METDO Tanzania

METDO Tanzania

Wednesday, July 26, 2017

ZIARA YA SHAKA WILAYANI SENGEREMA YAVUNA WANACHANA ZAIDI YA 50 KUTOKA CHADEMA

Na Mathias Canal, Sengerema-Mwanza

Ziara ya Kaimu Katibu Mkuu wa UVCCM Taifa Ndg Shaka Hamdu Shaka (MNEC) Leo Julai 26, 2017 katika Wilaya ya Sengerema Mkoani Mwanza imejihakikishia alama muhimu ya kuungwa mkono na Wananchi wengi hususani vyama vya upinzani.

Katika Ziara hiyo zaidi ya wanachama 50 wamekiaga Chama Cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) na Kujiunga na Chama Cha Mapinduzi kutokana na kuridhishwa na utekelezaji wa ilani ya ushindi ya CCM Mwaka 2015-2020.

Mara baada ya kurudisha kadi za CHADEMA Vijana hao wameeleza kuwa kuhama Chama hicho ni matokeo makubwa ya usimamizi wa rasilimali za Umma na kuongeza uwajibikaji serikalini unayofanywa na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na Mwenyekiti wa CCM Taifa Mhe Dkt John Pombe Magufuli.

Matokeo ya wanachama hao kukiama Chama chao Cha zamani kwa kusema kuwa ni Chama kilichojaa uongo na upotoshaji Mkubwa dhidi ya shughuli zinazofanywa na Rais Magufuli watakuwa mtaji mahiri kwa Chama Cha Mapinduzi CCM kwani kinazidi kujihakikishia jinsi kinavyoungwa mkono na Wananchi wengi pasina kujali vyama vyao.

Hayo yanajili Wakati wa ziara ya siku moja ya Kaimu Katibu Mkuu Wa Umoja wa Vijana wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) Ndg Shaka Hamdu Shaka mara baada ya kutembelea Kijiji cha Nyakutanga, Kata ya Bukokwa alipokuwa akizungumza na Vijana wa Jumuiya ya Chama hicho (UVCCM) pamoja na  wanachama wa chama cha Mapinduzi (CCM) Mara baada ya kufungua shina la wajasiriamali TUJIKOMBOE.

Vijana hao pia wamemuomba Kaimu Katibu Mkuu huyo kufikisha salamu kwa Rais Magufuli kama inawezekana abadili katiba na kuongoza nchi ya Tanzania kwa zaidi ya miaka 25.

Aidha, Wamesema kuwa Kuhama Kwao Chama kumetokana na hamasa kubwa pia unayofanywa na Kaimu Katibu Mkuu wa UVCCM Taifa kwa Ziara zake anazozifanya katika maeneo Mbalimbali nchini kukagua utekelezaji wa Ilani ya Uchaguzi.

Wanachama hao wapya wanafanya idadi wa Wanachama zaidi ya 751 waliojiunga na Chama Cha Mapinduzi (CCM) Kwa mwaka huu 2017 ambapo kati yao wqmejiunga kwenye vikundi saba vya ujasiriamali ambavyo vinajishughulisha navshughuli Mbalimbali katika kujipatia kipato.

MWISHO

Share:

0 comments:

Post a Comment

Copyright © WAZO HURU | Powered by Blogger Design by ronangelo | Blogger Theme by NewBloggerThemes.com