MKUU wa Wilaya ya Ikungi, Mhe
Edward Mpogolo amefanya ziara yake ya kwanza ndani ya Wilaya hiyo toka
ateuliwa na Rais John Magufuli akichukua nafasi ya Miraji Mtaturu ambaye
kwa sasa ni Mbunge wa Jimbo la Singida Mashariki.
DC Mpogolo amefanya ziara katika Kata nne za Iyumbu, Mgungira, Ighombwe na Mtunduru ambapo alitembelea miradi ya Maendeleo, kusikiliza na kutatua changamoto za wananchi pamoja na kueleza mambo makubwa ambayo yamefanywa na Rais Magufuli tangu achaguliwe mwaka 2015.
DC Mpogolo amefanya ziara katika Kata nne za Iyumbu, Mgungira, Ighombwe na Mtunduru ambapo alitembelea miradi ya Maendeleo, kusikiliza na kutatua changamoto za wananchi pamoja na kueleza mambo makubwa ambayo yamefanywa na Rais Magufuli tangu achaguliwe mwaka 2015.
Kero ambazo alikutana nazo na
kuzitolea ufafanuzi ni changamoto ya maji, miundombinu ya barabara,
uhaba wa vyumba vya madarasa, vituo vya afya, umeme na mawasiliano
ambapo DC Mpogolo aliwaeleza wananchi hao hatua ambazo Serikali
imezichukua katika kuzitatua.
” Ndugu zangu Serikali ya awamu ya
tano chini ya Rais Dk Magufuli kwa kutambua mnakabiliwa na changamoto
kwenye sekta ya afya tayari ameshatoa kiasi cha Shilingi Milioni 500
ambazo zitajenga kituo cha afya cha Iyumbu kitakachokua na uwezo wa
kuhudumia kata zaidi ya tatu.
” Suala la Maji katika kata ya
Mtunduru linaenda kuwa historia kwa maana ndani ya miezi miwili kutoka
sasa kisima cha maji kitakamilika na kimegharimu zaidi ya Milioni 438,
lakini kata ya Ighombe mkandarasi yupo site na ameshafikia kina cha maji
kilichobaki ni kutengeneza Tanki LA kuhifadhia maji,” amesema DC
Mpogolo.
Kuhusu elimu amewasifu wananchi wa
kata zote nne alizotembelea kwa namna ambavyo wamekua wakijitoa
kuchangia miradi ya maendeleo hasa katika ujenzi wa vyumba vya madarasa
ambapo amewaagiza wahandisi wa Wilaya kuhakikisha wanatoa ushauri katika
miradi inayojengwa na wananchi ili kuifanya iwe bora zaidi.
Amewatoa hofu wananchi hao kuhusu
changamoto ya umeme na kueleza kuwa Kata zote nne zipo katika mpango ww
mradi wa umeme wa REA na kwamba ndani ya kipindi kifupi umeme utakua
umewafikia.
” Ndugu zangu wana Ikungi suala la
umeme katika kata hizi nne umekua ni changamoto. Nimelala hapa
nimejionea. Niwahakikishie nimelichukua na kwa kushirikiana na wabunge
wenu tutapambana kuuleta umeme ili kuongeza uzalishaji wa huduma za
kijamii na kimaendeleo.
Nafahamu pia mna tatizo la
mawasiliano, na mimi nimejionea kwa sababu nimefika hapa. Tayari
Serikali ishatuma wataalamu wa minara na ninaamini hadi kufikia mwishoni
mwa mwaka tutakua tumepata mawasiliano ambayo yataongeza ukuaji wa
uchumi kwenye hizi kata zetu,” amesema DC Mpogolo.
Katika ziara hiyo DC Mpogolo
aliambatana na watalaamu mbalimbali kutoka Halmashauri ya Wilaya ya
Ikungi ambapo pia aliweka kambi kwa kulala kwenye kila kata ambayo
alifanya ziara lengo likiwa kujitambulisha na kusikiliza kero za
wananchi wake.
0 comments:
Post a Comment