METDO Tanzania

METDO Tanzania

Tuesday, September 25, 2018

"SEHEMU PEKEE YA VIJANA KUIMARISHA KIPATO NI KUPITIA SEKTA YA KILIMO" DKT TIZEBA

Dkt Charles Tizeba Waziri wa kilimo akisisitiza jambo wakati akizungumza na vijana wa Umoja wa Vijana wa Chama Cha Mapinduzi (UVCCM) Mkoa wa Tanga ambao wapo katika kambi maalumu ya kujitolea kwa ajili ya ujenzi wa Hospitali ya Wilaya ya Muheza leo tarehe 25 Septemba 2018. (Picha Zote Na Mathias Canal-WK)
Dkt Charles Tizeba Waziri wa kilimo pamoja na Mkuu wa Mkoa wa Tanga Mhe Martin Shigela wakikagua ujenzi wa hospitali ya Wilaya ya Muheza wakati walipotembelea kambi maalumu ya vijana wa Umoja wa Vijana wa Chama Cha Mapinduzi (UVCCM) Mkoa wa Tanga walioamua kufanya ujenzi kwa kujitolea, wakati akiwa safarini kuelekea Wilayani Korogwe leo tarehe 25 Septemba 2018.

Waziri wa kilimo Mhe Mhandisi Dkt Charles Tizeba akisisitiza jambo wakati akizungumza na vijana wa Umoja wa Vijana wa Chama Cha Mapinduzi (UVCCM) Mkoa wa Tanga ambao wapo katika kambi maalumu wakijitolea katika ujenzi wa Hospitali ya Wilaya ya Muheza leo tarehe 25 Septemba 2018.

Na Mathias Canal-WK, Muheza-Tanga

Imeelezwa kuwa sehemu pekee ya kuimarisha kilimo cha mwananchi mmoja mmoja, wananchi katika makundi ya kijamii hususani vijana ni kupitia sekta ya kilimo kwani ndio sehemu pekee ya ukombozi wa mkulima katika jamii.

Imeelezwa kuwa kuna uwezekano wa kufanya biashara mbalimbali nchini ambazo zinaweza kuongeza kipato lakini sahemu sahihi isiyokuwa na jazba na dhoruba katika utendaji ni kufanya kilimo biashara ambacho kamwe hakiwezi kumtupa mkulima.

Dkt Charles Tizeba Waziri wa kilimo, ameyasema hayo leo tarehe 25 Septemba 2018 wakati akizungumza na vijana wa Umoja wa Vijana wa Chama Cha Mapinduzi (UVCCM) Mkoa wa Tanga ambao wapo katika kambi maalumu ya ujenzi wa Hospitali ya Wilaya ya Muheza.

Vijana hao ambao wameamua kutumia nguvu zao pasina malipo wameamua kwa umoja wao kuunga mkono juhudi za Mwenyekiti wa Chama Cha Mapinduzi Taifa na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe Dkt John Pombe Magufuli kwa kauli yake inayohamasisha chachu na juhudi za kiutendaji kwa wananchi ya "Hapa Kazi Tu".

Aidha, katika kuhamasisha juhudi za kiutendaji Waziri huyo mwenye dhamana ya kilimo ameunga mkono juhudi za vijana hao kwa kuchangia fedha ya chakula shilingi 1,100,000 sambamba na kushiriki ujenzi wa jengo maalumu la upasuaji.

Waziri wa kilimo Mhe Dkt Charles Tizeba alitembelea ujenzi huo wa Hospitali ya Wilaya ya Muheza akiwa safarini kutembelea mashamba ya mkonge ikiwa ni siku ya pili ya ziara ya kikazi Mkoani Tanga aliyoianza jana tarehe 25 Septemba 2018 ya kukutana na makundi mbalimbali ya wakulima wa zao la Mkonge ili kutafuta ufumbuzi wa changamoto zinazowakabili wakulima wa zao hilo.

MWISHO.
Share:

0 comments:

Post a Comment

Copyright © WAZO HURU | Powered by Blogger Design by ronangelo | Blogger Theme by NewBloggerThemes.com