…………………….
Nteghenjwa Hosseah, Dongobesh
Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais
Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Mhe. Selemani Jafo amewaagiza
viongozi wa Halmashauri ya Wilaya ya Mbulu kuanza kupanga Mji wa
Dongobeshi kwa kuwa makao makuu ya Wilaya hiyo yanahamia hapo ndani ya
kipindi cha muda mfupi.
Waziri Jafo ameyasema hayo wakati alipokuwa kwenye ziara ya
kikazi katika Mkoa wa Manyara na kutembelea ujenzi wa Jengo la
Halmashauri ya Wilaya ya Wilaya ya Mbulu linalojengwa katika eneo la
Dongobeshi.
“Hapa pameshakua mjini sasa
maana Jengo la Halmashauri la Gorofa kama hili linaendelea kujengwa na
wote watumishi wote mtahamia hapa, bado kuna kituo cha Afya ambacho
kimeshakamilika na kuanza kutoa huduma na Serikali inaendelea na Ujenzi
wa Hospital ya Wilaya katika eneo hili miradi hii yote kwa kiasi kikubwa
itachangia ukuaji na uhamiaji wa watu hivyo ni vyema mkajipanga kuona
namna bora ya kupanga mji wenu” Alisema Jafo
Aliongeza kuwa Mnatakiwa muanze kufikiria maeneo yatakayofaa kwa
ajili ya upimaji wa viwanja hapa hapatakiwa kuanza kukua kiholela
pimeni viwanja watu wakae kwenye maeneo yaliyopangika na mji uweze
kukua vizuri.
Wakati huo huo Waziri Jafo
ameupongeza Uongozi wa Halmashauri ya Wilaya ya Mbulu kwa usimamizi
makini wa ujenzi wa Jengo la Halmashauri linaloendelea kujengwa katika
eneo la Dongobesh.
“Tumewaletea fedha kwa ajili ya ujenzi wa jengo la Utawala
lakini kukawa na mivutano ya wapi pangefaa kuwa Makao Makuu ya Wilayah
ii ambapo ndipo Jengo hili lilitakiwa kujengwa: Ninachofurahi kuona leo
ni kuwa mlipokea maelekezo na jengo limejengwa katika eneo la Dongobesh
ambapo ni katikati ya Wilayah ii na rahisi kwa wananchi kufika kutoka
kila pande za Wilaya hii”Alisema Jafo.
Kwa kujenga jengo hili
Dongobesh mmewatendea haki Wananchi wa Mbulu kwa kuwa mmewapunguzia
gharama ya muda na umbali ambao kwa muda mrefu imewagharimu kufuata
huduma za Muhimu katika Ofisi za Serikali aliongeza Jafo.
“Nimeridhishwa na ujenzi
unaoendelea na nimefurahi kuona mmeshakamilisha majengo ya chini,
nimeridhishwa na ubora wa Jengo pamoja na gharama nafuu toka kwa
Mkandarasi Mzinga holding Company pamoja na Mhandisi Mshauri Dar es
salaam Institute of Technology (DIT) niseme kazi nzuri na hongerni sana ”
alimalizia Jafo.
Akiwasilisha ripoti ya ujenzi wa Jengo la Halmashauri Mkurugenzi
Mtendaji wa Halmashauri hiyo Hudson Kamoga amesema ujenzi wa jengo la
Utawala unafanyika kwa awamu tatu na katika awamu ya kwanza inahusisha
ujenzi wa jengo la mbele ambalo litagharimu tsh Bil 4.7 awamu ya pili
itahusisha ujenzi wa ukumbi, ghala na mgahawa na awamu ya tatu
utahusisha ujenzi wa pande mbili za nyuma ya jengo.
Kamoga aliongeza kuwa Jengo hilo la Utawala limekadiriwa
kujengwa kwa gharama ya Tsh 6.7 ambapo gharama za ujenzi ni Bil 6.3 na
gharama sa mhandisi mshauri ni mil 351 huku gharama sa kuandaa mchoro
zikigharimu tsh mil 30 tu.
Ujenzi wa Jengo la Halmashauri ya Mbulu umetokana na kugawanyika
kwa Halmashauri ya Wilaya ya Mbulu na kupatikana kwa Halmashauri ya
Mji wa Mbulu pamoja na Halmashauri ya Wilaya ya Mbulu na kupelekea Mbulu
Mji kubakia Mjini na Halmashauri ya Wilaya kuhamia katika eneo la
Dongobesh ambapo ujenzi huo unaendelea.
0 comments:
Post a Comment