
Waziri wa Nchi Ofisi ya
Rais, Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa, TAMISEMI, Selemani
Jafo,akizungumza na waandishi wa habari leo jijini Dodoma wakati akitoa
taarifa kuhusu hali ya uandikishaji katika daftari la orodha ya wapiga
kura mara baada ya kufikia hitimisho siku ya Jana Octoba 17


Mwandishi mwandamizi wa
gazeti la Nipashe Dodoma Augusta Njoji akipokea kombe kwa niaba ya
Halmashauri ya Mlele ambayo imefanya vizuri katika uandikishaji daftari
la orodha ya wapigakura kwa ajili ya uchaguzi wa serikali wa serikali za
mitaa ambayo imeandikisha kwa asilimia 152 kutoka kwa Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais, Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa, TAMISEMI, Selemani Jafo


Mwandishi mwandamizi wa Radio Uhuru FM Sakina Abdulmasoud akipokea Cheti kwa niaba ya Mkuu wa mkoa wa Tanga Mhe.Martine Shigela, ulioshika nafasi ya nne katika
uandikishaji daftari la orodha ya wapigakura kwa ajili ya uchaguzi wa
serikali wa serikali za mitaa ambapo umeandikisha asilimia 90 kutoka kwa Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais, Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa, TAMISEMI, Selemani Jafo

Waziri wa Nchi Ofisi ya
Rais, Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa, TAMISEMI, Selemani
Jafo,akimkabidhi tuzo Mpigapicha wa gazeti la Uhuru, Halima Kambi kwa
niaba ya Mkuu wa Mkoa wa Pwani Mhandisi Evarist Ndikilo ,ulioshika nafasi ya pili kwa uandikishaji wa dafatari la orodha ya wapiga kura kwa asilimia 96.

Waziri wa Nchi Ofisi ya
Rais, Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa, TAMISEMI, Selemani
Jafo,akimkabidhi Kombe Mwandishi wa Gazeti la Daily News Katale
Mbashiru kwa niaba ya Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam Mhe.Paul Makonda
ambao umekuwa kinara kwa uandikishaji wa wapiga kura kimkoa kwa kuwa na
asilimia 108.
...............
Na.Alex Sonna,Dodoma
Waziri wa Nchi Ofisi ya
Rais, Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa, TAMISEMI, Selemani Jafo
amewapongeza viongozi na wananchi wa Mkoa wa Dar es saalam kwa kuitikia
kikamilifu zoezi la uandikishaji katika orodha ya wapiga kura na
kuongoza kwa zoezi hilo katika orodha ya mkoa.
Waziri Jafo ameyasema
hayo leo Jijini Dodoma wakati akizungumza na waandishi wa habari kuhusu
hali ya uandikishaji katika daftari la orodha ya wapiga kura mara baada
ya kufikia hitimisho siku ya Jana Octoba 17.
Amesema Mkoa wa Dar es
saalam mwanzo ulianza kwa kusuasua lakini baada ya kuanza kupeana hamasa
wameweza kufanya vizuri, amesema viongozi wa kazi zote na wananchi kwa
ujumla hatimaye kufanikiwa kwa kuandikisha kwa asilimia 108.
“Niwapongeze Mkoa wa Dar
es saalam wakati natangaza kwa mara ya kwanza Mkoa ulikuwa na hali
mbaya lakini viongozi wa ngazi zote wamehamasishana halikadhalika
wananchi kwa kiwango kikubwa hadi kuongoza niwapongeze sana” amesema
Waziri Jafo.
Aidha amesema kwa mujibu
wa Ofisi ya Takwimu wananchi wenye sifa ya kupiga kura ni 26,960,485,
lakini walijiwekea lengo la kuandikisha wapiga kura milioni 22,916,412
ambao ni sawa na asilimia 85, ya wananchi wenye sifa ya kupiga kura
(wanaume 10,924,479) na wanawake 11,991,933.
Amesema baadhi ya maeneo
yalikumbwa na changamoto mbalimbali ikiwamo mvua na baadhi ya vituo
kuwa mbali na makazi ya watu, hivyo baada ya siku ya mwisho waliamua
kuongeza siku tatu kwa ajili ya kuhakikisha kila mtu anapata fulsa ya
kujiandikisha.
Ameongeza kuwa “hadi
kufikia Octoba 17 jumla ya wapiga kura 19,681,259 walikuwa
wamejiandikisha katika orodha ya daftari la wapiga kura kwa mwaka 2019,
Kati ya hao wanaume 9,529,992 na wanawake10,151,267, sawa na asilimia
86, ya lengo la wapiga kura 22,916,412, na huu ndio uandikishaji wenye
mafanikio zaidi ukilinganisha na mwaka 2014” amesema.
Licha ya kila Mkoa
kuvuka lengo lakuandikisha kwa asilimia 50, Mkoa mitano iliyoongoza ni
Dar es saalam 108%, Pwani 96%, Mwanza 95%, Tanga 90% na Singida 90% na
wote wamezawadiwa kikombe maalamu
.
Huku Mikoa mitano ya
mwisho licha ya kuvuka lengo lakini imeshika nafasi tano za mwisho, wa
mwisho kabisa ni Kigoma 65%, Njombe 75%, Simiyu na Shinyanga 76%, ambayo
jumla ya Mkoa yote ni 86%.
“Kwa upande wa
halmashauri zilizofanya vizuri ni Mlele 152%, Ngorongoro 129%, Kibiti
126%, Temeke 122% na Monduli 122% ,na halmashauri zenye wapigakura wengi
zaidi ya laki tisa 90,000 iliyoongoza ni Temeke MC 122%, Ilala MC111%,
Mwanza CC 105%, Ubungo MC 103% na Kinondoni MC 96%” amesema.
Aidha amewapongeza
wananchi wote waliojitokeza, na viongozi wa ngazi zote kuanzia mikoa na
vitongoji kwa kuhamasisha katika kujiandikisha kwenye daftari la orodha
ya wapiga kura la uchaguzi wa serikali za mitaa.
0 comments:
Post a Comment