Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais,
Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa(TAMISEMI)Selemani jafo akizungumza
na wachezaji wa timu ya mpira wa pete Tamisemi.
Sehemu ay wachezaji wa timu ya
mpira wa Pete Tamisemi (Netball) wakimsikikliza Waziri wa nchi Ofisi ya
Rais Tawala za Mikoa na serikali za Mitaa, Selemani Jafo,alipokutana nao
le akiwapongeza kwa kufuzu kushiriki mashindano ya ligi ya Muungano
WAZIRI wa nchi Ofisi ya Rais
Tawala za Mikoa na serikali za Mitaa, Selemani Jafo akiwa katika picha
ya pamoja na Timu ya Mpira wa Pete Tamisemi (Netball) ambayo kufuzu
kushiriki mashindano ya ligi ya Muungano yatakayo fanyika Zanzibar
Novemba mwaka huu.
………………..
WAZIRI wa nchi Ofisi ya Rais
Tawala za Mikoa na serikali za Mitaa, Selemani Jafo, ameipongeza timu ya
mpira wa pete Tamisemi (Netball) kwa kufuzu kushiriki mashindano ya
ligi ya Muungano yatakayo fanyika Zanzibar Novemba mwaka huu.
Jafo amezitoa pongezi hizo Jijini
hapa wakati alipokuwa akizungumza na wachezaji pamoja na uongozi wa timu
hiyo ambayo imeshika nafasi ya nne na kukataa tiketi ya kushiriki
masindano ya ligi ya Muungano Zanzibar Novemba mwaka huu.
Amesema akiwa kama Waziri mwenye
dhamana ya Tamisemi anajivunia timu hiyo kwa kufanya vizuri katika
mashindano hayo pamoja na changamoto mbalimbali walizokuwa nazo.
“Niwapongeze sana kuwa sisi kama
Tamisemi tunayotimu nzuri sana hivyo kinachohitajika ni maandalizi ya
kutosha ili katika mashindano ya Muuungano Zanziba tuweze kufanya vizuri
zaidi”amesema Jafo.
Ameutaka uongozi wa timu hiyo
kuyafanyia kazi mapungufu waliyoyabaini katika mashindano hayo
yaliyokwisha ili watakapo kwenda katika michuano ya muungano wasipate
vikwazo.
“Kama ipo haja kusajili wachezaji
wengine ili kuongeza nguvu fanyeni hivyo ili tunapokwenda Zanziba tuwe
tofauti na tuliyokuwa hapa Dodoma”amesema Jafo.
Aidha katika kuwapatia motisha
wachezi wa timu hiyo Jafo ameagiza itafutwe fedha kiasi kisichopungua
Sh. 500,000 hadi 1,000,000 kwa kila mchezaji ili kuwaongezea morali ya
mchezo.
No comments:
Post a Comment