Waziri wa kilimo Mhe Mhandisi Dkt Charles Tizeba akizungumza na Umoja wa wabanguaji wadogo wa korosho Tanzania (UWWKT) katika mkutano uliofanyika kwenye ukumbi wa mikutano kwenye uwanja wa kimataifa wa michezo (National Stadium) Jijini Dar es salaam juu ya kujadili mwenendo wa ubanguaji wa korosho leo tarehe 27 Septemba 2018. (Picha Zote Na Mathias Canal, WK)
Muwakilishi wa Chama cha wabanguaji wakubwa wa korosho ( Cashewnuts Prossors Association) Ndg Peter Christopher akisoma taarifa ya chama hicho mbele ya waziri wa kilimo Mhe Mhandisi Dkt Charles Tizeba katika mkutano uliofanyika kwenye ukumbi wa mikutano kwenye uwanja wa kimataifa wa michezo (National Stadium) Jijini Dar es salaam juu ya kujadili mwenendo wa ubanguaji wa korosho leo tarehe 27 Septemba 2018.
Waziri wa kilimo Mhe Mhandisi Dkt Charles Tizeba akisisitiza jambo wakati akizungumza na Umoja wa wabanguaji wadogo wa korosho Tanzania (UWWKT) katika mkutano uliofanyika kwenye ukumbi wa mikutano kwenye uwanja wa kimataifa wa michezo (National Stadium) Jijini Dar es salaam juu ya kujadili mwenendo wa ubanguaji wa korosho leo tarehe 27 Septemba 2018. Mwingine pichani ni Kaimu Mkurugenzi wa Bodi ya Korosho Tanzania Prof Wakuru Magigi.
Mwenyekiti wa Umoja wa wabanguaji wadogo wa korosho (UWWKT) Bi Tumpale Salum Magehema akisoma taarifa ya umoja huo mbele ya waziri wa kilimo Mhe Mhandisi Dkt Charles Tizeba katika mkutano uliofanyika kwenye ukumbi wa mikutano kwenye uwanja wa kimataifa wa michezo (National Stadium) Jijini Dar es salaam juu ya kujadili mwenendo wa ubanguaji wa korosho leo tarehe 27 Septemba 2018.
Na
Mathias Canal-WK, Dar es salaam
Korosho ni moja ya mazao makuu ya biashara
nchini. Kwa sasa zao la korosho linalimwa zaidi mikoa ya Kusini mwa Tanzania,
yaani Lindi na Mtwara ikifuatiwa na Mkoa wa Ruvuma, Pwani na Tanga ambapo kwa
kiasi Fulani mkoani Singida wakulima pia wameamka kimkakati kwa kuanza kujikita
katika kilimo hicho.
Kuelekea uchumi wa viwanda nchini, serikali imesema kuwa itafanya
mazungumzo ya haraka na Benki ya Maendeleo ya Kilimo Tanzania (TADB) ili
kuboresha zaidi huduma sambamba na kufikia wakulima wengi kwa kuwapa mikopo ili
kuinua sekta ya kilimo ambayo ndiyo mtoaji wa malighafi zinazotumiwa na viwanda
hivyo.
Pamoja na zao hilo kuwa sehemu
ya mhimili mkubwa wa uchumi wa wakulima na Taifa kwa ujumla, bado wabanguaji wadogo
wa korosho nchini wamekuwa wakikabiliwa na ukosefu wa elimu ya ubanguaji wenye
tija ikiwa ni pamoja na ukosefu wa mitaji jambo linalopelekea wabanguaji hao
kukosa sifa ya kukopesheka.
Waziri wa kilimo Mhe Mhandisi
Dkt Charles Tizeba leo tarehe 27 Septemba 2018 ametangaza neema kwa wabanguaji
wadogo wa korosho kwa kuitaka benki ya maendeleo ya kilimo Tanzania (TADB)
kuwawezesha wabanguaji hao mikopo yenye masharti nafuu ili kuwa na mitaji itakayopelekea
kuongeza tija katika ubanguaji wa korosho nchini.
Waziri Tizeba ameyasema hayo
wakati akijibu maoni na mapendekezo yaliyosomwa kwenye taarifa ya Umoja wa
wabanguaji wadogo wa korosho Tanzania (UWWKT) katika mkutano uliofanyika katika
ukumbi wa mikutano katika uwanja wa kimataifa wa michezo (National Stadium) Jijini
Dar es salaam.
Ili kuongeza ufanisi na tija katika
ubanguaji chama hicho kimeishauri serikali kutoa elimu ya ubanguaji ili kupata
bidhaa bora yenye kukidhi viwango vya soko la Kimataifa na kuwezesha
upatikanaji wa mikopo yenye riba nafuu kwani kufanya hivyo wabanguaji hao
wadogo wataweza kuongeza uzalishaji kutoka Tani 64 kwa mwaka hadi kufikia Tani 192
kwa mwaka.
Dkt Tizeba aliagiza kutazamwa
upya mfumo wa stakabadhi ghalani ili kurahisisha ununuzi wa korosho kwani kwa
sasa unamtaka mnunuzi kununua kuanzia tani 50 jambo linalofanya wabanguaji
wadogo kushindwa kuingia katika soko hilo.
Alisema kuwa Sekta ya kilimo nchini ni kitovu cha maendeleo ya
viwanda kwa kutoa masoko na malighafi za viwandani ambapo inaajiri Watanzania
wengi takribani zaidi ya asilimia 67.
Katika utekelezaji wa Mpango wa Pili wa Maendeleo, Serikali
inaendelea kuimarisha mafanikio yaliyofikiwa katika sekta ya kilimo ikiwemo
kuimarisha masoko ya kilimo ili sekta hiyo iendelee kuwa na tija kwa wakulima nchini
na taifa kwa ujumla.
Alisema ili kuongeza ufanisi na tija Serikali katika mwaka wa
fedha 2017/2018 imefuta ada na tozo zipatazo 80 kati ya tozo na ada 139
zilizokuwa zinatozwa katika mazao ya kilimo nchini ambazo zilibainika kutokuwa
na tija kwa wakulima.
Katika kurahisisha utendaji kwenye zao la korosho Serikali
imefuta tozo tano kati ya tisa alizokuwa anakatwa mkulima wa zao la Korosho
baada ya kubainika kwamba hazikuwa sahihi.
MWISHO.
0 comments:
Post a Comment