wa  kuzindua kampeni ya uhimilishaji ng’ombe (Kupandikiza ng’ombe mimba kwa njia ya chupa) katika kambi ya Ranchi ya Kongwa jijini Dodoma.
Mtaalam Mwandamizi Mkuu wa Mifugo toka NAIC USA River,Philbert Balongo akichoma Sindano ng’ombe kwa njia ya kupandikiza mimba kwa njia ya chupa katika kambi ya Ranchi ya Kongwa jijini Dodoma.
NAIBU Waziri wa Mifugo na Uvuvi, Abdallah Ulega,akizindua kampeni ya uhimilishaji ng’ombe (Kupandikiza ng’ombe mimba kwa njia ya chupa) katika kambi ya Ranchi ya Kongwa jijini Dodoma.

……………………….
Na Alex Sonna, Kongwa
NAIBU Waziri wa Mifugo na Uvuvi, Abdallah Ulega amewahimiza wafugaji kuunga mkono zoezi la uhimilishaji ng’ombe (Kupandikiza ng’ombe mimba kwa njia ya chupa) ili kuwa na tija na kukidhi mahitaji ya viwanda nchini.


Ulega ametoa wito huo leo alipokuwa akizindua kampeni uhimilishaji wa ng’ombe uliofanyika kambi la Ranchi ya Kongwa, mkoani Dodoma.

Amesema lengo la kufanya uhimilishaji huo ni kupata ng’ombe milioni moja kwa mwaka ili kuboresha koosafu kutoka katika ng’ombe za asili na kuboresha zaidi.

“Lengo ni kuunga mkono jitihada za rais za Tanzania ya viwanda, tunataka tupate ng’ombe wa kutosha wenye tija wa kuingiza kwenye viwanda tunavyojenga, hivi sasa tunajenga viwanda vingi sana vya uchinjaji na uchakataji wa mazao ya mifugo, sasa hivi viwanda vyote vinahitaji malighafi na tunataka mifugo yetu iwe na tija zaidi,”amesema.

Ameeleza kuwa pia wamedhamiria kupata ng’ombe ambao wana uwezo wa kuhimili magonjwa wanakuwa na  kilo za kutosha na tija zaidi.

“Leo tumefanya uzinduzi katika kambi hili la wilaya ya kongwa ambapo tulishafanya uzinduzi kambi la mkoa wa Simiyu tumepata ng’ombe takribani laki saba, tutakwenda Rukwa, Katavi.

“Hii sayansi yake ni kwamba tunaowapandisha si wote watakaopata ndama, tuna makisio kati ya asilimia 60-70 ya kuhakikisha tunapata ndama, kwa hiyo tukipata katika ng’ombe tunaowapandisha wa wafugaji wetu, hapa ranchi ya kongwa tumepata ng’ombe 67,000 walioonekana wana uwezo wa kufanyiwa zoezi hili,”amesema.

Naibu Waziri huyo amesema asilimia 60-70 ya ng’ombe hao wanatarajiwa kupata mimba,huku akiwataka wafugaji wote nchini kuunga mkono serikali katika zoezi hilo la uboreshaji koosafu.


“Tuna njia ya upandishaji kwa kutumia mirija kwa maana ya chupa, vilevile tunayo njia nyingine ya kutumia viini tete itakapokuwa tayari tutaisambaza, lakini kwasasa tunayo njia ya kutumia mirija, tumetoa mbegu hizi bure katika makambi haya yote tunayofanyia upandishaji, mfugaji atachangia Sh.5,000 kwa ajili ya ng’ombe kuchomwa homoni,”amesema.


Naye, Mfugaji Anuari Bahanusi ameshukuru serikali kwa zoezi hilo na kwamba wamelipokea wakiamini kuwa ng’ombe zao zitakuwa na thamani.


Ametoa rai kwa wafugaji wote kuunga mkono zoezi hilo ili mifugo yao iwe na tija.

No comments:

Post a Comment