METDO Tanzania

METDO Tanzania

Thursday, November 25, 2021

CHIFU NDOVU SENGE ASIMIKWA KUWA CHIFU MKUU SINGIDA

 Na Hamis Hussein -SINGIDA


Umoja wa machifu mkoa wa singida umewaomba wanaumoja huo kufanya zoezi la kuwasimika machifu wengine katika maeneo yao kabla ya kwenda kushiriki mkutano mkuu wa machifu Tanzania  utakaofanyika mkoani Kilimanjaro katika kujiandaa kukutana na mkuu wa machifu Tanzania  chifu hangaya  ambaye ni rais wa awamu ya sita mh. Samia suluhu hasani.

Akizungumza wakati wa kumsimika mkuu wa machifu mkoa wa singida chifu  Mugenyi Senge Mugenyi Ndovu , mwenyekiti wa umoja wa machifu mkoa wa singida   Chifu  Mjengi Gwau amewataka  kushirikiana ili kutimiza malengo huku akitoa rai ya kuundwa kwa mabaraza ya wazee watakaosimamia mila na desturi za kitemi
" Na wengine wote tusaidiane wafanye haya , tunangojwa kwenda kufanya mkutano umoja wa machifu tannzania  moshi marangu ili tuchague viongozi wa umoja wa machifu , tushamaliza chifu Hangaya anatuita machifu wote dodoma ..... halafu tutaunda mabaraza ya wazee yatakayosimamia  mila na destiri zetu" amesema Chifu Mjengi .
Baada ya kusimikwaa kuwa mkuu wa machifu mkoa wa singida chifu mugenyi senge mugenye ndovu ameshukuru kupata nafasi hiyo na kueleza kuwa atakuwa ni kiunganishi kati ya serikali na jamii katika kufanikisha mambo mbalimbali ya kimaendeleo
"Mimi nimefurahi sana kwa kutawadhwa kuwa chifu , kuna miradi mingi sana ambayo serikali imekuwa ikitoa  lakini wananchi stahiki wanazotakiwa  kupata walikuwa hawapati kwa sababu hakukuwa na mtu wa kuwatetea ....... imekuwa ni nafasi nzuri ya mimi kuwatetea kwasababu nawajua raia  .... mimi nitakuwa kiunganishi kati ya serikali na jamiii." amesema chifu Mghenyi Senge Ndovu.

Kuhusu migogoro ya ardhi chifu huyo ameeleza namna ambavyo umilikishaji usiohalali unavyopelekea migogoro na kuiomba serikali kushirikiana
 katika kuitatua huku akitoa shukurani kwa  mkuu wa machifu Tanzania  chifu hangaya  rais wa jamhuri ya muungano wa Tanzania  samia suluhu Hassan
" Kuna baadhi ya watu ambao wametoka katika mikoa mingine wametumia njia za ujanja ujanja kumiliki  maeneo makubwa ya ardhi .... sisi tutasimama kuhakikisha wananchi wanapata haki zao.kwanza nimpongeze chifu hanya , wakatai anasimikwa kuwa mkuu wa machifu tanzania nilikuwa miongoni mwa machifu niliokuepo kwenye tukio  hilo  na hii  inaonesha utamaduni na mila zetu zinaheshimika . ameongeza chifu Mghenyi Senge Ndovu.

Katibu wa chifu ndovu amabaye pia ni mtoto wake salum mghenyi ndovu amesema mkuu huyo wa machifu atasimamia maeneo ya asili kama vile misitu na vyanzo vya maji
" kuna mambo mengi sana ambayo chifu atayasimamia zamani tulikuwa na maeneo yetu ya asili kama vile msitu , vyanzo vya maji ambayo kwa sasa havizingatiwi sana  kuna maagizo alitoa katibu wa wizara ya sanaa utamaduni dkt. hassani abasi kuwa machifu waorodheshe maeneo yao yalikuwa yakiutawala wa kichifu... hivyo kuna maeneo hapa singida yanahitaji usimamizi wa chifu na ndio kazi ambayo ataifanya .  amesema salum mghenyi  Ndovu katibu wa chifu Mghenyi senge Ndovu.

Mkoa wa singida una jumla ya machifu sita ambao huongoza shughuli mbalibali za kitemi kama mila na desturi ya jamii yao.



Share:

0 comments:

Post a Comment

Copyright © WAZO HURU | Powered by Blogger Design by ronangelo | Blogger Theme by NewBloggerThemes.com