Shujaa wa timu ya Taifa ya
Tanzania golikipa Juma Kaseja akibebwa juu juu na wachezaji wenzake mara
baada ya kumalizika kwa mchezo katika ya timu ya Taifa ya Burundi na
Timu ya Taifa ya Tanzania Taifa Stars kwenye uwanja wa Taifa ambapo
Taifa Stars imepata ushindi wa penalti 3-0 dhidi ya Burundi mchezo wa
kufuzu Kombe la Dunia mwaka 2022 nchini Qatar.
Golikipa Juma Kaseja akionesha
umwamba wake wa kupangua penati mbele ya mashabiki wa timu ya taifa huku
akiwa amebebwa kwenye uwanja wa Taifa leo.
Kapteni wa timu ya taifa ya
Tanzania na mchezaji wa timu ya Genk ya Ubelgiji akiongoza wachezaji
wenzake kuingia uwanjani kabla ya kuchezo mchezo wao wa leo kufuzu
fainali za kombe la Dunia 2022 nchini Qatar leo kwenye uwanja wa Taifa.
Mshabuliaji wa timu ya Taifa na
Kapteni wa timu hiyo Mbwana Samatta akiwachachafywa mabeki wa timu ya
Taifa ya Burundi katika mchezo huo uliofanyika kwenye uwanja wa Taifa
leo.
Mshabuliaji wa timu ya Taifa ya Tanzania na mchezaji wa timu ya El Jadid ya Morocco akiwania mpira na mabeki wa timu ya Burundi.
Mashabiki wakiwa wamefurika kwenye uwanja wa Taifa.
Wachezaji wa akiba wa timu ya Taifa ya Tanzania wakipasha.
Mwanamuziki Harmonize na Mkewe
Sara walikuwa ni miongozi mwa mashabiki waliojitokeza kushuhudia mchezo
wa kimataifa kati ya Taifa Stars na timu ya Taifa ya Burundi leo kwenye
uwanja wa Taifa.
*************************
Tanzania imefuzu hatua ya makundi
leo kwa ushindi wa penalti 3-0 dhidi ya Burundi mchezo wa kufuzu Kombe
la Dunia mwaka 2022 nchini Qatar.
Baada ya dakika 90 zilikamilika kwa timu zote kufungana bao 1-1 kisha zikaongezwa 30 nazo ngoma ikawa mbichi ya bila kufungana.
Timu zote zilianza kucheza kwa
tahadhari na kushambuliana kwa zamu mpaka dakika 120 zinakamilika ngoma
ilikuwa ni 1-1 jambo lililopelekea mshindi kupatikana kwa njia ya
mikwaju ya penalti.
Tanzania ilikuwa ya kwanza
kuandika bao lililofungwa na Mbwana Samatta dakika ya 29 na Burundi
walisawazisha dakika ya 45 bao likiwekwa kambani na Mshambuliaji Abdul
Fieston.
Kwa upande wa Tanzania wachezaji Erasto Nyoni, Himid Mao na Gadiel Mbaga waliweza kufunga huku Burundi wakikosa penalty zote.
Hii ilikuwa mechi ya marudiano baada ya kwanza kuchezwa nchini Burundi na timu zote mbili zikifungana 1_1.
Kwa Matokeo hayo Burundi
wametolewa huku Tanzania ikiingia katika hatua ya Makundi ya timu nne
zitakazowania nafasi ya kufuzu Kombe la Dunia 2022 nchini Qatar.
0 comments:
Post a Comment