METDO Tanzania

METDO Tanzania

Sunday, September 8, 2019

WAZIRI JAFO AIPONGEZA TAMISEMI (NETBALL) KWA KUFUZU KUSHIRIKI MASHINDANO LIGI YA MUUNGANO

Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa(TAMISEMI)Selemani jafo akizungumza na wachezaji wa timu ya mpira wa pete Tamisemi.
Sehemu ay wachezaji wa timu ya mpira wa Pete Tamisemi (Netball) wakimsikikliza Waziri wa nchi Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na serikali za Mitaa, Selemani Jafo,alipokutana nao le akiwapongeza kwa kufuzu kushiriki mashindano ya ligi ya Muungano
WAZIRI wa nchi Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na serikali za Mitaa, Selemani Jafo akiwa katika picha ya pamoja na Timu ya Mpira wa Pete Tamisemi (Netball) ambayo kufuzu kushiriki mashindano ya ligi ya Muungano yatakayo fanyika Zanzibar Novemba mwaka huu.
………………..
WAZIRI wa nchi Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na serikali za Mitaa, Selemani Jafo, ameipongeza timu ya mpira wa pete Tamisemi (Netball) kwa kufuzu kushiriki mashindano ya ligi ya Muungano yatakayo fanyika Zanzibar Novemba mwaka huu.
Jafo amezitoa pongezi hizo Jijini hapa wakati alipokuwa akizungumza na wachezaji pamoja na uongozi wa timu hiyo ambayo imeshika nafasi ya nne na kukataa tiketi ya kushiriki masindano ya ligi ya Muungano Zanzibar Novemba mwaka huu.
Amesema akiwa kama Waziri mwenye dhamana ya Tamisemi anajivunia timu hiyo kwa kufanya vizuri katika mashindano hayo pamoja na changamoto mbalimbali walizokuwa nazo.
“Niwapongeze sana kuwa sisi kama Tamisemi tunayotimu nzuri sana hivyo kinachohitajika ni maandalizi ya kutosha ili katika mashindano ya Muuungano Zanziba tuweze kufanya vizuri zaidi”amesema Jafo.
Ameutaka uongozi wa timu hiyo kuyafanyia kazi mapungufu waliyoyabaini katika mashindano hayo yaliyokwisha ili watakapo kwenda katika michuano ya muungano wasipate vikwazo.
“Kama ipo haja kusajili wachezaji wengine ili kuongeza nguvu fanyeni hivyo ili tunapokwenda Zanziba tuwe tofauti na tuliyokuwa hapa Dodoma”amesema Jafo.
Aidha katika kuwapatia motisha wachezi wa timu hiyo Jafo ameagiza itafutwe fedha kiasi kisichopungua Sh. 500,000 hadi 1,000,000 kwa kila mchezaji ili kuwaongezea morali ya mchezo.
Share:

0 comments:

Post a Comment

Copyright © WAZO HURU | Powered by Blogger Design by ronangelo | Blogger Theme by NewBloggerThemes.com