Waziri wa Ujenzi , Uchukuzi na Mawasiliano, Mhandisi Isack
Kamwelwe(kushoto) akipata maelezo kutoka
kwa Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Bandari Tanzaznia (TPA), Mhandisi Deusdedit
Kakoko (kulia) kuhusu kutua kwa Meli
kubwa ya mizigo ya MV Grand Duke kwenye gati jipya namba 0 katika Bandari ya
Dar es Salaam
Gari likitoka kwenye meli kubwa ya mizigo ya
magari MV Grand Duke baada ya kutua hapo jana kwenye gati jipya namba 0 ya
Bandari ya Dar es Salaam.
Na Paschal Dotto-MAELEZO
Waziri
wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano, Mhandisi Isack Kamwelwe amezikaribisha Nchi
Wanachama wa Jumuiya ya Maendeleo ya Nchi za Kusini Mwa Afrika (SADC) kutumia
bandari ya Dar es Salaam mara baada ya ukarabati wake hasa gati nambo sufuri
kuanza kupokea mizigo.
Akizungmza
Jijini Dar es Salaam alipotembelea kuona meli kubwa ya Mizigo ya Magari ya
kampuni ya Meli ya Mv Grand Duke
iliyotua bandarini hapo jana, Waziri Kamwelwe alifurahishwa kuona meli hiyo
kubwa nyenye urefu wa mita 200 na uwezo wa kubeba magari 6,000 ambapo imetua ikiwa na magari 1,347 imedhihirisha
uwezo wa bandari hiyo kwamba iko tayari
kupokea mizigo mikubwa.
“Tuko
hapa kuwahabarisha Watanzania, na Nchi Wanachama wa Jumuiya ya Maendeleo Kusini
Mwa Afrika (SADC), kwamba ukarabati wa Bandari ya Dar es Salaam unaenda vizuri
ikiwa ni pamoja na kukamilika kwa gati namba moja, mbili na hili gati namba
sifuri liko mwishoni na limeanza kupokea meli kubwa za Mizigo kama mnavyoona
hapo, hiyo ni meli ya mizigo ya magari yenye uwezo mkubwa sana”, Waziri
Kamwelwe.
Malengo
ya Serikali ni kufanya ukarabati wamagati nane ambapo mpaka sasa gati namba
moja na gati namba mbili yako kwenye
matumizi mara baada ya kukamilika na sasa meli zinaendelea kutoa huduma kama
kawaida, gati namba sifuri ambalo ni maalum kwa meli za mizigo ya magari
linaendelea na ukarabati lakini asilimia kubwa liko vizuri.
Waziri
Kamwelwe alisema kuwa mara baada ya gati hilo kukamilika Tanzania itakuwa na
uwezo mkubwa wa kupokea mizigo ya magari laki 6 kwa mwaka, lakini pia bandari hiyo inabeba tani milioni
17 kwa mwaka huku malengo ya Serikali ikiwa ni
kufikia tani milioni 25 ifikapo mwaka 2021.
“Malengo
yetu ni kufikia tani milioni 25 kwa mwaka tofauti na tani za sasa milioni 17,
kwa hiyo Nchi Wanachama wa SADC, bandari hii sasa inafanya kazi vizuri, kwa
hiyo majirani zetu kutoka SADC, DRC, Malawi, Zambia na nchi zingine za ukanda
huu wa Kusini mwa Afrika wanakaribishwa
sana kutumia bandari ya Dar es Salaam” Alisisitiza Waziri Kamwelwe.
Waziri
Kamwelwe alisema Serikali itaendelea kufanya kazi kwa kushirikiana na
wafanyabiashara kutoka Nchi Wananchama wa SADC ili maeneo ambayo yana changamoto ziweze kutatuliwa haraka.
“Serikali
imewekeza fedha nyingi katika ukarabati huo, kwa hiyo itahakikisha kuwa inaipa
bandari hii mizigo ya kutosha na hasa kutoka kwa Nchi Wanachama wa SADC, ili
kuwawezesha kupata huduma rahisi za usafirishaji” alisema Kamwelwe
kwa
upande wake Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Bandari, Mhandisi Deusdedit Kakoko,
alisema kuwa gati jipya namba sufuri
limeanza kufanya kazi kwa kupokea meli kubwa ya Mv Grand Duke ambayo imetua
jana na mzigo wa magari 1347.
“Hili gati ni Jipya ni kati ya magati nane ambayo yanajengwa, lenyewe limejengwa
kwa zege kama mnavyoona, lina uwezo wa kubeba
magari 10,000 kwa wakati mmoja kutoka uwezo wa kubeba magari 2,500 ambao
tulikuwa nao hapo mwanzo, lakini pia lina urefu wa mita 320 kwa hiyo ni gati
kubwa na hii meli ina urafu wa mita 200 kwa hiyo kuna mita 120 zimebakia kwenye
gati hili”, Alisema Mhandisi Kakoko.
Gati
hilo ambalo ni la kisasa Zaidi litakuwa na taa ambazo zitawezesha kufanyika
kazi usiku na mchana hapo bandarini, na
makabidhiano ya gati hilo yatafanyika kesho ambapo Mkandarasi ataikabidhi
Mamlaka ya Bandari (TPA).
Aidha, Mhandisi Kakoko alisema kuwa meli ya Abiria
ziwa nyasa imeingia kwenye majaribio ya mwezi mmoja ambapo mwezi ujao
inatarajiwa kukabidhiwa kwa Mamlaka hiyo
ili kuanza kuhudumia wananchi wa maeneo hayo.
MWISHO
0 comments:
Post a Comment