
Waziri wa Elimu, Sayansi na
Teknolojia Prof. Joyce Ndalichako akizungumza wakati wa kufunga
kongamano la Walimu wilayani Kasulu mkoani Kigoma

.Baadhi ya walimu wa Mkoa wa
kigoma wakifiatilia hotuba ya Waziri wa Elimu, Sayansi na Teknolijia
Prof. Joyce Ndalichako wakati akifunga Kongamano la Walimu
lililoandaliwa na Benki ya Biashara ya Walimu, Kasulu mkoani Kigoma.

Waziri wa Elimu, Sayansi na
Teknolojia Prof. Joyce Ndalichako akisalimiana na mmoja wa mwalimu
aliyeshiriki Kongamano la Walimu lililoandaliwa na Benki ya Biashara ya
Mwalimu, Kasulu Mkoani Kigoma.

Waziri wa Elimu, Sayansi na
Teknolojia Prof Joyce Ndalichako akiteta jambo na Mkurugenzi wa Benki ya
Biashara ya Mwalimu Richard Makungwa wakati wa hafla ya kufunga
Kongamano la walimu lililoandaliwa na benki hiyo Kasulu, Mkoani Kigoma

Mkurugenzi wa Benki ya Biashara ya
Mwalimu Richard Makungwa akizungumza wakati wa hafla ya kufunga
Kongamano la walimu lililoandaliwana Benki hiyo Kasulu, Mkoani Kigoma
…………….
Waziri wa Elimu sayansi na
Teknolojia Prof,JOYCE NDALICHAKO ameutaka uongozi wa Benki ya biashara
ya Mwalimu MCB BANK kuboresha huduma za kifedha ikiwemo kuweka vivutio
na masharti rafiki ambayo yatawawezesha walimu nchini kukopa fedha ili
kukuza vipato vyao.
Prof,Ndalichako ametoa wito huo wakati akifunga Kongamano la walimu
wilayani Kasulu Mkoani Kigoma na kusisitiza kuwa matarajio ya
serikali ni kuona benki ya biashara ya mwalimu inakuwa rafiki kwa walimu
nchini kwa kuondoa adha na vikwazo ambavyo kwa muda mrefu walimu
wamekuwa wakikabiliana Navyo katika taasisi mbalimbali za kifedha.
“Benki ya Biashara ya Mwalimu iwe
na ahueni kwa mwalimu anapokuwa ni mteja katika kufanya hivyo walimu
wengi watahamasika kujiunga na benki hii, kupitishia mishahara pamoja na
hata kuchukua mikopo”
Aidha ameutaka uongozi wa Benki
hiyo kusimamia vizuri fedha iliyokwisha wekezwa na walimu ili kuwavutia
walimu wengine ambao bado hawajajiunga na kusisitiza kasi ya uanzishwaji
wa ofisi za benki hiyo katika mikoa yote nchini iongezeke ili kuwavutia
wateja.
” Nafahamu kwamba tayari mnatoa
huduma kidijitali na mnashirikiana na Benki ya Posta kutoa huduma katika
maeneo ambayo hamna ofisi na lakini ni muhimu mkaharakisha uanzishwaji
wa ofisi zenu kila mkoa ili kurahisisha upatikanaji wa huduma,,
Waziri Ndalichako pia amewaasa
walimu nchini kuwa na Utamaduni wa kujiwekea akiba pindi wanapopata
mishahara yao ili iwasaidie kuanzisha miradi mingine ya kiuchumi ambayo
itakuwa mkombozi wa maisha yao pindi wanapostaafu.
“”Walimu tambueni akiba ni kile
kitu unachokiweka kwanza kabla ya kuanza matumizi, lakini watu wengi
wanadhani akiba ni bakaa baada ya matumizi kwa utaratibu huo kamwe
hakutakuwa na kitu kinachobaki,,
Kwa upande wake Mkurugenzi Mkuu wa Benki ya Mwalimu Richard Makungwa
amesema benki hiyo ime endelea kujiimarisha katika kusogeza
huduma kwa wateja wake nakwamba tayari imeanzisha ofisi zake katika
baadhi ya mikoa nchini ikiwemo MBEYA MOROGORO na MWANZA huku ishirikiana
na Benki ya Posta kutoa huduma kwa wateja ambao bado mikoa yao
haijafikiwa.
Amesema katika benki hiyo mwalimu
mmoja mmoja anamiliki hisa takribani asilimia 35.28 huku chama cha
walimu na kampuni yao wakimiliki takribani asilimia 16.17.
” ukiangalia utakubaliana nami
kuwa chombo hiki ni cha walimu na madhumuni yake ni kuwaletea maendeleo
wao wenyewe ndiyo maana tukasema lazima tuwafikia walimu popote walipo
,,alisema Mkurugenzi huyo.
Naye mkuu wa wilaya ya Kasulu
Kanali Simon Anange amesema mara nyingi watumishi wanakosa nidhamu ya
fedha na kutumia zaidi ya kile anachopata na kusisitiza kuwa ni vizuri
walimu wakawa na utaratibu wa kujiwekea akiba ili pindi wanapostaafu
waweze kuishi maisha ambayo wanaishi wakiwa kazini.
Nae mwalimu mstaafu aliyeshiriki
kongamano hilo Kalist Tarimo ameishukuru Benki ya Biashara ya Mwalimu
kwa kufanya Kongamano hilo ili kutoa elimu kwao lakini pia ameishaiuri
benki hiyo kuwana na ofisi katika kila Wilaya ili walimu waweze kutumia
huduma za benki hiyo.
Kongamano hilo limeandaliwa na Benki ya Biashara ya Mwalimu na limeshirikisha walimu kutoka Mkoa wa Kigoma.
0 comments:
Post a Comment