Na Mathias Canal, Wizara ya
Kilimo-Mtwara
Waziri wa Kilimo Mhe Japhet Hasunga (Mb) amesema
kuwa mpaka kufikia jana tarehe 14 Disemba 2018 wakulima 130,163 wamelipwa jumla
ya shilingi 133,259,933.855
Waziri wa Kilimo Mhe Japhet Hasunga ametoa
takwimu hizo tarehe 15 Disemba 2018 wakati akizungumza kwenye mkutano wa
wabanguaji uliofanyika katika Ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Mtwara.
Alisema kuwa katika Mkoa wa Mtwara wananchi
ambao wamekwishalipwa ni 77,055 huku jumla ya fedha iliyolipwa ni Bilioni 80,098,982,060
Katika mkoa wa Lindi tayari wakulima 41,564 wamekwishalipwa
kiasi cha Bilioni 42,502,635,227 huku katika mkoa wa Ruvuma wakulima 11,463 wamekwishalipwa
kiasi cha Bilioni 10,557,222,943
Aidha, Mhe Hasunga amesema kuwa katika mkoa wa
Pwani Milioni 101,091,960 zimekwishalipwa kwa wakulima 81
Alisisitiza kuwa vyama vilivyohakikiwa ni 461
na vilivyolipwa ni 451, ambapo jumla ya Kilo 40,381,798 zilizolipiwa.
MWISHO
0 comments:
Post a Comment