![](https://fullshangweblog.co.tz/wp-content/uploads/2019/10/A-5.jpg)
Naibu Waziri wa Mambo ya Nje na
Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Dkt. Damas Ndumbaro akisalimiana na
Waziri wa Mambo ya Nje wa Angola, Vicente Muanda wakiwa katika ukumbi wa
mikutano, mjini Brazzaville jana
![](https://fullshangweblog.co.tz/wp-content/uploads/2019/10/B-1.jpg)
Balozi wa Tanzania Nchini DRC
Luteni. Jen. Paul Mella akimueleza jambo balozi wa sudan wakati wa
mkutano wa ukanda wa maziwa makuu mjini Brazzaville jana
![](https://fullshangweblog.co.tz/wp-content/uploads/2019/10/C-1.jpg)
Mawaziri wa Mambo ya Nje wa nchi wanachama wa ukanda wa maziwa makuu wakifuatilia mkutano ulifanyika jana Brazzaville jana
![](https://fullshangweblog.co.tz/wp-content/uploads/2019/10/D-1.jpg)
Naibu Waziri wa Mambo ya Nje na
Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Dkt. Damas Ndumbaro akiwasilisha
pendekezo la Kiswahili kutumika katika ukanda wa maziwa makuu mjini
Brazzaville jana
![](https://fullshangweblog.co.tz/wp-content/uploads/2019/10/E.jpg)
Mawaziri wa Mambo ya Nje wa nchi
wanachama wa ukanda wa maziwa makuu wakiwa katika picha ya pamoja na
Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Kongo, Bwn. Clement Mouamba jijini Brazzaville
jana
…………………….
Na Mwandishi wetu, Brazzaville,
Katika jitihada za kukuza lugha ya
Kiswahili barani Afrika, Tanzania imeziomba nchi wanachama wa ukanda wa
maziwa makuu kuanza kutumia lugha ya Kiswahili kama lugha rasmi na
lugha ya kazi
Wito huo umetolewa katika mkutano
wa mawaziri wa mambo ya nje wa nchi wanachama wa ukanda wa maziwa makuu,
uliofanyika mjini Brazzaville leo na Naibu Waziri wa Mambo ya Nje na
Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Dkt. Damas Ndumbaro
“Tumewaomba wenzetu wa maziwa
makuu wakubali lugha ya Kiswahili kutumika kama lugha rasmi na lugha ya
kazi katika nchi zote za maziwa makuu. Pia nchi sita ambazo zipo hapa na
hazijaridhia mabadiliko ya mkataba wa Afrika kuruhusu Kiswahili
kutumika kama lugha rasmi katika Afrika (AU) nchi hizo zimetuhakikishia
kuwa zitaridhia mabadiliko hayo ili kuhakikisha kuwa Kiswahili kinaanza
kutumika kama lugha rasmi ya kazi,” Alisema Dkt. Ndumbaro
Kwa mujibu wa Waziri Ndumbaro,
matumizi ya lugha ya Kiswahili katika ukanda huo ni fursa ambayo italeta
umoja wa kitaifa, na katika ukanda wa maziwa makuu lakini pia umuhimu
wa Kiswahili kwamba ni lugha pekee ambayo haina uhusiano na ukoloni
barani afrika.
“Tunatumaini kwamba tutazipata
sahihi za nchi sita na tukisha zipata tutabakiwa na sahihi ya nchi moja
tu ili Kiswahili kiwe rasmi lugha ya kazi katika mikutano itakayo kuwa
inafanyika barani Afrika,” aliongeza Dkt. Ndumbaro
Nchi sita ambazo hazijaridhia
mabadiliko ya mkataba wa Afrika kuhakikisha kuwa Kiswahili kinatumika
kama lugha rasmi ya kazi ni pamoja na Angola, Jamhuri ya Kidemokrasia ya
Kongo, Sudani, Uganda na Zambia.
