KATIBU Mkuu Wizara ya Mifugo na Uvuvi
anayeshughulikia Mifugo Prof. Elisante Ole Gabriel amesema wizara hiyo
ina mpango wa kuondokana na changamoto ya malisho ya mifugo ambayo
imekuwa ikisababisha migogoro kati ya wakulima na wafugaji.
Prof. Gabriel amesema hayo katika Wilaya
ya Kibaha Mkoani Pwani, kwenye hafla fupi ya kupokea matrekta saba kwa
ajili ya Taasisi ya Utafiti wa Mifugo (TALIRI) pamoja na Shamba la
Malisho Vikuge kupitia mradi wa kuunganisha matrekta wa URSUS-TAMCO
unaofadhiliwa na Serikali ya Poland.
Akizungumza katika hafla hiyo katibu mkuu
huyo amesema matrekta manne ambayo yamenunuliwa na TALIRI kwa njia ya
mkopo wa miaka miwili wenye thamani ya takriban Tshs. Mil 220 na
matrekta matatu ambayo yamenunuliwa kwa fedha taslimu Tshs. Mil 192.1 na
Ofisi ya Msajili Hazina kwa ajili ya Shamba la Malisho Vikuge,
yatatumika kwa ajili ya kilimo kwenye mashamba ya malisho ya mifugo na
kuongeza wingi wa upatikanaji wa malisho na yenye ubora kwa mifugo
pamoja na kuondoa migogoro ya wafugaji kuingiza mifugo yao katika
mashamba ya wakulima pamoja na ufugaji wa kuhamahama kwa ajili ya
kutafuta malisho.
“Wizarani tunataka kuondokana na tatizo
la malisho katika nchi hii ambalo limeainishwa kwenye ibara ya 25 katika
ilani ya uchaguzi ya CCM ya mwaka 2015, changamoto ya malisho ni kubwa
kwa wafugaji tunaamini tutakapoondokana na changamoto ya malisho,
changamoto ya maji tutapunguza kwa kiasi kikubwa migogoro iliyopo,
tutapunguza tatizo la ubora wa mifugo yetu, ndiyo maana tumeamua kuanzia
Shamba la Malisho Vikuge.” Alisema Prof. Gabriel
Katibu mkuu huyo pia ameitaka TALIRI
kuhakikisha matrekta hayo yanatumika ipasavyo kwa ajili ya kuzalisha kwa
kutumia mtaji huo na kulipa deni kwa wakati ili taasisi nyingine za
serikali zilizo chini ya Wizara ya Mifugo na Uvuvi ziweze kunufaika na
mkopo huo ikiwemo Kampuni ya Ranchi ya Taifa (NARCO) ambayo imekuwa na
mashamba makubwa ya uzalishaji wa mifugo.
Kwa upande wake Mkurugenzi wa Shirika la
Maendeleo la Taifa (NDC) Prof. Damian Gabagambi, shirika ambalo
linasimamia mradi wa kuunganisha matrekta wa URSUS-TAMCO amesema faida
ambayo wanataka kuiona kupitia mradi huo hapa nchini ni kubadilika
kutoka kilimo cha mkono hadi kilimo cha kutumia matrekta.
“Serikali ilipoanzisha mpango huu
haikuanzisha ili kupata faida kama wafanyabiashara wengine, faida ambayo
serikali inatarajia kupitia mpango huu ni kilimo kilichobadilika,
kilimo ambacho kinaondoa jembe la mkono kwa hiyo kupitia mradi huu,
serikali imejipanga kupeleka jembe la mkono makumbusho.” Alisema Prof.
Gabagambi
Kwa upande wake Mkurugenzi Mkuu wa TALIRI
Dkt. Eligy Shirima na Meneja wa Shamba la Malisho Vikuge Bw. Richard
Mdegipala wamesema wanatakiwa kuleta mabadiliko katika sekta ya mifugo
hususan kwa kuboresha malisho ya mifugo na kuondokana na tabia ambayo
wafugaji wengi wanatumia kwa miaka mingi ya kutafuta malisho ya mifugo
yao porini.
Aidha wamesema matrekta hayo yatatumika
pia na majirani wa taasisi ya TALIRI pamoja na Shamba la Malisho Vikuge
na kwamba matrekta hayo yatawawezesha kuongeza gawio kwenye mfuko mkuu
wa serikali.
Hadi sasa Shirika la Maendeleo la Taifa
(NDC) kupitia mradi wa kuunganisha matrekta wa URSUS-TAMCO limeshauza
matrekta 413 katika maen
0 comments:
Post a Comment