METDO Tanzania

METDO Tanzania

Thursday, December 16, 2021

WAZIRI NDUMBARO AIBUKA KIDEDEA MICHUANO YA GOLF YA WABUNGE YA AFRIKA MASHARIKI

Waziri wa Maliasili na Utalii, Dkt. Damas Ndumbaro akiwa amepiga mpira wakati wa Mashindano ya Gofu ya Mabunge ya Afrika Mashariki 2021, yanayofanyika katika uwanja wa mchezo huo wa Kili Gof uliopo Usa River jijini Arusha ambapo kwa timu ya wanaume ya Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Ndumbaro ameibuka kuwa mshindi wa jumla kwa wanaume kwa kujipatia pointi 73.
Waziri wa Maliasili na Utalii, Dkt. Damas Ndumbaro akiwa mchezaji mwenzake wakielekea kupiga shimo la 18 katika Mashindano ya Gofu ya Mabunge ya Afrika Mashariki 2021, yanayofanyika katika uwanja wa mchezo huo wa Kili Gof uliopo Usa River jijini Arusha ambapo kwa timu ya wanaume ya Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Ndumbaro ameibuka kuwa mshindi wa jumla kwa wanaume kwa kujipatia pointi 73.

Na Mwandishi wetu, Arusha

WAZIRI wa Maliasili na Utalii, Dkt. Damasi Ndumbaro aibuka kidedea mashindano ya Gofu ya Wabunge ya Afrika Mashariki kwa ushindi wa jumla upande wa Wabunge Wanaume akIwakilisha Bunge la Jamhuri ya Muungano wa   Tanzania.

Waziri Dkt. Ndumbaro amekuwa kinara kwa kupata pointi 73 huku akiwaacha washindani wake kwa kiasi kkubwa 
 Akielezea ushindi huo, Dkt. Ndumbaro alisema kuwa uzoefu na kufanya  mazoezi mara kwa mara vimeweza kumbeba kwa kuibuka mshindi katika mashinadano hayo

“Mchezo ulikuwa na ushindani mkubwa, Kila mmoja wetu  alijipanga kuwa mshindi lakini matokeo mazuri yamekuja Tanzania, Siri ya ushindi wangu ni uzoefu wa mazoezi ninayofanya mara kwa mara.”Alisema Waziri Dkt. Ndumbaro.

Katika matokeo hayo ya Mabunge  Waziri Dkt. Ndumbaro ameibuka mshindi wa jumla katika mashindano hayo

“Mashindano ya Gofu ya Mabunge ya Afrika Mashariki 2021, yanafanyika katika uwanja wa mchezo huo wa Kili Gof uliopo Usa River jijini hapa

Mbali na mashindano ya gofu katika Jiji hilo pia kuna mashindano mengine ya  Mabunge ya Afrika Mashariki yanayoendelea kufanyika katika viwanja mbalimbali Jijini hapa

Bunge la Tanzania liliweza kujikusanyia ushindi wa jumla wa pointi 43.5, huku Kenya ikipata pointi 37, Uganda pointi 35.8 na Wabunge wa Bunge la  Afrika Mashariki ( EALA) waliibuka na ushindi wa pointi 17.7.

“Kipengele cha Wabunge Wanaume ushindi wa jumla ulienda kwa Waziri Dkt. Ndumbaro akiwakilisha Tanzania kwa kunyakua pointi 73 huku ushindi wa Wabunge wanawake Mhe. Neema Mgaya (Tanzania), yeye alipata pointi za jumla 48 zilizompa ushindi upande huo” Ilieleza taarifa hiyo.

Aidha, washindi wengine  kwa Wanawake ni Uganda ilipata pointi 36.2 na Tanzania ikapata pointi 31.5,  Kenya wao walipata pointi 20 huku Bunge la Afrika Mashariki  ( EALA ) likiibuka la mwisho  kwa pointi 16.6.

Ushindi mwingine kwa upande wa Wabunge wa Bunge la  Tanzania upande Wanaume walipata pointi  51.3, Kenya pointi 44.3,Uganda wao pointi 35.4 na kwa Bunge la EALA nao waliibuka na ushindi wa Pointi 19.6.
Share:

0 comments:

Post a Comment

Copyright © WAZO HURU | Powered by Blogger Design by ronangelo | Blogger Theme by NewBloggerThemes.com