Kwa sasa hivi ni lugha rasmi
lakini siyo lugha ya kazi kwa hiyo tumekwenda vizuri kwenye Kiswahili
tunaamini ni fursa nzuri ya kuanza kukuza lugha ya Kiswahili katika bara
la Afrika
Wakati huo huo, Dkt. Ndumbaro
aliongeza kuwa, katika mkutano huo nchi wanachama waliweza kuongelea
agenda kuu za nchi wananchama wa ukanda wa maziwa makuu ambazo ni Amani,
Utulivu na Usalama hususani katika eneo la mashariki mwa nchi ya
Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo.
Sanjari na hilo, nchi nyingi
zimeusifu uongozi wa Rais wa DRC, Felix Tshisekedi kuwa tangu alipoingia
madarakani amejitahidhi kuhakikisha kuwa kuna kuwa na amnai ndani ya
DRC pamoja na majirani zake. Pia Uganda, Rwanda pamoja na Angola
zimesifiwa kufanikisha kusaini makubalianao ya kuleta amanai kati ya
Uganda na Rwanda.
Akiongea awali wakati wa ufunguzi
wa Mkutano wa Mawaziri wa Mambo ya Nje Mgeni rasmi ambae alikuwa Waziri
Mkuu wa Jamhuri ya Kongo, Bwn. Clement Mouamba alisema kuwa mkutano wa
leo, umelenga kuisaidia nchi ya DRC katika changamoto inazopitia hasa
katika ukanda wa mashariki.
“Nawapongeza sana kwa kazi ambayo
mmekuwa mkiifanya kwa kushirikiana na wadau mbalimbali katika
kuhakikisha kuwa ugonjwa wa ebola unatokomezwa, kwani naamini kuwa umoja
wetu tunaweza,” alisema Mouamba.
Aliongeza kwa kuzitaka nchi
wanachama wa ukanda wa maziwa makuu kuendelea kulinda amanai na umoja
walionao ili kuweza kuendelea na shughuli mbalimbali za maendeleo kwani
bila amani ni vigumu sana kwa umoja huo kuendelea.
Kwa upande wake Waziri wa Mambo ya
Nje na Ushirikianao wa Jamhuri ya Kongo, ambae pia alikuwa mwenyekiti
wa mkutano huo Mhe. Jean Claude Gakosso aliwasisitiza mawaziri wa nchi
wanachama kuwa amani na umoja katika ukanda huo ni nguzo muhimu sana na
hivyo waendelee kuishika amani hiyo.
Pia aligusia ugonjwa wa ebola na
kuwataka nchi wanachama kutokata tama ya kupambana na ugonjwa huo licha
ya changamoto zinazojitokeza.
“Juhudi mbalimbali zilizochukuliwa
na Serikali ya DRC hadi sasa kwa kushirikiana na Shirika la Afya
Duniani (WHO) pamoja na wadau wengine katika kupambana na ugonjwa huo ni
kutoa chanjo ya kinga ya ugonjwa huo na elimu kwa wananchi wa maeneo
yaliyoathirika na ugionjwa huo” alisema Waziri Gakosso.
Mkutano wa leo ulitanguliwa na
mikutano miwili ambayo ilianza tarehe 11 hadi 14 Oktoba 2019, jijini
Brazzaville ambapo pamoja na mambo mengine ilijadiliwa suala la ugonjwa
wa ebola na hali ya amani katika maeneo yenye mlipuko wa ugonjwa huo.
Nchi wanachama wa ukanda wa maziwa
makuu ni pamoja na Angola, Burundi, Jamhuri ya Kati, Demokrasia ya
Kongo, Jamhuri ya Kongo, Kenya, Rwanda, Sudan, Sudani Kusini, Tanzania,
Uganda na Zambia.
Mwezi Augusti, 2019 Umoja wa
Maendeleo ya Nchi za Ukanda wa Kusini mwa Africa (SADC) ulifanyika
Tanzania Jijini Dar es Salaam nchi wananchama waliridhia na kuipitisha
kiswahili kuwa lugha rasmi ya nne ya Umoja huo baada ya Kiingereza,
Kireno na Kifaransa.
0 comments:
Post a Comment