Mbunge wa Viti Maalum anayewakilisha
vijana, Mhe Mariam Ditopile amempongeza Rais Dk John Magufuli kwa niaba
ya vijana nchini kwa kuzidi kuondoa kero za usafiri.
Mhe Ditopile ametoa kauli hiyo baada ya
jana Rais Magufuli kuzindua jengo la tatu (Terminal 3) la uwanja wa
ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere jijini Dar es Salaam.
Amesema jengo hilo limeongeza hadhi ya
uwanja huo na kwenda sawa na Uwekezaji ambao umekua ukifanywa na
Serikali ya awamu ya tano chini ya Rais Magufuli.
” Tumeingiza ndege za kutosha na
tunaendelea na Ujenzi mpya na ukarabati/upanuzi wa viwanja vya ndege,
hii inaonesha jinsi gani Serikali yetu imejipanga katika kukuza uchumi
wetu kupitia usafiri wa anga lakini pia uwezo wa ndege zetu kutua katika
viwanja vikubwa vya kimataifa kunaongeza soko la watalii nchini,”
amesema Mhe Ditopile.
Kuhusu usafiri wa Nchi kavu, Mbunge huyo
amesema kuna barabara za kutosha na zenye ubora kwa zaidi ya asilimia 95
Nchi nzima na zimeunganishwa na mtandao wa lami.
” Ujenzi wa reli ya mwendo kasi/Treni ya
umeme (SGR) unaendelea kwa kasi kubwa, Serikali inaenda kuwekeza ktk
reli ya TAZARA*kwa kuboresha miundombinu pamoja na injini na mabehewa ya
kutosha na ya kisasa kwa kushirikiana na wabia wenzetu jirani zetu wa
Zambia,” amesema Mhe Ditopile.
Aidha amempongeza Rais Magufuli kwa namna
anavyoendelea kukarabati vivuko na meli mbalimbali pamoja na kupanua na
kuongeza bandari kavu.
” Kwa haya maendeleo makubwa yanayofanywa
na Jemedari wetu Rais Magufuli hakika kunatupa deni kubwa sisi
wasaidizi wake kuhakikisha tunawatumikia wananchi wanyonge kama ambavyo
yeye mwenyewe Mhe Rais anafanya kwa vitendo,” amesema Mhe Ditopile.
0 comments:
Post a Comment