Waziri wa Kilimo Mhe Japhet Hasunga (Mb) ametembelea mabanda
ya wanaushirika kwenye “Kijiji cha Ushirika” katika maonesho ya Nanenane
yanayofanyika Kitaifa Mkoani Simiyu ambayo yamefunguliwa rasmi na Makamu wa
Rais Mhe. Samia Suluhu Hassan.
Maonyesho hayo yenye kauli mbiu “Kilimo, Mifugo na Uvuvi katika Ukuaji wa
Uchumi wa Nchi” yanahamasisha ari na hamasa ya uzalishaji wenye tija ili
kufikia uchumi wa viwanda.
Katika
Maonesho hayo, Vyama vya Ushirika wa aina mbalimbali Ushirika wa Mazao (Pamba,
Tumbaku, Kahawa) Ushirika wa Umwagiliaji, SACCOS, Ushirika wa Maziwa, Ushirika
wa Wafugaji Nyuki na Ushirika wa Wavuvi.
Pamoja
na mambo mengine, Tume ya Maendeleo ya Ushirika kwa kushirikiana na wadau,
taasisi zinazoshughulika na masuala ya ushirika inaendesha mafunzo ya Ushirika
katika “Kijiji cha Ushirika” ambapo Wanachama, Viongozi na Watendaji wa Vyama
vya Ushirika wanapa fursa ya kujifunza masuala muhimu ya Ushirika.
MWISHO
0 comments:
Post a Comment