![](https://fullshangweblog.co.tz/wp-content/uploads/2019/10/1-64.jpg)
Mbunge wa Geita Mjini ambaye pia ni Naibu Waziri wa Maliasili na Utalii, Mhe. Constantine akizungmza na wahitimu wa kidato cha nne wapatao 263 yaliyofanyika leo katika shule ya Sekondari ya Shantamine iliyoko mkoani Geita.
![](https://fullshangweblog.co.tz/wp-content/uploads/2019/10/2-54.jpg)
Baadhi ya Wahitimu wa kidato cha nne wakituimbiza wimbo wa kuwaaga wanafunzi wenzoa katika mahafali yao yaliyofanyika katika shule ya Sekondari ya Shantamine.
![](https://fullshangweblog.co.tz/wp-content/uploads/2019/10/3-43.jpg)
Mbunge wa Geita Mjini ambaye pia ni Naibu Waziri wa Maliasili na Utalii, Mhe. Constantine Kanyasu akimkabidhi cheti mwanafunzi bora, Editha Karlo aliyekuwa akiongoza masomo kwa jumla ya Wahitimu 263 wa kidato cha nne wakati wa mahafali yaliyofanyika leo katika shule ya Sekondari ya Shantamine iliyoko mkoani Geita.
![](https://fullshangweblog.co.tz/wp-content/uploads/2019/10/5-28.jpg)
Diwani wa kata ya Mtakuja, Constantine Morandi akizungumza na wahitimu wa kidato cha nne kabla ya Mbunge wa Geita Mjini, Mhe. Constantine Kanyasu akizungumza na baadhi ya wahitimu wa kidato cha nne wapatao 263.
************************
NA MWANDISHI WETU- GEITA
Mbunge wa Geita
Mjini ambaye pia ni Naibu Waziri wa Maliasili na Utalii, Mhe.
Constantine Kanyasu ameahidi kutoa kiasi cha shilingi milioni 20 kwa
ajili ya kukamilisha ujenzi wa ukumbi wa chakula katika shule ya
Sekondari ya Shantamine.
Amesema ataitoa
fedha hiyo kwa ajili ya kupunguza adha kwa wanafunzi wa shule hiyo
wanaolazimika kukaa nje wakati wa kula chakula hasa katika kipindi cha
mvua.
Ahadi hiyo
ameitoa leo mkoani Geita wakati alipokuwa akizungumza na jumla
ya Wahitimu 263 wa kidato cha
nne kwenye mahafali yaliyofanyika katika Shule ya Sekondari ya
Shantamine.
Ombi hilo
linakuja kufuatia risala iliyosomwa kwake na Wahitimu wa kidato cha nne
wakiomba kukamilishiwa ujenzi wa ukumbi huo utakaoweza kuwahudumia
wanafunzi wengi kutokana na idadi yao kuongezeka hali inayowalazimu
kupata shida wakati mvua ikiwa inanyesha
Katika hatua
nyingine, Mhe. Kanyasu ameahidi kuchimba kisima kirefu zaidi katika
shule hiyo kwa ajili ya kuwasaidia wanafunzi wa kike wanaolazimika
kutoka nje ya shule kutafuta maji
Ameeleza
kuwa maombi kwa ajili ya uchimbaji wa kisima hicho
yamewashawasilishwa katika wizara ya Elimu na Mafunzo ya Ufundi na
wanachosubili ni utaratibu wa namna ya kukichimba kisima hicho.
Hata hivyo Mhe.
Kanyasu ameeleza kuwa jumla ya visima viwili vilishachimbwa katika
shule hiyo lakini ilibainika kuwa havina maji na eneo hilo lilionekana
kuwa maji yake yana chumvi sana.
Akizungumzia
kuhusu ombi la kupatiwa umeme katika shule hiyo, Mhe. Kanyasu amesema
ifikapo mwezi mei mwakani shule hiyo itakuwa tayari ina umeme.
Aidha, Mhe.
Kanyasu amewaahidi wanafunzi wa shule hiyo kuwa atashirikiana na
madiwani wa Halmashauri ya Mji wa Geita kujenga mabweni kadiri pesa
inavyojitokeza ili kuwanusuru wanafunzi wanaolazimika kupanga nyumba nje
ya shule hali inayopelekea wanafunzi wengi wa kike kuacha masomo baada
ya kupata mimba.
Mbali na hilo,
Mhe. Kanyasu amewatakia heri wahitimu hao katika mitihani yao na
kuwataka wasiridhikena elimu hiyo na badala yake wajiendeleze zaidi
Naye. Diwani wa
Kata ya Mtakuja. Constantine Morandi amewataka wananfunzi hao wajiandae
kikamilifu katika mitihani ya kuhitimukidato cha nne ili kuweza kuileta
sifa shule hiyo
‘’Nina washukuru wazazi pamoja na waalimu kwa ushirikiano wenu katika kuhakikisha wanafunzi 263 wanahitimu masomo yao’
Akizungumza
mhitimu wa kidato cha nne kwa niaba ya wenzake , Anna Masumbuko amesema
wapo tayari kwa ajili ya mtihani wa mwisho na wanategemea kufaulu
vizuri katika mitihani yao.
Kwa upande wake
Mkuu wa shule hiyo, Kikula Swillah amesema wanafunzi hao wamejianda vema
na shule inategemea wanafunzi watafaulu na kujiunga na kidato cha tano
na wengine waliobaki watachaguliwa katika vyuo vya ufundi
0 comments:
Post a Comment