Na
Emmanuel Michael Senny
Uwekezaji mkubwa wa vifaa tiba
na miundo mbinu katika huduma za kibingwa kwenye Hospitali ya Benjamin Mkapa
(BMH), umeifanya serikali ya Rais Dk.John Magufuli kuacha alama isiyofutika kwa
miongoni kadhaa ijayo.
Moja ya mambo yanayovuta hisia
na hamasa ya wagonjwa kujitokeza kufanyiwa uchunguzi wa magonjwa mbalimbali
yanayohusu huduma ya mama na mtoto ni uwepo wa vifaa tiba vya kisasa,
vitendanishi na watalaam wabobezi katika idara mbalimbali ikiwamo huduma ya
mama na mtoto.
Jana, Afisa Uhusiano na Mawasiliano
wa Hospitali ya Benjamin Mkapa, Karim Meshack aliieleza timu ya wanahabari
waliofanya ziara ya mafunzo hospitalini hapo kwamba uwekezaji huo ni mkubwa
kufanyika katika utawala wa serikali ya awamu ya tano.
Akitoa taarifa kuhusu uwekezaji
huo, Karim alieleza: “Kumekuwepo na mafanikio chanya katika utoaji huduma na
mpaka sasa imefanya upandikizaji wa figo kwa wagonjwa 7 uliofanyika kwa
mafanikio makubwa huduma ambayo awali ilikuwa ikifanyika nje ya nchi.
Zaidi alisema, “Kwa sasa
hospitali hiyo ina kitengo cha wagonjwa wa ajali ambacho ni maalumu kwa
majeruhi hasa ikizingatiwa Dodoma ni mkoa ulio katikati ya nchi kwa hiyo
itakuwa rahisi kuhudumia watanzania kutoka maeneo mbalimbali ya nchi.”
Kwa mujibu wa sera ya taifa ya
afya ya mwaka 1990 iliyofanyiwa mapitio mwaka 2007, inaeleza kuwa serikali
itajielekeza katika mabadiliko ya magonjwa yanayotokea, sayansi na tekonolojia,
kwa kuwa serikali inatambua umuhimu wa afya bora kwa wananchi wake kwani afya
bora ni rasilimali muhimu kwa maendeleo.
Serikali inafanya maboresho hayo
ili kwenda sawa na sera hiyo ili kuzingatia dira ya maendeleo ya taifa ya mwaka
2025 na malengo ya milenia.
Pamoja na mambo mengine,
serikali inaelezwa kuwekeza rasilimali watu, fedha na miundo mbinu ya kisasa
katika Kitengo cha Kupandikiza Uroto cha Hospitali hiyo ya Benjamin Mkapa
ili kukabiliana na ugonjwa wa selimundu.
Mbali na uwekezaji huo, yamo pia
matibabu ya kibingwa ya magonjwa ya moyo ambapo mtaalam mbobezi wa magonjwa
hayo, Dk. Andrew Kasambala alisema kitengo cha moyo kimepanuliwa na kufanyiwa
maboresho makubwa yanayoipa heshima kutokana na shughuli za kibingwa kutoa
matokeo yaliyokuwa yakitarajiwa.
Lucy Baraka aliyemleta mama yake
hospitalini hapo kwa matibabu ya Miguu akitokea wilayani Gairo Mkoani Morogoro
na Kayaya Santa ambao walifika hospitalini hapo kwaajiri ya matibabu wamesifu
huduma zinazotolewa hospitalini hapo huku akiiomba Serikali kuboresha huduma
katika maeneo mengi zaidi ili kuweza kupata matibabu ya uhakika kwa ukaribu
zaidi.
Hospitali hiyo iliyopo kilomita
25 kutoka katika viunga vya Jiji la Dodoma, inafanya upasuaji wa matundu
unaotumia vifaa vya kisasa.
Mwisho
0 comments:
Post a Comment