METDO Tanzania

METDO Tanzania

Monday, September 11, 2017

DAS AWAASA WANAFUNZI WA KIBAHA INDEPENDENT WALIOMALIZA DARASA LA SABA KUACHANA NA MAKUNDI YA VIJIWENI

1
Katibu Tawala wa Wilaya ya Kibaha Sozi Ngate akitoa hotuba yake katika mahafali hayo ya 12 ya shule ya msingi Kibaha Independent yaliyofanyika shuleni hapo
2
Katibu Tawama Wilaya ya Kibaha Sozi Ngate wa kulia akisalimiana na mmoja wa viongozi wa shule hiyo Said  Mfinanga kushoto katika mara baada ya kumaliza kutoa hotuba yake katika sherehe za mahafali hayo.
3
Mwalimu mkuu wa shule ya msingi Kibaha Independent  Charles Majani akitoa maelezo kuhusina na shule hiyo katika sherehe za mahafali hayo
4
mmoja wa wanafunzi waliohitimu darasa la saba katika shule hiyo ya Kibaha Independent  akipokea cheti chake kutoka kwa mgeni rasmi Katibu Tawala Wilaya ya Kibaha Sozi Ngate
6
Baadhi ya wanafunzi wa darasa la saba katika shule hiyo ya Kibaha Independent wakionyesha umahiri wake wa kucheza moja shoo katika mahafali hayo.
PICHA ZOTE NA VICTOR MASANGU
…………………………
NA VICTOR MASANGU, KIBAHA

WANAFUNZI wa shule za msingi ambao wamemaliza darasa la saba wametakiwa kuachana na  vitendo  vya kutumia muda wao kwa  kushinda vijiweni na kujiingiza na utumiaji wa madawa ya kulevya  kwani kufanya hivyo kunachangia kwa kiasi kikubwa  kunapoteza nguvu kazi ya Taifa.

Kauli hiyo imetolewa na Katibu Tawala wa Wilaya ya Kibaha Sozi Ngate ambaye alikuwa mgeni rasmi wakati wa sherehe za mahafali ya 12 ya shule ya msingi ya Kibaha Independent iliyofanyika katika viwanja vya shule hiyo na kuhudhuliwa na viongozi mbali mbali wa dini na serikali .

Sozi alisema kwamba kuwa wanafunzi wa hao ambao wamemaliza darasa la saba kwa sasa wanatakiwa kuzingatia maadili ambayo wamefundishwa na walimu wao wakati wa kipindi chote ambapo  wakiwa shuleni na kuhakikisha wanaepukana kabisa  na tabia ya kujiingiza katika  makundi hayo ambayo hayana faida kwa upande wao.

“Mimi napenda kuwahasa wanafunzi ambao mmemaliza darasa la saba kuhakikisha kuwa  mnazingatia maadili mazuri ambayo mmefundishwa na walimu wenu, na kwamba vitendo vya utumiaji wa madawa ya kulevya nisingependa kuona kabisa mnafikia hatua hiyo kwani kufanya hivyo kunawasababishia madhara makubwa ya kiafya na kutotimiza malengo yenu,”alisema Sozi.

Pia Sozi aliwataka wazazi na walezi kuachana kabisa  na tabia ya kuwaozesha watoto wao pindi wanapokuwa masomoni kwani kufanya hivyo kunawanyia haki yao ya msingi ya  kuweza kupata elimu ambayo ndio ufunguo wao wa maisha.

“Kiukweli mimi sipendi kabisa kuona mzazi au mlezi anaamua kumwezesha mtoto wake na hatimaye anakatisha masomo, hii kiukweli  kwa upande wetu kama serikali hatuwezi kuivulimia kwani ni kiunyume kabisa na sheria kwa hivyo kitu kikubwa ni kuhakikisha mnaendelea kuwapatia malezi bora ili waweze kutumiza malengo yao waliyojiwekea,”alisema Sozi.

Kwa upande wake Mwalimu Mkuu wa Kibaha Independent  Charles Majani alibainisha kwamba wataendelea kushirikiana na serikali ya awamu ya tatu katika kuhakikisha wanaboresha elimu kwa wanafunzi hao ili kuweza kupunguza changamoto mbali mbali zilizopo katika sekta ya elimu

Alisema kwamba katika shule hiyo wameweka mikakati ya kuwajengea uwezo wanafunzi wao waweze kujifunza mambo mbali mbali ambayo yataweza kuwasaidia kufanya vizuri katika mitihani yao na kutimiza ndoto zao waliojiwekea.

Kadhalika aliiomba serikali kuhakikisha wanaiboresha  zaidi mitaala ya kufundishia kwa lengo la kuweza  kuongeza ufanisi zaidi katika suala zima la kuwafundisha wanafunzi ili  waweze kuelewa zaidi na kufanya vizuri katika masomo yao na kuongeza kiwango cha ufaulu.
Share:

0 comments:

Post a Comment

Copyright © WAZO HURU | Powered by Blogger Design by ronangelo | Blogger Theme by NewBloggerThemes.com