Waziri
wa Madini Doto Biteko kushoto na Waziri wa Nishati Dkt. Medard Kalemani wa pili
kushoto wakiangali jambo kwa mshangao mkubwa.
Waziri
wa Madini Doto Biteko akiwa kwenye Machimbo ya Madini ya Viwandani eneo la
Katoro.
Waziri
wa Nishati Dkt Medard Kalemani akizungumza kwenye kikao cha ndani na kamati ya
ulizi na usalama Wilaya ya Bukombe chini ya Mkuu wa wilaya hiyo Said Mtanda.
Kulia kwake ni Waziri wa Madini Doto Biteko.
Waziri
wa Madini Doto Biteko akiwapungia mkono Wananchi wa Bukombe mara baada mkutano
wa hadhara Mjini Bukombe.
Na Issa Mtuwa - Geita
Waziri
wa Madini Doto Biteko amewataka Wachimbaji wa madini nchini kutimiza wajibu wao
kwakuwa serikali imeshatimiza na inaendelea kutimiza wajibu wake kwa wachimbaji
na wadau wengine wote katika sekta ya madini.
Hayo
ameyasema leo tarehe 14/09/2019 katika siku yake ya kwanza ya ziara yake mkoani
Geita wakati akiongea na wachimbaji wa madini ya ujenzi eneo la Katoro. Akiwa
njiani kuelekea Bukombe Biteko aliongea na wachimbaji hao kwa kuwasisitiza
kulipa kodi ya serikali na tozo nyingine kama sehemu ya kutimiza wajibu wao na
kuunga mkono maamuzi ya Rais, Dkt. John Pombe Magufuli aliewasikiliza kiliochao
kuhusu utitiri wa kodi zilizokuwa kero kwa wachimbaji na Rais kuamua kuziondoa.
Biteko
amewaambia wachimbaji madini kote nchini kuwa, kwa sasa ni zamu yao kutimiza
wajibu kwa kulipa kodi, kuunga mkono jitihada alizo zionyesha Rais Magufuli
zilizopelekea mageuzi makubwa katika sekta madini.
Wakati
huo huo Biteko ambae pia ni Mbunge wa Bukombe ameungana na Waziri wa
Nishati Dkt. Medard Kalema katika
kukagua utekelezaji wa ilani ya chama tawala katika jimbo la Bukombe katika
usambazaji wa umeme kwa wananchi. Pamoja na kusikiliza kero za wana Bukombe
kuhusu Umeme Mawaziri hao wamejionea kusua sua kwa usambazaji wa umeme na hatua
iliyofikiwa jambo lililopelekea kung’olewa kwa Meneja wa Tanesco wilaya ya
Bukombe kwa kushindwa kutekeleza wajibu wake.
“Mhe.
Kalemani leo mimi sina cha kuongea ujio wako wana Bukombe wanasubiri kusikia
kutoka kwako umeme utawaka lini, kwani wamekuwa wakikuona kwenye vyombo vya
habari mara Kilimanjaro, Mara Songea,
Mara Tanga ukipita ukiwasha umeme Wanabukombe nao leo wanapenda wakuone
ukiwasha umeme hapa kwao” alisema Biteko Mbunge wa Bukombe huku akishangiliwa
na umati mkubwa wa Wananchi wa Bukombe.
Nae Waziri
wa Nishati Dkt. Medard Kalemani alijibu mapigo ya mbunge wa Bukombe kwa kutolea
majibu kero zote zilizowasilishwa na Biteko kwa niaba ya wananchi wake.
“Mhe.
Waziri, kwanza nikupongeze kwa kazi kubwa na nzuri unayoifanya kwa wananchi
wako. Pili, nimekuja hapa mara mbili na leo mara ya tatu maagizo niliyoyatoa
awali naona hayajatekelezwa, sasa nasema hivii, Meneja wa Tanesco wilaya ya
Bukombe kuanzia sasa namfuta kazi sio Meneja tena wa hapa Meneja wa Kanda tafuta kwa kumpeleka
hapa lete mwingine kesho”
“Pale
sokoni kesho, nasema kesho, ipelekwe Transformer na jioni saa 10 umeme uwake
kwenye maduka ya wafanyabiashara.
Mkandarasi naagiza ifikapo Desemba mwaka huu vijiji vyote 72 vya wilaya
ya Bukombe viwe vimesha unganishwa umeme. Mhe. Biteko mimi sijaja kukaa sana
hapa yangu ni hayo na kama haya yote niliyo yaangiza kwa kila jambo yasipotekelezwa
kwa tarehe zilizo pangwa nipigie simu” alisisitiza Kalemani wakati wa mkutano
wa hadhara na wananchi wa Jimbo la Bukombe.
Kwa
upande mwingine Dkt. Kalemani amemsifu Mbunge wa Bukombe ambae ni Waziri wa
Madini kwa kutoa vifaa 250 bure vya
kuunganishia umeme huku kila kimoja kikigharimu Tshs. 300,000 kila kimoja itakacho
fungwa kwenye nyumba ya ukubwa wa chumba na sebule.
Biteko
yupo kwenye ziara ya kikazi katika mikoa ya Geita, Kilimanjaro na Kagera.
0 comments:
Post a Comment