![](https://fullshangweblog.co.tz/wp-content/uploads/2019/10/N-1-1.jpg)
Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri
Mkuu anayeshughulikia Sera, Bunge, Kazi, Vijana, Ajira na Wenye Ulemavu
Mhe. Jenista Mhagama akizungumza na vijana walionufaika na mafunzo ya
ukuzaji ujuzi kupitia teknolojia ya kitalu nyumba (Greenhouse) katika
kijiji cha Chimbila “A” alipotembelea eneo hilo kukagua maendeleo ya
mafunzo hayo Wilayani Ruangwa.
![](https://fullshangweblog.co.tz/wp-content/uploads/2019/10/N-2-1.jpg)
Sehemu ya Vijana walionufaika na
Mafunzo hayo ya Kilimo cha Kisasa kwa kutumia teknolojia ya Kitalu
Nyumba wakimsikiliza Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu
anayeshughulikia masuala ya Sera, Bunge, Kazi, Vijana, Ajira na Wenye
Ulemavu Mhe. Jenista Mhagama (hayupo pichani) alipowatembelea kwa ajili
ya kukagua maendeleo ya mafunzo yao.
![](https://fullshangweblog.co.tz/wp-content/uploads/2019/10/N-3-1.jpg)
Bw. Lucas Mwindima ambaye ni mmoja
wa wanufaika wa mafunzo hayo akitoa taarifa fupi kuhusu mafanikio
waliyopata kupitia teknolojia ya kilimo cha Kitalu Nyumba.
![](https://fullshangweblog.co.tz/wp-content/uploads/2019/10/N-4-1.jpg)
Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri
Mkuu (Sera, Bunge, Kazi, Vijana, Ajira na Wenye Ulemavu) Mhe. Jenista
Mhagama akieleza jambo alipokuwa akigagua Kitalu nyumba kilichojegwa
katika Kijiji cha Chimbila “A” kilichopo Wilayini Ruangwa. Kulia ni Bw.
Lucas Mwindima ambaye ni mmoja wa wanufaika wa mafunzo hayo.
![](https://fullshangweblog.co.tz/wp-content/uploads/2019/10/N-5-1.jpg)
Naibu Waziri, Ofisi ya Waziri Mkuu
anayeshughulikia Kazi, Vijana na Ajira Mhe. Anthony Mavunde akizungumza
na vijana wa Kikundi cha Ruwangwa Materials wanaojihusisha na
utengenezaji wa matofali walipotembelea kikundi hiko kukagua maendeleo
ya mradi wao. Kulia ni Mkuu wa Wilaya ya Ruangwa Mhe. Hashim Mgandilwa.
![](https://fullshangweblog.co.tz/wp-content/uploads/2019/10/N-6-1.jpg)
Kiongozi wa Kikundi cha Ruagwa
Materials Bw. Mohammed Moshi akisoma taarifa fupi kuhusu utekelezaji wa
mradi wao walipotembelewa na Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu (Sera,
Bunge, Kazi, Vijana, Ajira na Wenye Ulemavu) Mhe. Jenista Mhagama. (Wa
tatu kutoka kulia) ni Waziri wa Vijana, Utamaduni, Sanaa na Michezo
kutoka Serikali ya Mapinduzi Zanzibar Mhe. Balozi Ali Abeid Karume na
Naibu Waziri, Ofisi ya Waziri Mkuu anayeshughulikia Kazi, Vijana na
Ajira Mhe. Anthony Mavunde. Kushoto ni Katibu Mkuu, Ofisi ya Waziri Mkuu
Bw. Andrew Massawe.
![](https://fullshangweblog.co.tz/wp-content/uploads/2019/10/N-7-1.jpg)
Baadhi ya Vijana wa Kikundi cha
Ruangwa Materials wakimsikiliza Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu
(Sera, Bunge, Kazi, Vijana, Ajira na Wenye Ulemavu) Mhe. Jenista Mhagama
(hayupo pichani), alipowatembea kwa lengo la kukagua maendeleo ya
kikundi hicho.
PICHA ZOTE NA OFISI YA WAZIRI MKUU
(KAZI, VIJANA, AJIRA NA WENYE ULEMAVU)
……………………………..
