Na Abdul Nondo
Niliwahi kuhojiwa Azam TV, katika kipindi cha morning Trumpet juu ya mfumo wa Udahili wa vyuo vikuu.baada ya TCU kutoa majina ya wanafunzi kuwa wamedahiliwa kimakosa.
Nilikuwa na Dr.wangu wa Chuo kikuu cha Dar, Dr. Berson mhadhiri Wa Chuo Ndaki ya habari Chuo kikuu cha dar.(SJMC).tulieleza kwa undani juu ya UDAHILI WA VYUO VIKUU.
Moja ya swali aliloniuliza ,Nd.Nurdin (mtangazaji), *je,mfumo Wa udahili kupitia TCU unafaa*?
Mimi nilijibu mfumo huu unafaa,ingawa unachangamoto ndogondogo ambazo zinaweza kutatuliwa.kauli ya mh.Rais alikuwa bado hajaitoa kuzuia udahili kupitia TCU .
Sababu nilizotoa kuwa jukumu hili halitakiwi kuhamishwa na kupelekwa Vyuoni ,badala ya TCU ni kuwa mfumo Wa udahili kupitia vyuo ulikuwepo kabla ya TCU, wanafunzi walikuwa wanaomba vyuoni moja kwa moja ,lakini changamoto nyingi zilikuwa zikijitokeza ndipo wakaamua kuunda chombo kitakachokuwa kinasaidia udahili(TCU) ambapo wanafunzi walikuwa wanaomba kupitia mfumo mmoja CAS(central admision system).
1.wanafunzi waliomba kwa sh.elf 50 tuu ,na kuomba vyuo 5.
2.vyuo vyote vilikuwavinapata wanafunzi.
3.wanafunzi wote walipata vyuo kutokana na vigezo vyao .
4.mfumo ulikuwa rahisi saana kwa wanafunzi hata mfumo Wa udahili wenyewe haukuwa nausumbufu.
Kabla ya TCU, kulikuwa na changamoto nyingi ambazo naziona sasa zitaanza ,katika udahili unaofanyika vyuoni. Na hii ni kwasababu mamlaka husika imefanya hivi bila kutoa elimu kwa wanafunzi.namna gani hili litafanyika badala yake kila Chuo kinatoa Muongozo wake.
1.suala la ada ya udahili ,zamani wanafunzi walikuwa wanalipa elf .50 tuu ,kuomba vyuo vyote ila sasa kila Chuo kilianza ada yake ya udahili ,UDSM ilianza na sh.20000/=(Degree),UDOM ilianza na Sh.30000/=(degree),kiujumla hakukuwa Muongozo uliotolewa rasmi juu ya ada sawa ya udahili kwa vyuo vyote , hivyokupelekea wanafunzi wengine kwa hali hii kulipa takribani laki na nusu au laki na 30 , kwa vyuo vyote ,hii ikapelekea wadau kupiga kelele ndipo Serikali kupitia TCU kutoa Muongozo Wa ada elekezi ya udahili sh.elf 10 kila Chuo lakini baada ya wengine kuliwa takribani laki na nusu .hii ni changamoto ya Kwanza.kwamba uamuzi umeanza tolewa vyuo vidahili bila kuwapa maelezo ya ada ya udahili.
2. kuchaguliwa zaidi ya vyuo viwili (multiple selections),sababu wanafunzi wataomba vyuo zaidi ya vitatu,hakuna mfumo Wa uhakika unaotambua mwanafunzi aliyedahiliwa zaidi ya Chuo kimoja ,eti njia ya kutatua hili mwanafunzi anatakiwa Ku confirm (kuthibitisha),chuo alichochaguliwa inaashiria kukubali kuwa amerithia Chuo Fulani ,kama huja confirm (kuthibitisha)Chuo Fulani inamaanisha hujaridhia kuchaguliwa Chuo hiko ila ulicho confirm.elimu hii wanafunzi hawana hivyo ,wengi hawataconfirm Chuo chochote hii itapelekea kukosa Chuo pote sababu haja confirm.,nitofauti na TCU ambapo wajibu Wa mwanafunzi ni mmoja kuomba tuu sio pia kukonifirm .
3.vyuo vingi kukosa wanafunzi hasa ambavyo havina majina makubwa,wanafunzi wengi wanawaza vyuo vya majina UDSM,UDOM,DUCE,ARDHI,MZUMBE,TUMAIN,MUHAS,na IFM,kuna vyuo ambavyo sio vyuo kwa wanafunzi sababu havina jina, hivyo wengi wataomba kwa vyuo hivyo vya majina ,hata kama hawana vigezo .hivyo wanafunzi wengi wata concentrate kuomba vyuo aina moja ,na lazima tujue wanafunzi ni wengi saana na vyuo hivyo vina limit ya admission capacity (limit ya uwezo wa udahili),kutokana na miundombinu ya Chuo na course husika lazima ziweke limit ya idadi ya wanafunzi hivyo wengi waliomba hata kama wanasifa hawawezi kulazimisha kudahili katika vyuo hivyo .
hii ni kwa sababu wengi wameomba ktk vyuo vichache na hii itapelekea wanafunzi kukosa vyuo walivyoomba kwa sababu kuna vyuo kadhaa ambavyo hawakuviomba.
Hivyo wataingia gharama upya ,kuomba katika vyuo ambavyo havina wanafunzi wengi na havikuombwa Mara ya kwanza.hii mwanafunzi atatakiwa kulipa tena ili apate access ya (password)ya kuomba tena ambayo ni gharama na usumbufu kwa mwanafunzi.
Mimi nashauri tuangalie huu utaratibu upya,kwani unachangamoto nyingi hadi sasa wanafunzi wengi hawaelewi chochote vyuo vingi havijafungua tovuti zao,aidha zinasumbua kufanya maombi kutokana na teknolojia ya Chuo husika.
Ni kweli TCU ilikuwa na changamoto zake lakini zitakazo jitokeza ni changamoto kubwa zaidi ya zilizokuwa TCU.
TCU ina shtumiwa kwa kuingia dili na vyuo binafsi kupeleka wanafunzi huko katika vyuo ambavyo sio chaguo lao wanafunzi,lazima tuelewe wanafunzi chaguo lao ni vyuo vya majina na vyuo hivi vina limit ya admission capacity hivyo si kila anaye hitaji UDSM atakuja UDSM hata kama ana one ,wenye one Tanzania ni wengi,sio kila anaye taka UDom atapelekwa UDOM sababu ya limit ya admission capacity ya Chuo husika , kama shutma hii ya TCU ni kweli serikali ingetumia njia yake kukomesha tabia hii, lakini sio kupeleka jukumu hili LA udahili vyuoni.
Abdul Nondo.
0659366125
0 comments:
Post a Comment