Naibu Waziri wa Kilimo Mhe Innocent Bashungwa (Mb) akiongoza kikao kazi kilichofanyika katika ofisi za wizara ya Kilimo maarufu Kilimo 1 Jijini Dar es salam leo tarehe 12 Disemba 2018 wakati alipokutana na kufanya mazungumzo na Mkurugenzi wa Ununuzi na Ugavi wa Afrika Mashariki wa kampuni (TBL) Ndg Gareth Da Gee.
Naibu Waziri wa Kilimo Mhe Innocent Bashungwa (Mb) akiongoza kikao kazi kilichofanyika katika ofisi za wizara ya Kilimo maarufu Kilimo 1 Jijini Dar es salam leo tarehe 12 Disemba 2018 wakati alipokutana na kufanya mazungumzo na Mkurugenzi wa Ununuzi na Ugavi wa Afrika Mashariki wa kampuni (TBL) Ndg Gareth Da Gee.
Na Mathias Canal, Wizara ya Kilimo-Dar es salaam
Naibu Waziri wa Kilimo
Mhe Innocent Bashungwa (Mb) amekutana na kufanya mazungumzo na Mkurugenzi wa
Ununuzi na Ugavi wa Afrika Mashariki wa kampuni (TBL) Ndg Gareth Da Gee
kujadili namna ya kufungamanisha Kilimo na Viwanda.
Amesema kuwa kampuni hiyo
inazalisha bia kwa wingi nchini Tanzania hivyo mazungumzo hayo yataongeza
chachu na tija katika kuongeza masoko ya wakulima nchini.
Mhe Bashungwa ameyasema
hayo leo tarehe 12 Disemba 2018 wakati wa kikao kazi kilichofanyika katika
ofisi za wizara ya Kilimo maarufu Kilimo 1 Jijini Dar es salam na kuhudhuriwa
pia na Kaimu Mkurugenzi wa sera na Mipango, Kaimu Mkurugenzi wa idara ya
usalama wa chakula, Kaimu Mkurugenzi wa idara ya maendeleo ya mazao.
Wengine ni Kaimu Mtendaji
Mkuu wa Wakala wa Taifa wa Hifadhi ya Chakula (NFRA), Kaimu Mkurugenzi wa
Taasisi ya utafiti Tanzania (TARI), Kaimu Mkurugenzi wa Benki ya Kilimo (TADB)
na Benki ya Uwekezaji (TIB), Kaimu Mkurugenzi wa Bodi ya nafaka na mazao
mchanganyiko, na Muwakilishi wa Baraza la uwezeshaji wananchi kiuchumi.
Katika kikao hicho Mhe
Bashungwa amesema kuwa mazungumzo hayo yataongeza mtazamo wa jumla kwa wakulima
nchini kujipatia masoko ya mazao ya mvinyo hususani mahindi, Shairi, Ngano,
Sukari na Mtama.
“Alisema kuwa kwa zao la
mahindi pekee nchini wakulima wana ziada ya Tani 810,000 huku bei ikiwa chini
hivyo Bodi ya Nafaka na Mazao mchanganyiko wanapaswa kukutana na TBL ili
kuangalia mahitaji yao kwenye mahindi na kuzingatia ubora ili wakulima waweze
kunufaika na fursa hiyo” Alikaririwa Mhe Bashungwa
Alisema kuwa moja ya
mikakati ya serikali ya awamu tano inayoongozwa na Mhe Rais Dkt John Pombe
Magufuli ni pamoja na kutafuta masoko ya mazao ya wakulima nchini ili wakulima
hususani wa mazao ya shairi, mahindi, ngano, sukari na mtama waweze kunufaika
na kilimo.
Vilevile ameipongeza
kampuni ya Bia ya TBL kwa kuanza kufanya utafiti kwenye zao la muhogo na zabibu
kwani wakulima wa mazo hayo wataongeza uzalishaji wa mazao hayo nchini.
Bashungwa amesema kuwa
serikali inaendelea na mkakati wake wa kuimarisha masoko ya wakulima nchini
ambapo atakutana na kufanya mazungumzo na uongozi wa viwanda vingine.
MWISHO.
0 comments:
Post a Comment