Mkuu wa Mkoa wa Dar
es salaam Mhe. Paul Makonda leo October 16 ametembelea na kukagua ujenzi
wa Jengo la Gorofa tano la Mama na Mtoto Hospital ya Rufaa ya
Mwananyamala na kumtaka Mkandarasi wa jengo hilo Kutoka Chuo cha Sayansi
na Teknolojia Mbeya kuongeza kasi na masaa ya kazi ili akabidhi jengo
hilo kabla ya Disemba 30 mwaka huu.
RC Makonda amesema
ujenzi wa Jengo hilo ulisimama tangu mwaka 2014 lakini kupitia uongozi
thabiti wa Rais Dkt. John Magufuli aliona hilo changamoto hiyo na kuamua
kutoa zaidi ya Shilingi Billion 2.1 kwaajili ya kukamilisha ujenzi huo
ili kupunguza kero kwa wananchi.
Aidha RC Makonda
amesema Jengo hilo litaanza kutumika mwezi January mwakani ambapo ndani
yake litakuwa na uwezo wa kuchukuwa Vitanda 100 vya Mama na Mtoto na
fedha ya kununua Vifaa tiba ipo tayari.
Pamoja na hayo RC
Makonda amesema mbali na ujenzi wa Jengo hilo Serikali inaendelea na
ujenzi wa Hospital ya Wilaya Mabwepande na tayari yupo kwenye hatua za
kujenga Kituo cha Afya Kawe na Bunju ambapo miradi yote ikikamilika
itasaidia kumaliza Changamoto za Afya Wilaya ya Kinondoni.
0 comments:
Post a Comment