
WAZIRI MKUU Kassim Majaliwa amezielekeza
mamlaka husika ziwachukulie hatua za kinidhamu watu wote ambao
hawakutekeleza majukumu yao ipasavyo kufuatia tukio la ajali ya moto
iliyotokea Agosti 11, 2019 mkoani Morogoro na kusababisha vifo vya watu
104, majeruhi pamoja na uharibifu wa mali.
Waziri Mkuu ametoa kauli hiyo leo
(Ijumaa, Septemba 13, 2019) , wakati akiahirisha mkutano wa 16 wa Bunge
la 11, Bungeni jijini Dodoma. Bunge limeahirishwa hadi tarehe 3, Novemba
mwaka huu.
“Baada ya tukio hilo la kusikitisha
tarehe 12 Agosti 2019niliunda Kamati Maalumu kwa lengo la kufanya
uchunguzi wa kina kuhusu ajali hiyo iliyosababisha vifo, majeruhi na
uharibifu wa mali.”
“Lengo lilikuwa kufahamu chanzo cha
ajali, mazingira baada ya ajali na hatua gani zichukuliwe kuzuia matukio
kama haya sambamba na kuwawajibisha wale wote ambao hawakutekeleza
wajibu wao ipasavyo kabla na baada ya ajali kutokea.”
Waziri Mkuu ametumia fursa hiyo
kuwashukurumadaktari na wahudumu wa Hospitali ya Rufaa ya Morogoro na
Hospitali ya Taifa ya Muhimbili nawadau wote ambao walishiriki kuokoa
maisha ya waathirika wa ajali hiyo tangu ilipotokea.
“Nawasihi Watanzania wenzangu
tujifunze kutokana na ajali hiyo iliyotokea Morogoro na hivyo
kuepuka mikusanyiko ya aina hiyo katika maeneo ya ajali. Aidha, tujenge
nyoyo za huruma na kuwa wepesi wa kutoa msaada kwa waathirika wa ajali
badala ya kutumia kama fursa za kujinufaisha isivyo halali.”
0 comments:
Post a Comment