Waziri wa Kilimo Mhe Japhet Hasunga akisisitiza jambo wakati wa kikao cha kazi alipokuwa akizungumza na viongozi wakuu wa vyama vya Akiba na Mikopo (SACCOS) sambamba na Vyama vya Msingi vya Ushirika vilivyopo katika Mkoa wa Mtwara katika ukumbi wa Mkuu wa Mkoa wa Mtwara, tarehe 14 Disemba 2018. (Picha Zote Na Mathias Canal, Wizara ya Kilimo)
Viongozi wakuu wa vyama vya Akiba na Mikopo (SACCOS) sambamba na Vyama vya Msingi vya Ushirika vilivyopo katika Mkoa wa Mtwara wakifatilia hotuba ya Waziri wa Kilimo Mhe Japhet Hasunga akisisitiza jambo wakati wa kikao cha kazi katika ukumbi wa Mkuu wa Mkoa wa Mtwara, tarehe 14 Disemba 2018.
Waziri wa Kilimo Mhe Japhet Hasunga akisisitiza jambo wakati wa kikao cha kazi alipokuwa akizungumza na viongozi wakuu wa vyama vya Akiba na Mikopo (SACCOS) sambamba na Vyama vya Msingi vya Ushirika vilivyopo katika Mkoa wa Mtwara katika ukumbi wa Mkuu wa Mkoa wa Mtwara, tarehe 14 Disemba 2018.
Na Mathias Canal, Wizara ya
Kilimo-Mtwara
Waziri wa Kilimo Mhe Japhet Hasunga (Mb)
ameagiza kurejeshwa ndani ya miezi mitatu madeni yote yaliyokopwa kwenye vyama
vya akiba na mikopo (SACCOS).
Alisema kuwa mwananchi watakaoshindwa kutii maelekezo
hayo katika kukamilisha deni lake ndani ya miezi mitatu hatua kali za kisheria
zitachukuliwa dhidi yao.
“ Nataka kila aliyekopa kwenye Saccos arejeshe
deni lake kwa kufuata utaratibu wa makubaliano na kama wasipotekeleza ndani ya
miezi mitatu niliyotoa serikali itaagiza wahusika wote kukamatwa maana dawa ya
deni ni kulipa” Alisisitiza
Waziri wa Kilimo Mhe Japhet Hasunga ametoa
agizo hilo tarehe 14 Disemba 2018 wakati wa kikao cha kazi katika ukumbi wa
Mkuu wa Mkoa wa Mtwara alipokuwa akizungumza na viongozi wakuu wa vyama vya
Akiba na Mikopo (SACCOS) sambamba na Vyama vya Msingi vya Ushirika vilivyopo
katika Mkoa wa Mtwara.
Kikao hicho kimehudhuriwa pia na Kaimu Mrajisi
wa vyama vya Ushirika nchini, Mkaguzi wa vyama vya ushirika na Saccos, Kaimu
Mrajisi msaidizi wa mkoa wa Mtwara, Wenyeviti na watendaji wa SACCOS pamoja na
vyama vya msingi vya ushirika vilivyopo mkoani Mtwara.
Mhe Hasunga amelitaka Shirika la Ukaguzi wa Hesabu za Vyama vya Ushirika (COASCO) kutimiza
majukumu yake kwa weledi kwa kukagua na kuhakikisha vyama vyote vinafunga
mahesabu huku akitaka vyama ambavyo sio hai kuchukuliwa hatua.
Pia ameagiza kila chama Tanzania kiwe na
daftari la wanachama walio hai na wafu sambamba na kuhakikisha kuwa viongozi
wote wawe na maadili na uwezo wa kuvisimamia vyama vyao ipasavyo.
Katika hatua nyingine alimtaka Mrajis wa
ushirika Tanzania Bw Tito Haule kuwasilisha mpango kazi wa namna ya kukutana na
wanachama wa ushirika nchi nzima katika kutatua changamoto zao. “ Na ni lazima
taarifa itengenezwe ikionyesha idadi ya vyama mlivyokutana navyo na kueleza ni
mambo gani mmezungumza kila mwezi” Alisema
Aliongeza kuwa Viongozi ni lazima kutoa mapendekezo
ya mabadiliko ya sheria ya Ushirika itakayosaidia kuondoa usumbufu kwenye
ushirika ili uendelee kuwa mkombozi wa wananchi. “Mje na mfumo wa namna ya
kuwasaidia wananchi kupata pembejeo bila kuingia madeni yasiyokuwa na tija”
Alisisitiza
MWISHO.
0 comments:
Post a Comment