![](https://fullshangweblog.co.tz/wp-content/uploads/2019/10/P-1-4.jpg)
Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri
Mkuu anayeshughulikia masuala ya Sera, Bunge, Kazi, Vijana, Ajira na
Wenye Ulemavu Mhe. Jenista Mhagama akizungumza na vijana wakati wa
bonanza la michezo katika wiki ya vijana lililofanyika Mkoani Lindi
Oktoba 12, 2019.
![](https://fullshangweblog.co.tz/wp-content/uploads/2019/10/P-2-4.jpg)
Mkuu wa Mkoa wa Lindi, Mhe. Godfrey Zambi akizungumza wakati wa kongamano hilo.
![](https://fullshangweblog.co.tz/wp-content/uploads/2019/10/P-3-3.jpg)
Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri
Mkuu anayeshughulikia masuala ya Sera, Bunge, Kazi, Vijana, Ajira na
Wenye Ulemavu Mhe. Jenista Mhagama akiangalia mchezo wa Bao walipokuwa
wakishindana Mzee Said Masteti na Abdallah Makwela. (Wa nne kulia
waliokaa) ni Waziri wa Vijana, Utamaduni, Sanaa na Michezo Mhe. Balozi
Ali Karume na Naibu Waziri, Ofisi ya Waziri Mkuu (Kazi, Vijana na Ajira)
Mhe. Anthony Mavunde. Mchezo huo wa Bao alipenda kuucheza Baba wa Taifa
Mwl. Julius Kambarage Nyerere.
![](https://fullshangweblog.co.tz/wp-content/uploads/2019/10/P-4-3.jpg)
Vijana kutoka Shule ya Lindi Sekondari na angaza wakiwa uwanjani wakicheza mpira wa pete wakati wa bonanza hilo.
![](https://fullshangweblog.co.tz/wp-content/uploads/2019/10/P-5-3.jpg)
Mchezaji wa timu ya Sekondari ya
Lindi Mwalimu Said (wenye jezi ya bluu) akijaribu kuwatoka wachezaji wa
Angaza wakati wa bonanza hilo lililofanyika katika viwanja vya Shule ya
Sekondari ya Lindi.
![](https://fullshangweblog.co.tz/wp-content/uploads/2019/10/P-6-3.jpg)
Sehemu ya vijana wakifuatailia
mchezo wa mpira wa miguu utambulikao kama soka mara baada ya bonanza
hilo kufunguliwa na Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu
anayeshughulikia masuala ya Sera, Bunge, Kazi, Vijana, Ajira na Wenye
Ulemavu Mhe. Jenista Mhagama Oktoba 12, 2019.
![](https://fullshangweblog.co.tz/wp-content/uploads/2019/10/P-7-2.jpg)
Baadhi ya Viongozi pamoja na
wakazi wa Lindi wakifuatilia michizo ambayo ilikuwa ikiendelea katika
viwanja vya Shule ya lindi sekondari.
![](https://fullshangweblog.co.tz/wp-content/uploads/2019/10/P-8-2.jpg)
Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri
Mkuu anayeshughulikia masuala ya Sera, Bunge, Kazi, Vijana, Ajira na
Wenye Ulemavu Mhe. Jenista Mhagama akimkabidhi kombe kwa Mshindi wa
Kwanza wa Mchezo wa Bao Bw. Said Masteti ambao ulikuwa Mchezo unaopendwa
na Baba wa Taifa Mwl. Julius Kambarage Nyerere. (Wa tatu kutoka kulia
ni Waziri wa Vijana, Utamaduni, Sanaa na Michezo Mhe. Balozi Ali Karume.
Kulia ni Mkuu wa Mkoa wa Lindi, Mhe. Godfrey Zambi
PICHA ZOTE NA OFISI YA WAZIRI MKUU
(KAZI, VIJANA, AJIRA NA WENYE ULEMAVU)
…………………..
Na; Mwandishi Wetu
Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri
Mkuu anayeshughulikia masuala ya Sera, Bunge, Kazi, Vijana, Ajira na
Wenye Ulemavu Mhe. Jenista Mhagama amewamiza vijana nchini kutumia
michezo ili kuimarisha amani, upendo na mshikamano.
Waziri Mhagama alitoa kauli hiyo
wakati wa Bonanza la michezo kwa vijana lililofanyika katika shule ya
Sekondari Lindi ikiwa ni sehemu ya kuadhimisha wiki ya vijana nchini
kuelekea kilele cha mbio za mwenge wa uhuru kwa mwaka 2019 na Kumbukizi
ya Miaka 20 ya kifo cha Baba wa Taifa Mwl. Julius Kambarage Nyerere.
Akizungumza wakati wa ufunguzi wa
bonanza hilo ambalo vijana walikusanyika kwa lengo la kushiriki katika
michezo mbalimbali, Mheshimiwa Mhagama alieleza kuwa michezo imekuwa
ikitumika kwa kiasi kikubwa katika kuimarisha ushirikiano na kuwajengea
vijana ari ya uzalendo.
“Kupitia michezo mnayofursa kama
vijana kuendelea kuenzi falsafa za waasisi wa taifa Mwl. Julius
Kambarage Nyerere na Hayati Mzee Abeid Amani Karume ambao walikuwa
wazalendo kwa taifa lao na waliimarisha muungano kwa maslahi ya
watanzania wote,” alisema Mhagama
“Ni matumaini yangu kuwa kupitia
michezo hii mtaendela kujikumbusha falsafa za waasisi hao kupitia
michezo hii tunayoifungua leo kwa kuwa itatoa hamasa kwa vijana kupenda
nchi yao na itajenga ari ya kuendeleza kuimarisha mshikamano kupitia
michezo,” alisema Mhagama
Aliongeza kuwa michezo hiyo iliyowakutaisha vijana ikatumike kama sehemu ya kuwa na amani, uvumilivu na mshikamano.
“Vijana mnatakiwa kujenga taifa
kwa vitendo vinavyodumisha amani, upendo na mshikamano kama ambavyo Baba
wa Taifa Mwl. Julius Kambarage Nyerere alivyotujengea taifa lenye
umoja,” alieleza Mhagama
Aidha Waziri Mhagama aliendelea
kuwasihi vijana kutambua wajibu wao katika jamii na kuifanya michezo
kuwa ni miongoni mwa mambo muhimu wanayopaswa kuyaendeleza katika
kutekeleza mipango waliyonayo.
Pamoja na hayo alirejea ujumbe wa
Mwenge wa uhuru mwaka huu ambao pia umesisitiza ushiriki wa wananchi
katika uchaguzi wa Serikali za Mtaa. Aliwaomba vijana kujitokeza kwa
wingi na kushiriki katika uchaguzi ili waweze kupata viongozi bora kwa
maendeleo ya taifa.
Waziri Mhagama alitumia fursa hiyo pia kuwapongeza wadau mbalimbali na vijana walioshiriki bonanza hilo.
Kwa upande wake Mkuu wa Mkoa wa
Lindi Mhe. Godfrey Zambi alisema kuwa Bonanza hilo la michezo
limejumuisha vijana kutoka sehemu mbalimbali ikiwa ni njia moja wapo ya
kuwaendeleza vijana ili waweze kuimarika kiafya na kiakili.
0 comments:
Post a Comment