Na; Mwandishi Wetu
Vijana Wilayani Ruagwa
wameipongeza Serikali kwa kuwawezesha kupata mafunzo ya kilimo cha
Kisasa kwa kutumia teknolojia ya kitalu nyumba (Greenhouse) ambayo
yamekuwa ni chachu kwao kujikwamua kiuchumi.
Pongezi hizo zimetolewa Oktoba 11,
2019 wakati wa ziara ya Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu
anayeshughulikia masuala ya Sera, Bunge, Kazi, Vijana, Ajira na Wenye
Ulemavu Mhe. Jenista Mhagama alipotembelea vijana hao katika Kijiji cha
Chimbila “A” kilichopo Wilaya ya Ruagwa kukagua maendeleo ya mafunzo
waliyopata vijana kupitia teknolojia ya Kitalu Nyumba.
Mheshimiwa Mhagama alieleza kuwa
Serikali kupitia Ofisi ya Waziri Mkuu imeonesha kuwajali, kuwatambua na
kuwathamini vijana kwa kuwapatia mafunzo hayo ambayo yamekuwa
yakiwasaidia sana katika kuwaendeleza vijana kulima kwa mkakati.
“Mafunzo hayo yamewajengea uwezo
vijana wa kushiriki kwa wingi kwenye kilimo cha aina hii kwa kuwa
kinatija na ufanisi, hivyo vijana watakuwa kupata mavuno zaidi katika
eneo dogo kuliko eneo la wazi, uwezo wa kupata soko la mazao utakuwa wa
uhakika, matumizi ya maji ni madogo katika kilimo hiko na hudhibiti
viwatilifu,” alisema Mhagama
Alieleza kuwa Ofisi ya Waziri Mkuu
ilianzisha Programu ya Ukuzaji Ujuzi ikiwemo mafunzo hayo ya kilimo cha
Kisasa ikiwa ni mkakati wa serikali baada ya kubaini asilimia 56 ya
nguvukazi nchini ambao ni vijana wamekuwa na changamoto ya ajira, katika
kutatua changamoto hiyo kundi hilo limewezeshwa kwa kujengewa uwezo wa
kupatiwa ujuzi katika fani mbalimbali.
Waziri Mhagama aliongeza kuwa
Mafunzo hayo ya kilimo kupitia teknolojia ya kitalu nyumba yatawasaidia
kuboresha stadi bora za kilimo kwa vijana hususan waliopo vijijini ili
waweze kujiajiri, kuajiri wenzao na kushiriki katika shughuli mbalimbali
za kimaendeleo.
Aidha aliwasihi vijana kuendelea
kutunza vitalu nyumba hivyo kwa kuwa watanufaika kiuchumi na sambamba na
kuwaleta maendeleo yao na jamii kwa ujumla.
Baadhi ya vijana walionufaika na
mradi huo akiwemo Bw. Lucas Mwindima alisema kuwa Serikali ya Awamu ya
Tano inayoongozwa na Mhe. Rais, Dkt. John Pombe Magufuli imeonesha
dhamira ya dhati katika kuwawezesha vijana wanapata ujuzi
utakaowawezesha kukuza ujuzi wao na kuwaondoa katika hali ya umaskini.
“Tunamshukuru Rais Magufuli kwa
kutuwezesha vijana kupata mafunzo haya ya kilimo cha kitaalamu
yaliyoleta tija tunaona uzalishaji wa mazao ulivyokua tofauti na zamani
na mazao tunayozalisha yanafursa ya kupata masoko ndani au nje ya nchi,”
alisema Mwindima
Katika kupongeza jitihada hizo
wanufaika wa programu ya kilimo hicho walibainisha mafanikio mbalimbali
ikiwemo kupata ujuzi wa kilimo cha mazao biashara pamoja na ongezeko la
ajira kwa vijana waliowezeshwa elimu hiyo.
Pia Waziri Mhagama alitembelea
kikundi cha Ruangwa Materials ambacho kimenufaika na Mkopo wa Maendeleo
ya Vijana unaoratibiwa na Ofisi yake kupitia Idara ya Manedleo ya
Vijana.
0 comments:
Post a Comment